Ukaguzi wa magari yafanyike kwa magari yote ya Abiria na ya wanafunzi kuepusha janga jingine

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Kumekuwa na Wimbi kubwa la ukagunzi wa magari yanayobeba wanafunzi sehemu tofauti tofauti katika nchi yetu ya Tanzania. Na matunda yameonekana magari mengi yameonekana hayana sifa na kuzuiliwa na shughuri hiyo ya kuendelea kuwabeba wanafunzi kama ilivyotokea huko Arusha na Mwanza.

Wito wangu kwa Trafiki ni kujikita katika shughuri ya kukagua magari yote ya abiria hata ya watu binafsi kuhakikisha watu wanaotumia vyombo vya moto wanakuwa salama. Kujikita kukagua magari ya wanafunzi halafu tukapoteza abiria 50 kwenye magari haya ya Abiria tutakuwa hakuna chochote tulichookoa.

Wamiliki wa vyombo vya moto wapate Semina ya kutosha wafundishwe kuthamini maisha ya watu zaid kuliko pesa. Maana wamiliki wa magari wamekuwa wagumu kufanya service magari yao matokeo yake kila mara wanabadilisha tu oil basi matairi mabovu wanajikita kujilimbikizia pesa tu.

Rushwa kwa matrafiki ni miongoni mwa sababu kubwa inayofanya kila siku ajali nchini zinaongezeka, Madereva wanaendesha kwa spidi kubwa, leseni hawana, wamelewa lakini utashangaa anasafirisha Abiria toka Dsm mpk songea wakati Njia nzima matrafiki wapo.

Watanzania wenzangi tusaidie serikali katika changamoto hii kubwa za Ajali ya Barabarani katika nchi yetu maana inatuachia majonzi makubwa, inaondoa nguvu kazi, inaacha yatima wengi, inazalisha watoto wa Mtaani kila sehemu.

Trafiki wetu wa Tanzania kwasasa wamejikita kupiga mabao tu mtu kaegesha gari vibaya ndo wanakimbilia huko, mtu hajaripa kodi ndo watakudaka na kukupigania kama mpira wa kona, lakini gari bovu hawana mda huo wapo radhi wachukue 10000 ili wakauawe watu 50. TANZANIA BILA AJALI INAWEZEKANA.
 
Tunahitaji kuwa kama Regulators wa Aviation business.Baada ya uchunguzi wa ajali tuje na maboresho yanayolenga kuzuia aina flani ya ajali
 
Back
Top Bottom