Ujinga wa Watanzania utawatafuna mpaka kaburini!

Ujinga wa Watanzania utawatafuna mpaka kaburini!

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,393
Reaction score
4,086
Kwa kuwa Idadi kubwa ya Watanzania tumeamua kuwa wajinga basi tujiandae kutafunwa na ujinga wetu mpaka siku tunazikwa.

Watanzania tulio wengi tumekubali kupangiwa lila kitu na kikundi cha watu wachache wenye akili zao. Leo Waziri wa Fedha anasema Wananchi ndio Walitaka Tozo. Leo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anasema Mkoa wa Mbeya unafurahia Tozo, halafu leo CCM eti inaiagiza Serikali iangalie swala la Tozo wakati Wabunge wake ndio waliopitisha Tozo baada ya Serikali ya CCM kupeleka Muswada wa Tozo Bungeni na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kusaini.

Watanzania ujinga wetu ndio unatuponza ndio maana Hayati Rais wa Kenya aliwahi kumwambia Hayati Baba wa Taifa kuwa anatawala maiti. Maiti unaweza kuifanya utakavyo ndivyo Watanzania wafanyavyo na CCM serikali yao.

Hakuna Ajira, matozo kila kukicha, bidhaa zote zipo juu, mafuta ya kula, sukari mchele vyote juu, Petrol ipo juu, madawa gharama watanzania wapo kimya kama maiti hawataki au wanaogopa kudai haki zao hakika ujinga wetu utatutafuna mpaka kaburini.

JamiiForums2096221206.jpg
JamiiForums-1818296427.jpg
 
Bahati mbaya hata wewe mwenyewe umekuwa jasiri nyuma ya key board! Ukikutana live na wale jamaa waliofundishwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili, utajikuta na wewe unakuwa mpole tu kama Eric Kabendera.

Binafsi naona muda bado haujawadia! Ukiwadia tu kila kitu kitakaa sawa. It is just the matter of time. Hakuna aliyeumbwa kuwa mjinga milele. Kuna siku tu tutatoka huko tuliko sasa.
 
Ameen mkuu, huyu mtu aliyewafanya watanzania kuwa mazuzu ni mwongo na mchawi mkubwa, binafsi sio zuzu kabisa.
 
Hata kuandika herufi kubwa ni Ujinga.
Viongozi wa Jamiiforums wanakazi ya kuhariri uandishi wa aina hii.
 
Kupigania haki Tanzania ni sawa na kuomba maji jangwani, vyombo vyetu vya sheria vinaendeshwa chini ya matakwa ya viongozi na sio katiba.
Muangalie Lissu, alipambania sana kufuata sheria, Ila mwisho wote tunajua aliishia wapi.

Tanzania itakuwa huru,siku mihimili yetu ikiweza kujitegemea katika kufanya maamuzi na kujiendesha, kinyume na hapo wenye nchi wataendelea kutamba sanaa.
 
Bahati mbaya hata wewe mwenyewe umekuwa jasiri nyuma ya key board! Ukikutana live na wale jamaa waliofundishwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili, utajikuta na wewe unakuwa mpole tu kama Eric Kabendera...
Watanzania Siyo wajinga by Shujaa Maguful
 
Bahati mbaya hata wewe mwenyewe umekuwa jasiri nyuma ya key board! Ukikutana live na wale jamaa waliofundishwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili, utajikuta na wewe unakuwa mpole tu kama Eric Kabendera...
Upole ukipita kiasi ni Ujinga na ndio maana kenyatta alituita Maiti
 
Yahitaji moyo wa chuma kupingania haki kwa watu wasio jitambua Kama Watanzania angalia mfano hata humu JF,baada ya vyama vya upinzani kukaa kimya hasa CDM kuhusu tozo kulikuwa na thread nyingi za kutoa lawama kwa mwenyekiti Mbowe kwa ukimya wake lakini Mbowe alipo jitokeza kuongea kuhusu tozo thread zikabadilika kutoka kwenye kulaumu mpaka kuanza kumnanga kwamba asali imekwisha ndioa maana kajitokeza kusema kitu,watu wa aina hii hata hawajui wanataka nini Ni vilaza na mazuzu.

Wanacho shangilia na kukipenda ni hiki mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi kupitia kamati ya chama inaitaka serikali kuangalia suala la tozo ambayo serikali inaongozwa na mwenyekiti wa chama mwisho mwenyekiti wa chama ambaye ni rais ataamua kuhusu tozo ambazo alipitisha yeye mwenyewe na mwisho atapewa jina la mtetezi wa wananchi yaani ni zile zile drama na siasa za maji taka ndani ya nchi hii za kutengeneza tatizo Kisha kulitatua mwenyewe ili upate sifa toka kwa wajinga
 
Mkuu

Jitahidi kuielewa Tozo!!

Unafikiri alieanzisha Tozo ni Mama!!?au Mwigulu!?

Makinika!nchi yetu inapitia kipindi cha mpito baada ya Baba kufariki,kuna matengenezo kufika kule tunapo pataka!!Tozo ni chambo cha matengenezo Hayo katika KIPINDI HIKI cha mpito!!

Mama na Mwigulu wasingeweza kuwaumiza watz kwa Tozo coz wanayasaka Madaraka huko mbeleni yaani 2025-2030!hivyo hawawezi wakera wananchi kwa KIPINDI KIFUPI hivo kutoka SASA!!

Tozo ni kete inayosogezwa Pole Pole kusababisha chaos fulani Ili jambo fulani lipitishwe na wenye Mamlaka walioko juu ya vyeo tuvionavyo!!!

Nadhani nimekupa mwanga kama una swali uliza!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
Kwa kuwa Idadi kubwa ya Watanzania tumeamua kuwa wajinga basi tujiandae kutafunwa na ujinga wetu mpaka siku tunazikwa...
Mkuu, nikweli, kabisa kwamba watanzania wengi bado tumelala, nakubweteka. Ila werevu wanasema kulaumu bila kutoa itimisho sahihi, ya nini kifanyike nayo ni ulemavu wa ubongo.

Nini tufanye kuepuka hali hii inayoendelea kutufanya tuwe maiti tunao tembea.

Tuki_base kwenye kulaumiana wakati Taifa ni letu sote matokeo yake yataendelea haya haya,mpaka mwisho.

Njoo na nini?? itakayo tukomboa kutoka hapo tulipo na hiyo ndiyo real patriotism sahihi.

Ila shukrani kwa hoja nzuri inayo fikirisha
 
Kuandika kwako tu Ni changamoto halafu unatuita watanzania wajinga huku wewe mwerevu ukishindwa kueleweka, Tuache watanzania tuijenge nchi yetu kwa mikono yetu Wenyewe
 
Back
Top Bottom