Ukada ndio uliozifanya Shule 7 Kisiwani Unguja kushika nafasi 7 katika 10 za mwisho

Rajab_Omar

JF-Expert Member
May 15, 2016
16,477
27,176
Kwanza Kabisa Natanguliza Shukurani Zangu Zote Kwa Wadau Wa JF.

Ni Masikitiko Makubwa Kwa Wazanzibari Wanaoshuhudia Elimu Ya Visiwani Zanzibar ikiwa Tayari imeshazikwa Kutokana Na Chuki Za Watawala Wa Zanzibar.

Sababu Kubwa Ya Kuzikwa Kwa Elimu Ya Zanzibar Ni Kueka Mbele Ukada/Uccm na Uunguja Kuliko Taaluma Husika. Ni Hii inatokana Na Pale Maafisa Wa Elimu Wa Wilaya, Mikoa na Wizarani Kwa Ujumla Ni Makada Ambao Hawana Taaluma Yeyote Katika Fani Ya Elimu Kwani Wengi Wao Ni Watu Wenye Vijidiploma Vya Miaka Ya 70 na 80 ambao Waliishia Form 3, Bali Wameekwa Kukamata Nyazifa Muhimu Katika Wizara Hiyo Nyeti Ya Elimu Kulingana Na Ukada Wao na Uunguuja Wao.

Kwa Mfano:
Aliyekuwa Waziri Wa Elimu Miaka ya 2006s Mh Haruna Ali Suleima Huyu Aliishia Kufeli Kidato Cha Nne na Akawa Mwalimu Wa Shule Ya Kwao Makunduchi, Lakini Kutokana na Ukada Wa Kupitiliza Baada Ya Muda Kawa Waziri Wa Elimu Na Nikasikia Katunukiwa Digree 2 na Sasa Ana Masta ya Kutunukiwa.

Aliyekuwa Waziri Mnamo Mwaka 2010 mpaka 2015 Mh Ali Juma Shamhuna Na Yeye Aliishia Kidato Cha 4 akadondokea Kadiploma Cha Pale Nkrumah, Lakini Kwa Vile Ni Kada Mkubwa Basi Akaishia Kuwa Waziri Wa Elimu, Hatimae Kaishia Kutoa 7 bora za Mwisho.

Na Waziri Wa Elimu Huyu Tulie Nae Mh Riziki Pembe Naye Ndiyo Huyo Ki.Laza Mwengine Aliyeekwa Pale Kwa Ukada Wake na Wala Si Taaluma Yake.

Kiukweli Zanzibar Tunao Wasomi Wazuri Ambao Ni Maptofessa na Phd lakini Wote Huishia Tanzania Bara au Ughaibuni Kutokana Na sera Mbovu Za Makada Wa Zanzibar Kueka Ukada Mbele Kwenye Kila Jambo.

Wasomi Wangapi Leo Hii Wamedharauliwa Kisa tu ni WAPEMBA, Professa Mnyaa, Professa Mbarawa, Professa Juma Wameonekana Umuhimu Wao Ndani Ya Tanzania Bara, Lakini Haukuonekana Umuhimu Wao Hata Siku Moja Ndani Ya Zanzibar ingawa ni Makada Wenziwai Kisa tu ni Wapemba.

Ni Kituko Cha Ajabu Zanziba Pekee Kwamba Unamkuta Mwalimu Mkuu/Principal Wa Shule Ya Sekondari Ana Elimu Ya Diploma! Hivi Badala Ya Zero Hapa Tutegemee Nini??
Karibuni Vijana Asilimia 90% wa Kizanzibari Wanaofanya Masters na Phd basi Hawarudi Tena Zanzibar bali Huishia Huko Tz Bara Kutokana Sera Mbovu Za Elimu Za Ukada na Uunguja Wa Wazanzibar!
Hata Ukiangalia Maandishi Yao Katika Hile Maskani Ya CCM ya Mwembe Kisonge Pale Unguja Utaona ni Chuki tu Na Ubaguzi ndiyo uliotawala Na Kusahau Jukumu lao La Kuleta Maendeleo! Angalia Hapa King [/QUOTE]


Mfano Katika Shule Kubwa Ya LUMUMBA SECONDARY SCHOOL ambayo Ni Katika Shule Saba za Unguja Zilizoboronga!
Hii Ni Shule Kubwa Kabisa Ya Serikali Pale Unguja Ambayo Ni Kituo Cha Ukada Kwa Ngazi Zote Za Utawala Shuleni Pale, Pale Palikuwa Na Mwalimu Wa Somo la Biology Kwa Kidato Cha 5 na 6 Ambaye Ni Mwalimu Hodari Sana Mwenye Taaluma Ya Ufundishaji na Mfaulishaji, Basi Mwalimu Yule Alifukuzwa Shuleni Pale Kwa Kushutumiwa Kutenda Kosa Ingawa Hakutenda Kosa Na Ndiyo Maana Hakupelekwa Mahakamani Wala Hakufungwa Bali Yupo Huru!! Ukweli Ni Kwamba Huyu Mwalimu Kilichomfukuzisha Pale Ni UPEMBA wake tu Na Wala Si Jengine, Coz Angelikuwa Kada na Muunguja Basi Angelikuepo Pale.
Sasa Shuleni Unaoondosha Waalimu Wajuzi Na Kueka Makada Wasio na Taaluma Tutegemee nini Kama Sio Zero na IV??

Si Kweli Kama Wazanzibari Hatuna Akili, Mbona Tunapoingia Vyuoni Huwa Tunagraduate?? Bali Ni Siasa Za Undumilakuili Zinazochezwa Na CCM bara Dhidi ya CCM Zanzibar za Kuuwa Elimu ili Wazidi Kutawaliwa, Kwani CCM zanzibar itakapokuwa na Wasomi Basi itataka Mageuzi Jambo Ambalo Katu CCM hawataliruhusu.

Kwa Tabia Hii Ya Sekta Ya Elimu Kuongozwa Na Makada badala Ya Wasomi na Wabunifu, Basi tutegemee Zero Kwa Wingi.

Wenzetu Watanganyika Wacha Wawakabidhi Wizara Prof. Sisi tukabidhi Wizara Kada Wa CCM.
 

Attachments

  • Mabango ya Kisonge.pdf
    2 MB · Views: 69
Du ni hatari sana poleni wanzanzibar kwa kuwa wamwisho makada makada hahahahaha hah wameua elimu waliyo wengi watoto wao hawasomi shule hizo wao watoto wao wanasoma nje.
 
Du ni hatari sana poleni wanzanzibar kwa kuwa wamwisho makada makada hahahahaha hah wameua elimu waliyo wengi watoto wao hawasomi shule hizo wao watoto wao wanasoma nje.
Mkuu Unapoingia tu Katika Taasisi Ya Elimu, Basi Cha Kwanza Kabla Ya Kuambiwa Upeleke Academic Certificate, Basi Unaambiwa Upeleke Birth Certificate! Ukionekana Tu Umezaliwa Pemba, Basi unaambiwa Wewe "Chotara" hutufai na Hiyo Phd au Masta Yako.
Wao Makada tu Ndiyo Qualificasions Zao hata Kama Kaishia Kidato Cha Pili Basi Atakuwa Waziri, Mkurugenzi au Mtendaji Wizara ya Elimu. Hatimae anazalisha Zero.
 
Mzururaji
Mkuu Silazimiki Kukujibu Lakini Hayo Unayoyazungumzia Hapa Sio Pahala Pake Zipo Forum Za Kidini Humu Kapeleke Thread Kule Sio Hapa.
Kwanza Kumbuka Hizo Shule 7 zilizoshika Mkia si Za Pemba sisi Hatumo Kabisaa, Bali ni Za Unguja. Sisi Pemba Hatukatai Kuwa Hatujafanya Vibaya ila Hata Kama Hatukufanya Vizuri Sana ila Haijambo Kwani Tumetoa Mpaka Mwanafunzi Mmoja Katika Wanafunzi Kumi bora Tanzania waliofanya Vizuri Zaidi Katika Masoma ya Biashara.
Angalia Hapa S5150/0611 M 6 I
G/STUDIES - 'D'
ADV/MATHS - 'D'
ECONOMICS - 'B'
COMMERCE - 'C'
ACCOUNTANCY - 'A'
Si Lazima uchangie unaweza Kuangalia tu na Kupita. Pathetic fool...
 
Mbona ufaulu katika hizo enzi za mw Harun ulikuwepo.
mbona pia katika kipidi cha mheshimiwa Shamhuna katika hiyo miaka yake ya mwanzo hawakushika hizo namba za kumi kutokea chini!
Halafu mbona mheshimiwa Riziki Pembe kimsingi ana masters! why unapotosha jamii!

kutofaulu kwa wanafunzi katika mitihani yao ya kidato cha sita kimechangiwa pakubwa na CUF! kwani sasa hivi vijana wengi wa kidato cha sita walirubuniwa na CUF kuwa wao niwasomi sana na kwamba watapewa nafasi kubwa na kuongoza nchi endapo CUF itaingia madarakani! matokeo yake wakaacha kushuhulikia masomo na badala yake wakajiingiza kwenye siasa! sasa wacha wavune walichokipanda naiwe nifundisho kwa wengine!

sababu ya pili ni kwamba wanafunzi wengi wa kidato cha sita waliofeli wengi akili zao kama za mtuma post! yaani kiburi na dharau kwa walimu wao na viongozi wao! hapo bado unategemea kutakuwa na ufaulu!

Tatu liko wazi sana yaani niwapenda starehe kuliko kusoma kilasiku wao ni day out tuu!

Nne kutwa wapo kwenye whatsup na face book! wengi wao ni maadimin kwenye whats up na watoa drip na ubuyu wa mtendeni na CUF!

Mheshimiwa Riziki Pembe angalizo kwako tafadhali piga marufuku day out zote za wanafunzi and ongeza muda wa masomo hasa kwa watihaniwa!
 
mbona ufaulu katika hizo enzi za mw Harun ulikuwepo.
mbona pia katika kipidi cha mheshimiwa Shamhuna katika hiyo miaka yake ya mwanzo hawakushika hizo namba za kumi kutokea chini!
Halafu mbona mheshimiwa Riziki Pembe kimsingi ana masters! why unapotosha jamii!

kutofaulu kwa wanafunzi katika mitihani yao ya kidato cha sita kimechangiwa pakubwa na CUF! kwani sasa hivi vijana wengi wa kidato cha sita walirubuniwa na CUF kuwa wao niwasomi sana na kwamba watapewa nafasi kubwa na kuongoza nchi endapo CUF itaingia madarakani! matokeo yake wakaacha kushuhulikia masomo na badala yake wakajiingiza kwenye siasa! sasa wacha wavune walichokipanda naiwe nifundisho kwa wengine!

sababu ya pili ni kwamba wanafunzi wengi wa kidato cha sita waliofeli wengi akili zao kama za mtuma post! yaani kiburi na dharau kwa walimu wao na viongozi wao! hapo bado unategemea kutakuwa na ufaulu!

Tatu liko wazi sana yaani niwapenda starehe kuliko kusoma kilasiku wao ni day out tuu!

Nne kutwa wapo kwenye whatsup na face book! wengi wao ni maadimin kwenye whats up na watoa drip na ubuyu wa mtendeni na CUF!

Mheshimiwa Riziki Pembe angalizo kwako tafadhali piga marufuku day out zote za wanafunzi and ongeza muda wa masomo hasa kwa watihaniwa!

Nadhani Mwakani Badala ya 7, tutegemee Zote 10 za mwisho Zitatoka Unguja.

Yaani Unajiita Una Akili Hali ya Kuwa Unashabikia Watu Kufeli Kwa Maneno Haya "Wacha wavune walichokipanda naiwe nifundisho kwa wengine"!

Halafu Bado Una Hoja Za FaceBook na Watsapp??
Mkuu mimi Nipo Twitter, Intgrm, JF, Facebook, Watsapp, Viber, Ummaland na Kijiwe Mtaani na Out kama Kawa Mbona Sikufeli Mwaka 2011?? Acha Mawazo Mgando hayo! Hapa Pana Watu ni JF-Expert Member na Wapo Chuo Vipanga ile Mbaya.

Hebu Nitajie Shule Ya Secondari Moja tu Hapo Unguja Ambayo Mwalimu Mkuu/Principal Sio Kada Wa CCM??

Je Ualimu Ni Jambo la Ukada??
Na Je Kulingana Na Hoja Zako Kwamba Vijana Wa Advance Walihadaliwa na CUF, hivi Waliofeli hapo Unguja Wote ni CUF??
Kwamana Hiyo Hakukua Na Kijana CCM hata mmoja Ndani ya F6? huoni Kama ni aibu kwa chama tawala hiyo??

Mkuu Waliofeli si Kuwa Wamehadaliwa na CUF kama Unavyoclaim, Bali Wamo Vijana Wengi Mazombi wa CCM ambao Munajiita Hamudanganyiki na Sera Za CUF nao Wamefeli, Sasa Na Hawa itakua Fundisho kwa ccm au??

Mkuu Badilisheni sera za elimu yenu mupate mabadiliko!!!

Kwakweli maelezo yako yananipa wasi wasi kuhusu elimu yako nahisi nawewe unakajinafasi fulani katika Kaserekali kenu kakikada ndio ukapayuka hivyo.
 
Back
Top Bottom