Ujumbe wa Theresa May kwa wanaojiita WANADEMOKRASIA

ggenerale

Senior Member
Jan 20, 2018
178
356
Baada ya kupambana sana, leo tumeshuhudia kitu ambacho inawezekana kwa wana demokrasia wetu kikawa ni ndoto ama kigumu sana kukifanya.

Waziri Mkuu wa kwa Malkia aka Uingereza atangaza kuachia hapo mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kilichonivutia zaidi ni haya maneno aliyosema kwenye hotuba yake

in a democracy, if you give people a choice you have a duty to implement what they decide. I have done my best to do that.

Akimaanisha kwenye demokrasia unapowapa watu/raia uhuru wa kuchagua na wakachagua wanachotaka, basi una jukumu la kutekeleza kile walichochagua/ kutaka....

Hili ni somo kubwa kwa wanademokrasia wengi wanaojiita au kujinadi wanafanya demokrasia huku wakiwa wanaenda kinyume na matakwa ya wale waliowaweka madarakani..

MADARAKA NI MZIGO NA SIO SIFA NA ULAJI...
 
Ulitaka kutushawishi nini kaka
Natamani ningekuwa na nia hiyo ya kutaka kuwashawishi...

Ninachosema ni kwamba wanaosema wao ni wanademokrasia basi wawe wanademokrasia kweli...sio kufanya ubabaishaji
 
Back
Top Bottom