Ujumbe huu uwafikie Madaktari wa Tanzania

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,274
6,592
"Katika mazingira ya sasa kwenye sekta ya afya
huko nchini Kenya, kukubali kuajiriwa nafasi ya
udactari Kule, ni Sawa na uvamizi wa AJIRA za
wenyeji, siyo hivyo tu, Bali ni Sawa na uharamia
dhidi ya UTAFUTAJI WA HAKI YA MADAKTARI
KUDAI HAKI YAO YA KUONGEZEWA MISHAHARA,
zaidi ya yote MADACTARI watakaokubali kuajiriwa
tafsiri yake ni kwamba watakua wameungana na
serikali ya Kenya kuwakandamiza na kuwaonea
madactari wa Kenya!
Na kwa mtazamo wangu madactari wa Kenya wako
sahihi, na kama serikali ya Kenya inaona kiwango
wanachotaka MADAKTARI wao ni kikubwa sana,
basi wangetumia njia sahihi ya kufanya mapatano
ya mezani na siyo hii njia ya kichonganishi
wanayotaka kuitumia.
Kwa wale wanaopenda kusikiliza vyombo vya
habari hasa hasa vya kimataifa bila shak
mtakumbuka wakenya walishawahi mvamia
mkandarasi kisa tu hawakupewa kibarua kwenye
hiyo kandarasi, walifanya uvamizi tena wa vurugu
kubwa!
Natabili kwamba azma ya serikali ya Kenya kuajili
madactari kitoka TANZANIA ikitimia, madactari wa
Kenya watafanya maandamano makubwa sana,
tena maandamano hayo yataungwa mkono na
wanasheria, wapinzani na wazalendo wa nchi wasio
na itikadi.

NB; Hakuna kitu kibaya kama kushiriki kufifisha
juhudi za mtafuta HAKI.
 
Kwani sie tuna reserve ya madaktari mpaka tuwapeleke nje? Au ndio kujifaragua kwa kipuuzi na kutafuta sifa za kijinga
 
Maoni ya moja ya daktari wa Kenya.
6tag-381482445-1473894436140689434_381482445.jpg
 
Kwanza nitashangaa kama kuna daktari atakubali kuajiriwa Kenya kwani hiyo itakuwa ni sawa na kujitoa mhanga
 
Ikitokea daktari wa Tz kauwawa huko katika mazingira tatanishi, vita yaweza tokea.
Madaktari mtakaoajiriwa Kenya muwe na tahadhari. Kumbukeni ninyi mnakuwa cheap labour na mnanyang'anya haki na kipato cha wenzenu
 
Wewe unaitwa deadbody na avatar yako inaonyesha uko kwenye ardhi ya Kenya. Nia yako ya kuwatisha madaktari toka Tz wasije Kenya inajulikana. Serikali ya Kenya imeomba madaktari pia toka nchi zingine kama Cuba na China? Jee na hao mtawafanyia hivo hivo au ni waTz tu?
 
We have misplaced priorities.
Kwa takwimu za WHO za mwaka 2006, Kenya ina madaktari 12 kwa kila watu laki moja. Tanzania tunao 2 tu.

Nani anapaswa kumpelekea mwenzake madaktari kwa takwimu hizo?

Tatizo letu afya sio kipaumbele. Tunashindwa kuajiri madaktari 1500 kwa mwaka pamoja na uhaba mkubwa tulionao.

What a shame!
 
Siamini kama Cuba itapeleka madaktari wao kwa hali ya Kenya kwa sasa.
Viongozi wao wana akili timamu.
 
Wewe unaitwa deadbody na avatar yako inaonyesha uko kwenye ardhi ya Kenya. Nia yako ya kuwatisha madaktari toka Tz wasije Kenya inajulikana. Serikali ya Kenya imeomba madaktari pia toka nchi zingine kama Cuba na China? Jee na hao mtawafanyia hivo hivo au ni waTz tu?
Usijitoe ufahamu ndg yangu kama huwajui Wakenya tuulize sisi tunao interact nao mikoa ya mipakani. Hakika mtafanywa asusa. Kwanza wagonjwa wao hawatawakubali kirahisi; pili mnatumiwa kama mamluki kupigana jtk mazingira msiyoyajua
 
Isije tokea vurugu kama za Africa kusini ambapo wananchi wa huko walidai kuwa wageni wanachukua ajira zao
 
We have misplaced priorities.
Kwa takwimu za WHO za mwaka 2006, Kenya ina madaktari 12 kwa kila watu laki moja. Tanzania tunao 2 tu.

Nani anapaswa kumpelekea mwenzake madaktari kwa takwimu hizo?

Tatizo letu afya sio kipaumbele. Tunashindwa kuajiri madaktari 1500 kwa mwaka pamoja na uhaba mkubwa tulionao.

What a shame!
Ukisema kila madaktari wawili wanatibu wagonjwa laki moja maanake kwa watu milioni 45 waliopo tz tuna madaktari wapatao 900?
 
Back
Top Bottom