Hivi wale Majangili 40 hivi wanaojulikana aliowasema Rais Mstaafu walishakamatwa? Na je, wale waliokuwa wanahojiwa na Tv ya Al-Jazira kule maeneo ya Mwenge nao wako keko?
Nadhani kupambana na ujangili wala hatuhitaji ndege, vifaru wala AK 25. Tunahitaji kuzuia tu wanunuzi wa nyara hizo, kudhibiti njia zote zinazotumika kusafirishia nyara hizo na kuhakikisha kuwa wanaokamatwa wanachukuliwa hatua kali.
Jingine ni kuhakikisha kunakuwepo na ulinzi shirikishi kwa kuwatumia wananchi wanaozunguka hifadhi zetu. Hili litawezekana kwa kuhakikisha kuwa na wao wanafaidika na rasili mali hizo!