aseenga
Senior Member
- Jul 13, 2011
- 106
- 86
Wanajamvi salaam! Ni muda mrefu sasa nimekua nikifuatilia kipindi cha 360 katika channel ya clouds fm. Kipindi hicho kinachoendeshwa na babie kabaya, Sam Sasali pamoja na kanjanja mmoja aitwae Hasan Ngoma. Kijana huyu aliletwa katika kipindi hicho baada ya aliekuwa mtangazaji wa kipindi hicho Hadson Kamoga kuchaguluwa na mh. Raisi kuwa mkurugenzi.
Tangu Hassan aje Clouds ameonekana ni mtu anaetafuta nafasi ya uteuzi kwa kusifia na kuongeza chumvi akidhan kwamba labda mh rais atamuona.
Kwa mnaofuatilia mtakumbuka mwanzon kabisa jamaa alikua yupo upande sana wa serekali haswaa kupitia mkuu wa mko wa Dar lakini lilipotokea tatizo la mkuu wa mkoa na Clouds jamaa nae akabadilisha upepo angalau akaanza kuwa neutral.
Leo jamaa kanishangaza sana, wakati wa uchambuzi wa magazeti asubuh ilisomwa habari ya mgongano uliopo kati ya serekali, Tundu Lissu pamoja na starling company. Jamaa anasema "kwa hili nipo tayari kusemwa na watanzania, watu wanasema natafuta uteuzi na nikiri ni kweli natafuta uteuzi na jama mheshimiwa unaniona ni kweli natafuta uteuzi".
Anasema kwamba ni bora serikali ikaongeza kodi eti ili deni lilipwe na ndege zije. Anasema mawakili wawekewe kodi maana wapo wengi jambo litakalosaidia kupata pesa ya ziada.
Sasa mi napata tabu kidogo kuelewa hivi kuna teuzi zinaeza kufanywa kwa mtu kama huyu ambae ni dhahir shahir kabisa ana uwezo mdogo sana katika kufikiri.
Nadhani ni wakati wa chama cha wanahabari Tanzania kuangalia watangazaji wa namna hii. Chama kianze kuhakiki vyeti vya hawa wanahabar kwa kuanza na huyu.
Huyu jamaa anawafanya muonekane vilaza kwa sababu ya maslah yake binafsi.
●NAJUA KUNA AMBAO MNAMJUA ZAIDI. SHUSHA MAMBO HAPA.