kwa haya makabila tuliyomiks hivi haya sijui kama imebaki tamaduni za kufuata kiviiile!
mfano mimi
mume wangu babake ni mchaga mamake mhaya
mimi mamangu mngoni(aliyelelewa unyakyusani toka ana mwaka)babangu mngoni aliyelelewa dar es salaam toka ana miaka 5 sijui!
hapo unaweza kuimagine hawa cutees wangu nawafundisha utamaduni wa aina gani!
so kwa wakati fulani kulingana na muda tulio nao pengne hili halina nafasi saaaana!
tunaenda kimjini mjini kwa kiasi kikubwa mengne yanabaki kuwa tabia binafsi za mtu sio utamaduni wa kabila husika!
BTW muda si mrefu Kongosho utaniuliza rangi ipi ndo poa kumiski kwenye harusi!
shikamoo ZOMBIE:yo:
ahahahahahhahahhahhahahhaha chezeya zombie wewe!Ha ha ha, very soon
Naona ndimu na embe mbichi zinataka kunihusu
Anyway, ndio maaana nimeandika ukabila/utamaduni, nikijua fika kuna wanaochanganya makabila hata 4 so effect ya kabila inakuwa na nguvu ndogo au msukuma aliyekulia Kanyigo.
Lakini kila mahali wana utamaduni wao athari ya eneo unaloishi "social interactions", je ni busara kuchagua yule mnayekaribiana kwenye hizi social interactions? Kupunguza mikwazo isiyo na mantiki?
Acha ukabila wewe mambo ya kuoana kabila moja cjui utamaduni unafanana yalishapitwa na wakati unapotumia mapenzi kama driving force ya ndoa umepoteza dira..ndoa ni mkusanyiko wa vitu vingi sana..acha ukabila lazima watu tuchangamane..makabila tofauti tofauti ndo vizuri..maana mapenzi nayo hua yanaishaga so watu huishi kwa kulipana fadhila tu amin hivyo..
Acha ukabila wewe mambo ya kuoana kabila moja cjui utamaduni unafanana yalishapitwa na wakati unapotumia mapenzi kama driving force ya ndoa umepoteza dira..ndoa ni mkusanyiko wa vitu vingi sana..acha ukabila lazima watu tuchangamane..makabila tofauti tofauti ndo vizuri..maana mapenzi nayo hua yanaishaga so watu huishi kwa kulipana fadhila tu amin hivyo..
yaniwe acha tu!Yaani mambo ya Konnie ndio yaenda haraka hivyo....loh!!!
Hili suala la mahusiano na ukabila nilishawahi kulichangia hapo kabla.
Kama familia yako inazingatia hayo, ni vyema wana nao kufuata tamaduni hizo.
Ninadhani ni rahisi zaidi kumuelimisha mtu wa utamaduni wako akakuelewa na kuutekeleza kuliko wa kabila lako asieona umuhimu wa tamaduni zako
Juu ya hivyo, ikiwa nyote ni waumini wa "utamaduni wa dunia", sioni vipi utamaduni wa kikabila unaweza kusababisha mizozo kwenye ndoa
Kongosho ,namna unavyoitafsiri dunia,watu na mazingira ni jambo muhimu sana kwenye suala la maisha na ndoa kwa ujumla
'
Kama wewe unadhani ni bora tamaduni yako kuliko mwingine itakudhuru katika namna ya kuwasiliana,kuishi na kuoa/olewa kwenye jamii tuliyomo
'
Kinachotufanya muda huu tunajadili jambo hili ni changamoto ambazo wengine tunaziita matatizo
'
Ni kweli hatuko huru 100%,kumbuka kama hatuko huru ni pamoja katika namna zote mbili,yaani hauko huru kuacha kupractice yaliyo ya tamaduni yako lakini pia hauko huru kuyafanya pia
'
Kuna mambo ambayo ni laana kwenye tamaduni moja lakini ni baraka kwenye tamaduni nyingine
'
Kwa muktadha huu tutake tusitake ni lazima either tukaishi kijijini kama tunazipenda tamaduni zetu au kama tuko mjini tukubali kuacha baadhi ya mambo ya tamaduni zetu ili tujenge mahusiano bora kwa wenzetu wa jamii nyingine
'
Tukishindwa tutakua na wakati mgumu sana,Mungu kuna wakati aliwazuia wana wa Israel kuoa watu wa mataifa kwa sababu kama hizi,lakini baadae ilibidi awaruhusu kutokana na mabadiliko ya nyakati,sasa kama Mungu analiona hilo je mimi na wewe?
'
Tunalazimishwa na nyakati kujifunza tamaduni za watu wa aina zote
'
Leo ukienda Peru utamkuta mchina ameolewa huko,unadhani kungekua hakuna huo muingiliano leo tungejua wahindi wanakula sana pilipili?
'
Leo ukiolewa na mhini u know what to do at least!
Hivi, utamaduni wa kikabila uko evenly distributed duniani?? Hauna 'strata'?
Nilichokusudia kwenye "utamaduni wa dunia" ni ile kutofuata utamaduni wa kabila moja bali kukusanya principles za haki katika tamaduni zozote tu zile duniani na kuzifuata.
Global village,global citizen...
Hata Bible inashauri uoe mtu wa kabila yako.Kumbuka Samson na Delilah.
ndoa za kabila moja ndo mzuka. na ndio mana watu wanaooana makabila tofauti wanatafuta wa kujirusha nao nje ambao pia ni wa makabila yao. kwa mfano mi na mume wangu, kila mmoja anajirusha nje na wa kabila lake. ah ningejua ningeolewa na kabila langu ningekua napata vitu vya home bana