Ujinga huu utatuisha lini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujinga huu utatuisha lini.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 3, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtu mzima sasa,wa takriban miaka 53.Nimesoma kidogo, kiasi cha kuwa na degree ya pili katika fani ya kilimo.Lazima niseme ukweli kwamba nimesoma vitabu vingi,majarida ya aina mbalimbali nakadhalika.Sijapata ushashidi wowote wa maana kwamba kuna nchi yeyote imeweza kupiga hatua kimaendeleo kwa kutumia misaada.Naomba kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi huo alete.Mexico inatajwa kwamba kidogo imejitahidi,lakini sina ushashidi wowote kwamba hayo maendeleo uchwara iliyo nayo yametokana na misaada.Sasa kama hali ndiyo hiyo, huu ujinga na ulimbukeni wa kushabikia Marekani,World Bank,IMF na kadhalika unatoka wapi.Lazima tuweke mambo wazi.Hawa watu wanapokuja wana maslahi yao.Wanayotupa kama masharti 'actually' ndiyo faida yao.Kwam fano,wanapokuambia ubinafsishe ni kwamba, 'they are taking over your resources' na wewe unabaki kuwa mtumwa tu ''and that's what we are'.'Actually' sisi ni kama misukule,inayofanya kazi bila hata kujua kinachoendelea.Nitoe mfano hai wa sector ya mawasiliano,Vodacom.Vodacom inasema ina wateja milioni 4.Kama kila mmoja kati ya hao atatumia shillingi 1000 tu kwa siku, Vodacom inapata billioni4 kwa siku.Ni hela nyingi sana.Sasa tujiulize, kijana wetu anayefanya kazi Vodacom anapata mshahara shillingi ngapi? Mungu wangu akipata millioni1.5 ana bahati sana tena hiyo ni kwa mwezi.Sasa kama sisi sio misukule ya kufanyia watu kazi ni nini.Ngojeni ni waambie hali ndio hiyo kila mahali.Analeta kwa mkono huu anachukua kwa huu tena katika kiwango cha kutisha.Tena niseme nini, kile anacholeta ni kile alichokuibia.Jamani aibu hii ya kufanywa misukule tutaachana nayo lini?Mungu ibariki Afrika.
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  unless sikukuelewa,Japan after the second world war,iliweza kuscale heights za development,as a direct result of msaada then known as the MARSHALL AID PLAN
   
 3. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tikerra,

  I feel your frustration, sasa unapokuwa na hoja tena nzito namna hiyo weka basi na solution. umeleta hoja lakini sasa nini unafikiri kifanyike, how different should the whole thing be approached?

  GM
   
Loading...