Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Leo siku ya tarehe 24/05/2016. Kamati ya fedha na uongozi, chini ya mstahiki meya manispaa ya Kinondoni, imetembelea Jengo litakalo tumika kufanya huduna za TIKA(tiba kwa kadi) ambapo wazee wote ndani ya manispaa watatibiwa bure, na wananchi wakawaida watachangia 40,000 tuh, kupata kadi zitakazo wafanya watibiwe bure hospitali za manispaa ya kinondoni kwa muda wa mwaka mmoja,ambapo huduma hizo watapata hospitali zote zikiwemo Mwananyamala hosp, sinza palestina hosp,magomeni hosp,Tandale hosp,mabwepande hosp,mburahati hosp,pamoja na zahanati za manispaa ya kinondoni 16,pamoja na ziara hiyo ya kuaarisha miundombinu ya kutoa huduma za afya.
Kamati imeonana na Madaktari na kuwapamoyo juu ya changamoto zinazo wakabili,huku wakihakikishiwa maslahi yao,kama kukoka kwa posho kwa wakati,kupanda madaraja ya ngazi za utumishi kwa wakati,na posho za waredi na zamu kupangiwa taratibu nzuri,kama motisha ya kuongeza bidii kukabiliana na wingi wa wagonjwa wanaohitaji huduma.
Vile vile kamati imekagua ujenzi wa wodi ya mama na mtoto hospitali ya mabwe pande,ambapo shillingi millioni 100,zimetumika kipindi hiki cha january mpaka march,huku madiwani wamekataa kiasi kilicholipwa kwa ukarabati wa barabara ya igesa sinza(makaburini) na ile barabara ya mlandizi(mtogole mpaka kijiweni) kwamba zimelipiwa shillingi millioni 392,kwa matengenezo kinyume na halihalisi