Ujio wa Kinana, CHADEMA imeshinda

Ujio wa Kinana, CHADEMA imeshinda

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,018
Reaction score
20,489
Uteuzi wa Kinana ndani ya CCM, una sura nyingi na ni kamali ya mwisho kabisa kwa siasa za Lumumba. Naweza kusema haya nikijenga hoja katika mambo makuu matatu hivi. Mosi ni Uwezo wa Kinana katika eneo la siasa, Pili Uzoefu wa Kinana Katika kisiasa, Na Tatu ni mazingira ya kisiasa na kidunia.

Hoja ya Kwanza ya Kinana ya Uwezo wake katika siasa, haina mfano ndani ya Chama cha Mapinduzi, Kinana alifanya mapinduzi makubwa ndani ya CCM 2014/15 kwakutumia mbinu muhimu inayoitwa Spin Doctor ambayo ni taaluma ya juu sana katika Ujasusi na ili mtu ujifunze ni lazima uwe na kipaji cha hali ya juu cha maswala ya kubadili nyeusi kuwa nyeupe, ambacho kimsingi mtu huzaliwa nacho.

Kwa tafasiri pana ya kikoloni Spin doctor nikuwa, In politics, a spin doctor is someone who is skilled in public relations and who advises political parties on how to present their policies and actions. Synonyms: PR person, publicist, propagandist,

Hivyo kwa suala la Uwezo wa Kinana kisiasa si wakutiliwa mashaka ndani ya chama chao, Ikikumbukwa kwamba Katibu Mkuu wa CCM sasa Ndugu Chongolo alikuwa msaidizi muhimu wa Kinana katika utumishi kipindi cha siasa za hoja 2013/15, na Sasa wamekutana. Kwaujumla Kinana ni oldest Propagandists mkubwa aliyefunzwa kijamaa toka kwa majasusi wa Kibulgaria na Kirusi ambapo siasa za zamani za kijamaa ziliendana na taaluma hii hasa katika nchi ambazo chama kimeshika hatamu.

Hoja ya pili kwa Kinana inayohusu Uzoefu katika Utendaji wa Kisiasa si nzuri kwasabu Kinana amekuwa katika siasa huku akikumbwa na kashfa nyingi kiasi kwamba ameshindwa kujisafisha hali inayotafsiriwa tangu aingie katika siasa amekuwa na uwezo mdogo wa kujibu hoja ukilinganisha na uwezo wake mzuri wa kuanzisha agenda za kipropaganda. Kwatafsi hii tunaweza kusema CCM haijatibu chama kuwa cha Siasa, ila imejaribu kukiondoa chama kuwa cha kidikteta na mauaji na kukipeleka kuwa chama cha Waongo na walaghai (Propagandists party), Swali ni Je dunia ya sayansi na teknolojia bado kuna vyama vya kuhubiri uongo vikaaminika na jamii inayoshinda kwenye internet masaa 24/7 na inajua kila kinachoendelea duniani? Jibu jepesi ni hapana. Hivyo ujio wa kinana ni mahangaiko ya ccm katika kujinusuru.

Hoja ya Tatu ya Mazingira ya kisiasa na kidunia, nitafafanua kwakusema, Tanzania mpya imekuwa na Morden Spin Doctor wazuri wa kizazi kipya, hii ni aina mpya ya propaganda ambazo ni tofauti kabisa na zile za akina mzee Kinana, Hizi zinahusu Hoja na facts, na matumizi makubwa ya teknolojia tu, "In this regard, modern propaganda is highly network-centric in the way technologies and methodologies are used and adapted to exploit ..." Kinana anakuwa nje kabisa ya hoja hii na kwa ccm simuoni mtu wa kukaa katika hoja hii.

Katika hoja hii ya Morden Spin Doctor, hapa ndio unakutana na kizazi cha siasa za Upinzani ambako wengi hawakubaliani na siasa na mwenendo wa CCM na wameamua kutafuta majukwaa mengine kama Chadema ili kuelezea misimamo na matamanio yao katika nchi yao. Mathalani kuna Freeman Mbowe huyo ni mtaalamu wa siasa za kisasa ambazo zinataka majawabu sio majibu, Tundu Lissu huyu ni Scholer wa leo ambe nyeusi anaiita nyeusi hapaki rangi wala hafumbwi mdomo, John Mnyika huyu anaamini moja jumlisha moja ni mbili na sio moja wala kumi na mboja, kuna Godbless Lema, Heche, Salumu Mwalimu nk.

Kinana ni mzuri wa kuanzisha hoja, kijasusi tunaita Proactive, lakini ni mbovu haijapata kutokea kwenye kujibu hoja ama kijasusi tunaita reactive, Sasa kwenye modern political ili ushinde dunia hii ya utandawazi ni lazima uwe Proactive & Reactive kama alivyo Mbowe au Lissu au zamani alivyokiwa Dr Slaa au yule Mch Gwajima wa zamani.

Fikiria Kinana 2025 aje na hoja akiwaambia Watanzania kwamba Serikali ya Rais Samia ilifanya makosa sana kuweka tozo kwenye pembejeo ndiomaana bei ya mbelea ilipanda sasa, na kwamba sasa waichague ccm kwakuwa mgombea wao anakwenda kuondoa tatizo hilo. Unadhani atajibiwaje na hawa wanasiasa wasomi wa kileo wanaotaka majawabu sio majibu? Tena hoja hii anaweza kukabidhiwa Malisa GJ tu amjibu Mzee Kinana na ikatosha kabisa kuvunja uongo huo.

Bahati mbaya zaidi katika nchi ya giza, Modern Spin Doctor katika utawala uliopita na hata mindset za wanaccm na vyombo vyao vya dola wanawaitwa wachochezi, hivyo waliaamriwa kushinda polisi, mahakamani na jela na ukibisha sana unazawadiwa kifo. Kwamtazamo wangu, Ujio wa Kinana ni kwamba sasa tutakwenda kuona siasa za aina mbili katika taifa, Kwanza ni siasa za Uongl za Chama tawala, Na Pili ni siasa za Hoja na Ukweli za Chadema ambacho ndio chama pekee Kikuu cha Upinzani Tanzania.

Soma vitabu vya Mtu baada ya Mtu, Ujasusi, Madaraka na Strategy kupitia App bora kabisa ya Vitabu Tanzania kwa 5,000 tu kwa wiki. Nenda Play Store pakua sasa jisajili lipia wiki, mwezi au mwaka ujisomee vitabu vyote Link 👉👉👉Yericko Nyerere App - Apps on Google Play

Contact 0715865544

FB_IMG_1649226648293.jpg
 
Uteuzi wa Kinana ndani ya CCM, una sura nyingi na ni kamali ya mwisho kabisa kwa siasa za Lumumba. Naweza kusema haya nikijenga hoja katika mambo makuu matatu hivi. Mosi ni Uwezo wa Kinana katika eneo la siasa, Pili Uzoefu wa Kinana Katika kisiasa, Na Tatu ni mazingira ya kisiasa na kidunia...
Utapata kandarasi ya kuimaliza CHADEMA. utapata maisha na furaha Nyerere
 
Sijaelewa, kwahiyo unasemaje kushinda huko unamaanisha kuanzia sasa hv tutambue kuwa mbowe ndo raisi na tundu lissu ni waziri mkuu au lissu ndo raisi na mbowe waziri mkuu?!!!
 
Hoja ya pili kwa Kinana inayohusu Uzoefu katika Utendaji wa Kisiasa si nzuri kwasabu Kinana amekuwa katika siasa huku akikumbwa na kashfa nyingi kiasi kwamba ameshindwa kujisafisha hali inayotafsiriwa tangu aingie katika siasa amekuwa na uwezo mdogo wa kujibu hoja ukilinganisha na uwezo wake mzuri wa kuanzisha agenda za kipropaganda.

Kwa tafsiri hii tunaweza kusema CCM haijatibu chama kuwa cha Siasa, ila imejaribu kukiondoa chama kuwa cha kidikteta na mauaji na kukipeleka kuwa chama cha Waongo na walaghai (Propagandists party), Swali ni Je dunia ya sayansi na teknolojia bado kuna vyama vya kuhubiri uongo vikaaminika na jamii inayoshinda kwenye internet masaa 24/7 na inajua kila kinachoendelea duniani? Jibu jepesi ni hapana. Hivyo ujio wa kinana ni mahangaiko ya ccm katika kujinusuru.

Mkuu hukumbuki Mchungaji Msingwa alimuomba msamaha kwa kuzushia
 
mkubwa hivyo app yako mbona hatuwezi kujisajili tatizo nini
Unakwama eneo gani mkuu? Kama unatumia simu ya Android nenda Play store pakuwa jisajili kwakuingiza namba yako ya simu unayotumia kwenye internet, kisha lipia kwakupitia namba hiyo hiyo uliyojisajiri... App itafunguka automatical
 
Uteuzi wa Kinana ndani ya CCM, una sura nyingi na ni kamali ya mwisho kabisa kwa siasa za Lumumba. Naweza kusema haya nikijenga hoja katika mambo makuu matatu hivi. Mosi ni Uwezo wa Kinana katika eneo la siasa, Pili Uzoefu wa Kinana Katika kisiasa, Na Tatu ni mazingira ya kisiasa na kidunia.

Hoja ya Kwanza ya Kinana ya Uwezo wake katika siasa, haina mfano ndani ya Chama cha Mapinduzi, Kinana alifanya mapinduzi makubwa ndani ya CCM 2014/15 kwakutumia mbinu muhimu inayoitwa Spin Doctor ambayo ni taaluma ya juu sana katika Ujasusi na ili mtu ujifunze ni lazima uwe na kipaji cha hali ya juu cha maswala ya kubadili nyeusi kuwa nyeupe, ambacho kimsingi mtu huzaliwa nacho.

Kwa tafasiri pana ya kikoloni Spin doctor nikuwa, In politics, a spin doctor is someone who is skilled in public relations and who advises political parties on how to present their policies and actions. Synonyms: PR person, publicist, propagandist,

Hivyo kwa suala la Uwezo wa Kinana kisiasa si wakutiliwa mashaka ndani ya chama chao, Ikikumbukwa kwamba Katibu Mkuu wa CCM sasa Ndugu Chongolo alikuwa msaidizi muhimu wa Kinana katika utumishi kipindi cha siasa za hoja 2013/15, na Sasa wamekutana. Kwaujumla Kinana ni oldest Propagandists mkubwa aliyefunzwa kijamaa toka kwa majasusi wa Kibulgaria na Kirusi ambapo siasa za zamani za kijamaa ziliendana na taaluma hii hasa katika nchi ambazo chama kimeshika hatamu.

Hoja ya pili kwa Kinana inayohusu Uzoefu katika Utendaji wa Kisiasa si nzuri kwasabu Kinana amekuwa katika siasa huku akikumbwa na kashfa nyingi kiasi kwamba ameshindwa kujisafisha hali inayotafsiriwa tangu aingie katika siasa amekuwa na uwezo mdogo wa kujibu hoja ukilinganisha na uwezo wake mzuri wa kuanzisha agenda za kipropaganda. Kwatafsi hii tunaweza kusema CCM haijatibu chama kuwa cha Siasa, ila imejaribu kukiondoa chama kuwa cha kidikteta na mauaji na kukipeleka kuwa chama cha Waongo na walaghai (Propagandists party), Swali ni Je dunia ya sayansi na teknolojia bado kuna vyama vya kuhubiri uongo vikaaminika na jamii inayoshinda kwenye internet masaa 24/7 na inajua kila kinachoendelea duniani? Jibu jepesi ni hapana. Hivyo ujio wa kinana ni mahangaiko ya ccm katika kujinusuru.

Hoja ya Tatu ya Mazingira ya kisiasa na kidunia, nitafafanua kwakusema, Tanzania mpya imekuwa na Morden Spin Doctor wazuri wa kizazi kipya, hii ni aina mpya ya propaganda ambazo ni tofauti kabisa na zile za akina mzee Kinana, Hizi zinahusu Hoja na facts, na matumizi makubwa ya teknolojia tu, "In this regard, modern propaganda is highly network-centric in the way technologies and methodologies are used and adapted to exploit ..." Kinana anakuwa nje kabisa ya hoja hii na kwa ccm simuoni mtu wa kukaa katika hoja hii.

Katika hoja hii ya Morden Spin Doctor, hapa ndio unakutana na kizazi cha siasa za Upinzani ambako wengi hawakubaliani na siasa na mwenendo wa CCM na wameamua kutafuta majukwaa mengine kama Chadema ili kuelezea misimamo na matamanio yao katika nchi yao. Mathalani kuna Freeman Mbowe huyo ni mtaalamu wa siasa za kisasa ambazo zinataka majawabu sio majibu, Tundu Lissu huyu ni Scholer wa leo ambe nyeusi anaiita nyeusi hapaki rangi wala hafumbwi mdomo, John Mnyika huyu anaamini moja jumlisha moja ni mbili na sio moja wala kumi na mboja, kuna Godbless Lema, Heche, Salumu Mwalimu nk.

Kinana ni mzuri wa kuanzisha hoja, kijasusi tunaita Proactive, lakini ni mbovu haijapata kutokea kwenye kujibu hoja ama kijasusi tunaita reactive, Sasa kwenye modern political ili ushinde dunia hii ya utandawazi ni lazima uwe Proactive & Reactive kama alivyo Mbowe au Lissu au zamani alivyokiwa Dr Slaa au yule Mch Gwajima wa zamani.

Fikiria Kinana 2025 aje na hoja akiwaambia Watanzania kwamba Serikali ya Rais Samia ilifanya makosa sana kuweka tozo kwenye pembejeo ndiomaana bei ya mbelea ilipanda sasa, na kwamba sasa waichague ccm kwakuwa mgombea wao anakwenda kuondoa tatizo hilo. Unadhani atajibiwaje na hawa wanasiasa wasomi wa kileo wanaotaka majawabu sio majibu? Tena hoja hii anaweza kukabidhiwa Malisa GJ tu amjibu Mzee Kinana na ikatosha kabisa kuvunja uongo huo.

Bahati mbaya zaidi katika nchi ya giza, Modern Spin Doctor katika utawala uliopita na hata mindset za wanaccm na vyombo vyao vya dola wanawaitwa wachochezi, hivyo waliaamriwa kushinda polisi, mahakamani na jela na ukibisha sana unazawadiwa kifo. Kwamtazamo wangu, Ujio wa Kinana ni kwamba sasa tutakwenda kuona siasa za aina mbili katika taifa, Kwanza ni siasa za Uongl za Chama tawala, Na Pili ni siasa za Hoja na Ukweli za Chadema ambacho ndio chama pekee Kikuu cha Upinzani Tanzania.

Soma vitabu vya Mtu baada ya Mtu, Ujasusi, Madaraka na Strategy kupitia App bora kabisa ya Vitabu Tanzania kwa 5,000 tu kwa wiki. Nenda Play Store pakua sasa jisajili lipia wiki, mwezi au mwaka ujisomee vitabu vyote Link 👉👉👉Yericko Nyerere App - Apps on Google Play

Contact 0715865544

View attachment 2177625
well narated
 
Back
Top Bottom