Ujuzi Vs Kazi

Apr 18, 2012
95
213
18403598_1185001774945447_8685659388719766330_n.jpg

Injini ya Meli ya M.V Nansio ilikuwa inagoma kupiga starta (kuwaka) kwa muda wa miezi kadhaa,wamiliki wa Meli walihangaika huku na kule kutafuta mafundi wanaoweza kutatua tatizo wasiweze kuwapata kwani kila fundi aliyejaribu kuichunguza hakuweza kujua tatizo liko wapi.

Baadaye wamiliki wa Meli walipata taarifa kuwa kuna mzee anaujuzi wa kutatua matatizo kama hayo tangu akiwa kijana,

hivyo wale wamiliki wa meli walifunga safari na kumfuata alikokuwa. Mara baada ya kufika kwa yule mzee wakatoa maelezo namna Meli yao inavyosumbua kupiga starta, baada ya hapo yule mzee alichukua mkoba wake wenye vifaa anavyotumia kutengeneza kisha akaongozana nao hadi sehemu iliyokuwepo meli.

Baada ya kufika mzee alianza kuichunguza ile Meli, alipanda juu na kushuka chini mara baada ya hapo akatoa nyundo na kuanza kugonga maeneo fran ya injini, kisha baada ya hapo alichukua nyundo yake na kuirudisha kwenye mkoba wake, then akawaambia sasa mnaweza kuiwasha, wale wamiliki wa Meli hawakuamini kama lile zoezi la kugonga injini kwa nyundo lingezaa matunda ukizingatia lilifanyika ndani ya dakika moja.

Wamiliki wa Meli waliwasha Meli yao na kuona tatizo limetatuliwa kweli, basi wakamfuata yule mzee na kumuuliza bei ya kutengenezea,

Yule mzee akasema Tsh millioni 20 inatosha sana, wale wamiliki wa meli walishangaa wakisema kugonga tuu na nyundo ndani ya dakika moja ndoo unataka tukulipe milioni 20?

yule mzee akawajibu gharama ya kugonga na nyundo ni elfu nne (the 4,000/=) na kujua tatizo lilipo ni milioni kumi na tisa na laki tisa na tisini na sita elfu(Tsh 19,996,000/=)

Mzee aliwakazia macho kisha akawambia kumbukeni hili jambo popote muendako,

Katika maisha nguvu zinaumhimu lakini kujua wapi panahitaji utumie nguvu ndo kitu muhimu zaidi. Wengi wameshindwa kugundua wapi watumie nguvu zaidi ktk maisha yao.
Hiyo hoja iliwaingia sawa sawa walimuita chumba cha hazina wakamlipa kisha mzee aliondoka moyo wake ukiyasifia matokeo ya ujuzi wake kwa furaha tele.
 
Hahahaaaaa., mzee aliwapa jibu ambalo hawakulifikiria kabisa. Nyundo moja ni buku nne tu.

Tukumbuke kuwa maamuzi tunayoyafanya yana gharama kubwa, haijalishi ni hasi au chanya. Hivyo tunapaswa kuwa makini na maamuzi yetu kabla ya kushusha nyundo.
 
Back
Top Bottom