Ujinga ni kutumia mbinu ile ile!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,533
NAwasikitikia sana wabunge wa upinzani kudhani kwamba kwa kutumia mbinu ya vituko,kelele au vihoja inaweza kufanikisha hoja zao ...hii ni mbinu ya kitoto na iliyoshindwa sio hapa Tanzania tu bali duniani kote!

Jengeni hoja zitakazowaunganisha na wabunge wa CCM kuibana serikali kwa manufaa ya umma...hizi comedy na vihoja waachieni kina majuto na Zembwela...bungeni tunataka weledi wa hoja na ushawishi....

mawaziri hawawasilishi hoja zao kwa vihoja...sio kwamba hawawezi kufanya bali wanatumia karama yao ya ushawishi kuwashawishi wabunge wengi na wananchi wengi juu ya kile serikali inachokiamini.

Wabunge wa upinzani wamekuwa kama wabunge wa 2nd hand yaani waziri au serikali haiwezi kufikiria hata chembe kuchukua hoja zao kwani hata uwasilishaji tu imekuwa ni tatizo.

Mimi niko jimboni nasubiri maendeleo na sio idadi ya miongozo iliyoombwa na mbunge!!

MBINU YA KUSUSA AU KUPIGA KELELE HAIWEZI KUSHINDA ...TALK AND PRESENT SENSE ILI TUWAKUBALI!!
 
Mbona na wewe unatumia mbinu ileile ya uandishi wa mahaba ya lichama lenu, kwa hiyo na wewe ni zuzu?
 
Inakuhitaji uwe na akili za bangi na konyagi kujadili mustakabali wa Taifa na watu wa ccm
 
Back
Top Bottom