Ukamataji wa wasiokuwa na risiti waanza, wafanyabiashara 25 wakamatwa Temeke

lauzi96

JF-Expert Member
Jul 10, 2014
422
797
Ile sheria ya kuhakikisha kila anaenunua anadai risiti imekuwa mwiba kwa wafanyabiashara wilaya ya Temeke maana leo si chini ya wafanyabiashara 25 wamelala chang'ombe wanasubiri kupelekwa mahakamani.

Jinsi walivyokamatwa waliingia maofisa wa serikali kwenye maduka mf sonara anaangalia mzigo wako kama cheni za dhahabu halafu anakuomba risiti ulizonunulia hizo bidhaa kama huna unapelekwa kwenye mikono salama.

Kwa hiyo ndugu zangu fuateni sheria bila shurutu ukinunua mzigo dai risiti.
 
Ili nchi iendelee lazima ifike wakati tuwe na utaratibu maalum wa kimaisha na sio kuishi kiubabaishaji kama hivi. Ukinunua dai risiti na ukiuza toa risiti. Hakuna namna nyingine, hongera Dk Mpango kwa kulisimamia hili watanzania tunathamini sana kazi yako nzuri
 
Watu wengi sasa hivi hawataki risiti kwa sababu wanapata punguzo la kutosha iwapo hawatadai risti,kodi kubwa ya serekali ni mzigo kwa watumiaji(consumers) sababu ya tariff zisizo na kichwa wala mguu ambazo ni kandamizi kwa mtumiaji,pili kodi haimfikii mwananchi wa chini,inaishia kwenye matumbo ya kina MUHESHIMIWA.
 
Ili nchi iendelee lazima ifike wakati tuwe na utaratibu maalum wa kimaisha na sio kuishi kiubabaishaji kama hivi. Ukinunua dai risiti na ukiuza toa risiti. Hakuna namna nyingine, hongera Dk Mpango kwa kulisimamia hili watanzania tunathamini sana kazi yako nzuri
Unampa hongera ili akamue mpaka damu itoke au vipi?.
 
Ile sheria ya kuhakikisha kila anaenunua anadai risiti imekuwa mwiba kwa wafanyabiashara wilaya ya temeke maana leo si chini ya wafanyabiashara 25 wamelala chang'ombe wanasubiri kupelekwa mahakamani,jinsi walivyokamatwa waliingia maofisa wa serikali kwenye maduka mf sonara anaangalia mzigo wako km cheni za dhahabu halafu anakuomba risiti ulizonunulia hizo bidhaa km huna unapelekwa kwenye mikono salama,kwahyo ndugu zangu fuateni sheria bila shurt ukinunua mzigo dai risiti
ninunue alaf nidai risiti, hata pipi nidai risiti, kumbe ii sio nchi ya viwanda tena ni nchi ya kodi?
 
Kwani hiyo sheria ishasainiwa na raisi au ndo mizuka? Kwa maana sheria kupitishwa na bunge bado haijawa sheria hadi mkuu atie saini. Ebu nielewesheni hapo wakuu maana elimu yangu ya hapa na pale ya kuishia la pili b sielewiiiii
 
Wakati Kenya wanaanza zoezi LA EFD kipindi cha Mh Mwaikibaki wakenya walilalamika sana lakini wameshazoea hii imepeleka serikali yao kupata makusanyo mazuri sana kila mwaka nafikiri hata sisi itasumbua lakini ni njia ya kuiwezesha serikali yetu kupata mapato.
 
Back
Top Bottom