Ujumbe kwa Pengo: Kanisa Katoliki kutokubatiza watoto wa nje ya ndoa hauwatendei haki kiimani

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,545
22,050
Haya maamuzi yanayotolewa na wanaojiita wazee wa kanisa wakati mwingine sio sahihi kabisa. Naomba ujumbe huu uwafikie viongozi wakuu wa kanisa katoliki wapate kulitolea ufafanuzi.

Mara kadhaa nimekuwa nikisikia matangazo kanisani kuhusu ubatizo wa watoto ndani ya kanisa Katoliki kwamba wanaoruhusiwa kupewa ubatizo ni wale watoto wa ndani ya ndoa tu, na wale wasiokuwa ndani ya ndoa ni marufuku kubatizwa! Sasa hivi imekuwa kama sheria; Watoto wa nje ya ndoa hawabatizwi.

Haya mapingamizi huenda yanalengo moja zuri la kuhamasisha watu kufunga ndoa, lakini tumesahau yafuatayo:

1. Kuna watoto wa nje ya ndoa. (Wachepukaji, waliokuwa dini ya wake wengi then wakahamia ukristo, waliobakwa n.k) Hawa watoto hawana kosa.

2. Watoto waliozaliwa na wazazi wao kufariki pasipo ndoa.

***********************

Maandiko yanasema "Waacheni watoto wadogo waje kwangu" watoto wadogo kiimani ni wale wasiomjua Mungu.

Maandiko yanasema pia; "Yesu amekuja Kwa ajili ya wenye dhambi". Kwanini tunawatenga hawa watoto wa nje ya ndoa? Kwanini tunatoa maamuzi ya kibinadamu na si kwa mapenzi ya Mungu?

Tunawafukuza waumini wakabatizwe wapi? Tumesahau ya kwamba maandiko yanasema (Mchungaji) aliwaacha kondoo tisini na tisa na kwenda kumtafuta aliyepotea mmoja? Aliyepotea ni nani ndugu zangu wakristo? Si ni hawa wasiobatizwa! Walio nje ya ndoa, wanaoonekana machoni kwetu wachafu! Sasa iweje sisi tunawafukuza?

Yaani kanisa limekuwa busy kuonea huruma mashoga waliochomwa kama sodoma lakini watu ambao wanaohitaji msaada kidogo tu mnawatenga kuwabatiza lakini michango yao ya fedha kwenye jumuiya mnachukua.

Ujumbe huu ufike kwa viongozi wakuu wa kanisa Katoliki wapate kulitafakari jambo hili: pia usambazeni ili upate kuwafikia walengwa!

Madhara ya kutowabatiza ni haya

1. Kanisa linaacha kazi yake ya kulea watu kiimani na kuwa taasisi ya maamuzi ya kidunia.

2. Kanisa linapoteza hawa waumini kwakuwa wanalazimika kutafta ubatizo katika dini zingine.

3. Kanisa linachangia kuzalisha dhambi katika dhambi kwa waumini kushawishika kutoa Mimba.

4. Kanisa linapingana na maandiko matakatifu.

5. Kanisa linajivua majukumu ya kuchunga kondoo wake!
6. Kanisa linaacha kazi ya uinjilishaji linataka ready made person
 
Mbona Yusuph alizaa na Mariam ambaye alikua ni mchumba... Kama yesu angezaliwa kipindi hiki maana yake asingebatizwa na hao wazee wa kanisa...
Unachokoza watu hapo.wenyewe wanakwambia huyo ni bikira.shauri zako.
 
Wanabatizwa hasa misimu ya sikukuu kama Pasaka na Noel ....muhimu uwe unashiriki kwenye Jumuiya ndogo ndogo za Wakristu.....kama sehemu nyingine hawabatizi haijakaa njema walitakiwa wawe na msimamo mmoja tu
 
Back
Top Bottom