Ujue ugonjwa hatari wa ebola

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,397
33,267
UJUE UGONJWA HATARI WA EBOLA



images

EBOLA:
Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “EbolaVirus”.Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinazosababisha kutokwa na Damu mwilini,(Viral Haemorrhagic Fevers)Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa huu hakijulikani.Hali inayosababisha mlipuko wake pia haijulikani.Ugonjwa huu pia hauna tiba wala chanjo.Hata dawa za jadi hazijathibitika kutibu ugonjwa huu.


url



Dalili za Ebola
Dalili za ugonjwa huu ni:-
· Homa kali,inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua,njia ya haja kubwa na dogo,mdomoni,masikioni,machoni n.k.
· Kutapika damu
· Kuharisha damu
· Fizi kuvuja damu
· Kutokwa na damu na kuvia chini ya ngozi.Kwasababu ya kutokwa na damu sehemu za haja kubwa nandogo,choo namkojo pia vitaonekanakuwa na damu.



Kuenea kwa Ebola.
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kupita njia mbali mbali.
Njia hizi ni:-
· Kuingia mwilini au kugusana na:-​
· Mate​
· Damu​
· Mkojo​
· Machozi​
· Kamasi​
· Majimaji mengine ya mwili,ikiwa ni pamoja na jasho.​
· Kugusa mtu aliyekufa kwa ugojnwa wa Ebola​
· Kushika/kugusana na wanyama jamii ya nyani.​
· Kuchomwa na sindano au vifaa ambavyo havikutakaswa​
· Uginjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.​
· Kugusa taka ngumu au maji taka yaliyotokana na kumhudumia mgonjwa Ebola.​
Athari za ebola
· Unasambaa kwa haraka sana​
· Unasababisha vifo vingi kwa muda mfupi​
· Jamii huingiwa na hofu na wasi wasi na kushindwa kufanya shughuli zao za kawaida​
· Ni gharama kuwahudumia/kutibu wagonjwa.​
· Mipaka inaweza kufungwa na watu wakashindwa kusafiri kutoka eneo/nchi moja hadi nyingine.​
Kinga ya Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika.Ni muhimu hapa tuweke mikakati thabiti inayotekelezeka ya kukinga na kudhibiti ugonjwa huu mapema.


Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu:-
· Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate,damu,mkojo,jasho,kinyesi,machozi na maji majimengine yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.
· Kwa kuwa ugonjwa huupia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana,epuka kuwa na mpenzizaidi ya mmoja.
· Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtummwnye dalili za Ebola
· Kuwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu.
· Wananchi wanatahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa kwa Ebola;badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
· Kufanya ufatiliaji madhubuti wa ugonjwa huu.
· Wananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola
· Zingatia usafi wa mwili na tabia na kiroho.
KUMBUKA
Ugonjwa wa Ebola ni hatari sana.
Unasambaa haraka na unasababisha
Madhara na vifo vingi.
Epukana nao
 
Thanks kwa elimu hii nzuri, but nilikuwa Kagera kipindi fulani wakati ugonjwa huu ukisemekana kutokea Uganda, na watu walikuwa wanasema kwamba kuna kabila fulani huko ndani ndani kwenye vijiji vya uganda huwa wanapenda kula nyani na ndo wanapata huu ugonjwa sijui ni kweli.

Ni hatari na inaogopesha sana.
 
Huu ugonjwa ni hatari sana! Ukikupata unatapika damu na kuharisha damu hadi unadanja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom