‘Ujinga’ wa CHADEMA na Katiba Mpya

CHADEMA ni chama cha wachaga tu
 
Hii iwafikie TWAWEZA, ndio watakaowe kutuambia mleta mada ni mtu wa aina gani.
 
Kwa akili kama ya huyu aliyeleta huu uzi, itabidi tuanze kupima akili za wapiga kura kama wanajitambua na ikiwezekana ukitaka kupiga kura lazima ulipe tozo
 
Wewe ndio hata hujui kinachoendelea nchi hii.Wakati mfumo wa vyama vingi unaingia nchini kwetu Mwanzoni mwa miaka ya 90, wananchi wote wa Tanzania waliambiwa wapige Kura na kutoa Maoni Yao kwamba, mfumo wa vyama vingi viruhusiwe Tanzania au tuendelee na mfumo wa chama kimoja Cha CCM? Wananchi wakaamua(kwa ujinga wao au kwa kutokujua umuhimu wa vyama vingi) kwamba Tuendelee na mfumo wa chama kimoja.

Nyerere kwa sababu Yeye alikuwa na akili, Akaona Hawa Wa-Tanzania wangu Ni mazuzu. Hawajui umuhimu na faida ya vyama vingi kwenye siasa. Kwa kuwa Yeye alikuwa Ni Mwenyekiti wa CCM wakati hUO na Mzee Mwinyi alikuwa Rais, Akatumia TURUFU YA UBABA WA TAIFA,akasema na kupitisha kwa nguvu kwamba Tanzania Ni Lazima iwe nchi ya vyama vingi. Vinginevyo isingekuwa Nyerere,Ina maana mpaka leo hii huenda Tanzania ingekuwa nchi ya chama kimoja Cha CCM kisheria.

MIMI NINAAMINI PIA KWAMBA,MAMA SAMIA NI RAIS MWANAMKE MWENYE UWEZO NA AKILI NYINGI KULIKO VIONGOZI WENZAKE WOTE WALIOKO CCM KWA SASA(Ambao wengi Ni wabinafsi na wachumia matumbo Yao na ya familia zao). Huyu mama ndio Nyerere wetu wa wakati huu. Atatuletea katiba mpya ya WARIOBA hata Kama wananchi wengi hawataki kwa sababu ya umbumbu wao.

Mungu wetu Tunakuomba mbariki Rais Mama Samia,mpe Afya njema na maisha marefu Kama ya Yule Malkia Elizabeth wa Uingereza(Aliyekufa hivi karibuni) na Zaidi(kwa mapenzi yako Ee Mungu) Ili aendelee kuwa Baraka kwa mataifa yetu ya TANGANYIKA NA ZANZIBAR.Aminaa.
 
Haikuwa 90%, ilikuwa 80%. Na wala hakukuwa na kura ya maoni bali ilikuwa kamati tu iliyochukua maoni ya wananchi.
 
Wao wanaamini sana kwamba watu wameichoka ccm hivyo automatically hao watu wapo upande wao.
 
Hao wengi wanaopitisha katiba wanapatikanaje? Kama wanapatikana kwa njia khalali sawa, lakin kama wanapatikana kwa hila basi haitokuwa.

Halafu ondoa hiyo mentality ya kuwa kuna anayeomba katiba na mwingine anayeombwa, anayetoa na anayepokea. Hakuna anayeombwa katiba bali ni wananchi wote tunatengeneza katiba kwa ajili ya nchi yetu leo na kesho. Huu ni wajibu wetu sote, kwa hiyo hata kwenye kuunda makundi ya kuja kupitisha katiba ni wajibu wetu sote tuzingatie hilo, lazima ifanyike affirmative action kuona kwamba makundi yanaundwa kwa namna ambayo yatapelekea upatikanaji wa katiba bora ya nchi.
 
Kwa bahati mbaya sana naona kuwa hata sasa tunaye Nyerere na pia tuna Rais wa nchi ambaye ni Samia, sasa sijui kama huyu Nyerere wa sasa atafanya hivyo unavyo wish au atafanya vyengine.
 
Kwa wanao kumbuka maneno yako ni sahihi
 
Nyerere aliruhusu vyama vingi kivipi na wakati katika utawala wake chama kilikuwa kimoja tu ambacho ni CCM.
Mleta mada unaweza kutuambia ni wapi katika utawala wa Nyerere aliruhusu vyama vingi?
Tatizo la JF kwa sasa ni kwamba imevamiwa na watoto ambao hata hiyo historia ya mageuzi ya kuruhusu vyama vingi hawajui na hawafanyi juhudi zozote za kujua.

6 Pack; Rais Mwinyi akiwa mwenyekiti wa CCM, aliongoza upinzani dhidi mageuzi hayo akitumia vyombo vyote vya dola kuhakikisha vyama vingi haviruhusiwi nchini.

Kamati Kuu ya CCM, viongozi na wananchama wa CCM walipinga mfumo huo mpya wa vyama vingi na walitumia vyombo hivyo vya dola kupambana na wana mageuzi.

Vyombo vya habari kama radio ya taifa na magazeti ya serikali yaliendesha propaganda kali yakiwaeleza wananchi hatari ya vyama vingi.

Mifano ilitolewa ya nchi kama Rwanda ya hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kama mfumo wa vyama vingi ungeruhusiwa ndani ya Jamhuri yetu ya Muungano.

Hali hii iliendelea na wanamageuzi wengi walijeruhiwa na kulemazwa na vipigo vya polisi huku Waziri Mkuu John Malecela akiwafananisha na mchwa wa kukanyagwa tu.

Hadi siku Baba wa Taifa, wakati huo akiwa ni Rais Mstaafu alipowaasa CCM akiwaonya kuwa wasiporuhusu kwa amani wawe tayari kuyaruhusu kwa shari.

Ghafla upepo ulibadilika, CCM walinywea pamoja na asilimia 90% ya wananchi kutotaka mfumo huo kutokana na hila na propaganda za CCM kama chama tawala.

6 Pack, usilolijua ni kama usiku wa giza. CCM ilijengwa katika msingi ua uongo, hofu na ufashisti. Hawakutaka democrasia ya vyama vingi wala Katiba huru ya vyama vingi.

Hadi leo CCM wanaogopa hiyo Katiba kama ukoma kwani hayo madaraka wanaamini ni yao na hawapo tayari kuyaachia hata kwa miaka mia kama wanavyodai.
 
he! kumbe vyama vya ushirika ni vya ccm? eti asasi za ccm?! vyama vya wafanyakazi ni vya ccm!?
 
CHADEMA ni chama cha wachaga tu
ndo maana tunashauri hiki chama wakikabidhi kwa watu n makundi mbali mbali ya kijamii,tatizo vijana wanakula ugoro hata kutafuta fursa humohumo kwenye makundi ya ccm hawataki,Mfano kanda ya ziwa kuna vikundi vya uchimbaji madini utakuta wengi wenye vikundi ni CCM ,vijana wa chadema wanakula kahawa na kujitenga,

.sasa ikitokea wawakilishi wa kueleza changamoto za uchimbaji watajitokeza wachimbaji wa ccm ndo watakua wawakilishi kisheria as legall legiltimacy ,MWENZENU HECHE ANAKULA FURSA ZA MADINI KIMYAKIMYA ILA WW KIJANA WA UFIPA UNAHAMASISHWA KUANDAMANA,NA KUDEKI LAMI HUO NI UJINGA,KWA NN HECHE ASIWAUNGANISHE NA HUO MTANDAO ILI MJIJENGE,
 
Mimba yako ina umri gani?
 
Nyerere aliruhusu vyama vingi kivipi na wakati katika utawala wake chama kilikuwa kimoja tu ambacho ni CCM.
Mleta mada unaweza kutuambia ni wapi katika utawala wa Nyerere aliruhusu vyama vingi?
Mkuu mataga ni zero brain
 
Kwa akili kama ya huyu aliyeleta huu uzi, itabidi tuanze kupima akili za wapiga kura kama wanajitambua na ikiwezekana ukitaka kupiga kura lazima ulipe tozo
Wanaopiga kura kwa taarifa yenu ni wale wanaokopshwa fedha kwa riba nafuuu kabisa,na wanavikundi vya ujasilia mali vinavyotambulika,shida inakuja mnposima kwenye majukwaa na kusema serikali haitoi mikopo ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…