SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020 katika sekta ya miundombinu ya huduma za reli fungu la 41, serikali ya CCM ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza ujenzi mkubwa wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway). Reli hii ya kisasa inatarajiwa kuwa na jumla ya urefu wa km 1219 ikianzia jijini Dar es salaam ikipita Mikoa ya Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora na kuelekea Mwanza na Kigoma kabla ya kuvuka mipaka ya nchi yetu ikisonga nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
Reli hii mpya ya kiwango cha Kimataifa inatarajiwa kupitisha Treni ya umeme na mafuta na itakuwa na uwezo wa kukimbia Kilometa 160 kwa saa moja ikiwa na abiria katika mabehewa mia moja ambapo ni sawa na muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma au dakika tisini kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro wakati Treni ya mizigo yenye mabehewa mia moja ambayo ni sawa na semitrela mia tano itakuwa na uwezo wa kukimbia Kilometa 120 kwa saa moja. Reli hii inawezo wa kupitisha kwa wakati mmoja treni yenye mzigo wa tani elfu thelathini.
Ikumbukwe kuwa katika historia ya nchi yetu, reli hii ya Standard Gauge Railway (SGR) ni ya kwanza kujengwa kwa kutumia fedha za watanzania kwa kiasi kikubwa, ambapo hapo awali nchi imekuwa na njia kuu mbili za reli yaani reli ya kati iliyojengwa na Wajerumani miaka ya 1899 -1929 na Reli ya TAZARA yaani Tanzania and Zambia Railway Authority iliyojengwa miaka ya 1970 kwa msaada wa watu wa China ambapo Reli hizi zote ni za kiwango cha kati yaani Medium Gauge Railway (MGR).
Reli ya kati na reli ya TAZARA kwa sasa zote zimekuwa zikisuasua katika utendaji kazi hasa kutokana na kujengwa kipindi kirefu na usimamizi kuwa duni. Reli hizi zina uwezo wa kubeba mizigo yenye tani elfu tano pekee kwa awamu moja ambayo ni mara sita zaidi ya reli mpya ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR), na pia Reli hizi zina uwezo wa kukimbia kilometa ishirini kwa saa ambapo ni sawa na mara nane zaidi ya SGR.
Reli hii ya kisasa yaani Standard Gauge Railway ni bora zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, kati na kusini mwa Jangwa la Sahara ikilinganishwa kwa ubora wake, mwendo kasi, gharama za ujenzi na urefu wa reli yenyewe.
Ikilinganishwa na Reli zingine za nchi mbalimbali barani Afrika Reli hii ndio Reli ya masafa marefu yenye mwendokasi zaidi kuwahi kujengwa katika karne ya 21 mfano,Kenya, Ethiopia na Afrika ya Kusini Standard Gauge Railway, treni yao ya abiria husafiri kwa kilomita 120 kwa saa moja ambapo ni chini zaidi ya Tanzania Standard Gauge Railway ambapo mwendokasi wa treni ni kilomita 160 kwa saa.
Kwa upande mwingine, reli hii ya Tanzania ndio Reli iliyogharimu kiasi kidogo zaidi cha fedha ikilingamishwa na ujenzi wa reli ya SGR unaofanana katika nchi mbalimbali ikiwemo Ethiopia, Kenya na Afrika ya kusini ambapo, Nchini Kenya kipande cha reli cha Kilomita 482 kimegharimu shilingi trilioni 7.4, Ethiopia kipande cha umbali wa kilomita 730 kimegharimu shilingi trilioni 9.2 ambapo Tanzania kipande kilomita 726 kutoka Dar es sallam hadi Dodoma kimegharimu shilingi trilioni 7.06 na hii inafanya ujenzi wa Reli ya kisasa ya Tanzania kuwa ndio reli bora zaidi na inayogharimu fedha nafuu ukilinganisha na nchi jirani.
Kipekee kabisa ukilinganisha na ujenzi wa reli za masafa marefu za nchi zingine barani Afrika Tanzania inajenga urefu wa kilomita 726 yaani kutoka Da es salaam, Morogoro mpaka Dodoma kwa kutumia fedha za ndani sawa na shilingi trilioni 7.062 kabla ya kuendelea kuelekea Mwanza na Kigoma kupitia Singida na Tabora ambapo inafanya kuwa na jumla ya kilomita 1219. Hii ni tofauti na Nchi za jirani ambapo reli ya kisasa ya Ethiopia na Kenya zenye urefu wa kilomita 730 na 482 zote zimejengwa kwa mkopo kutoka serikali ya China.
Ujenzi wa reli hii ya kisasa umegawanyika katika vipande vitano, ambapo uzinduzi wa ujenzi awamu ya kwanza nay a pili umekwisha fanyika. tarehe 12 Aprili 2017 uzinduzi awamu ya kwanza ulifanyika ambapo awamu hii inaanzia Dar es Salaam mpaka Morogoro kilomita 300 na inagharimu shilingi tirioni 2.8. Awamu ya pili ni kuanzia Morogoro mpaka Makutupora Dodoma kilomita 400 ambapo ujenzi unaendelea, awamu hii inagharimu shilingi tirioni 4.3 na uzinduzi huu umekwisha fanyika tarehe 14 machi 2018, ambapo uzinduzi awamu zote umefanywa na Mh John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Tanzania.
Reli hii ya kisasa inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji wa uchumi na kutatua changamoto ya ajira. Inakadiriwa kuwa ujenzi wa reli utatoa jumla ya ajira elfu 30 za ajira rasmi na ajira laki sita zisizo rasmi. Mbali na suala la ajira, reli hii itakuwa ni kichocheo cha uchumi ndani ya nchi na nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, DRC Kongo na Sudani Kusini ambapo mizigo mingi zaidi itasafirishwa kutoka bandari ya Da es salaam kuelekea katika nchi hizo kwa haraka na kwa bei nafuu
Tafiti zimethibitisha kuwa, usafiri wa reli ni bora, salama, haraka na nafuu zaidi katika usafirishaji wa mizigo mingi zaidi na abiria wengi zaidi. Ripoti ya benki ya maendeleo ya Afrika ya mwaka 2015 inaeleza kuwa “usafiri wa reli ni muhimili mkubwa kwa maendeleo ya uchumi na kama Afrika tusipoweza kuwekeza kwenye reli hatutaweza kutumia ipasavyo rasiliamali zetu katika namna ya kutuletea maendeleo”.
Lakini pia tafiti nyingine zinaonesha kuwa katika bara la Afrika gharama za usafiri ni kubwa kuliko maeneo mengine Duniani mathalani, wastani wa kusafirisha kontena moja la futi 20 ndani ya Afrika Mashariki kilomita 1500 ni dola za kimarekani elfu tano ($5,000), hii ni sawa na kusafirisha kontena hilo hilo kutoka China hadi Tanzania umbali wa kilomita 9000. Hali hii inapelekea kushusha kwa pato la Afrika kwa kati ya asilimia 1-2 na kupandisha gharama za bidhaa kutokana na gharama ya usafiri kwa asimilimia 40. Hivyo basi nchi yeyote ili ipige hatua kwa haraka ni lazima iwe na miundombinu hasa ya reli ya uhakika.
Pia reli hii ya kisasa itasaidia zaidi kukua kwa sekta nyingine ikiwemo za kilimo, uvuvi na ufugaji kutokana na wakulima na wafanyabiashara kuweza kusafirisha mazao na bidhaa kwa urahisi zaidi na kwa bei nafuu kutoka na kuelekea mikoa ya Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Pwani, Dar es salaam na mikoa mingine. Zaidi, reli hii itasaidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zinapotea kila mwaka kufanya marekebisho ya barabara zilizoharibiwa kutokana na kupitisha mizigo mizito. Reli hii inajengwa na kampuni ya Yapi Markerz ya Uturuki ambapo awamu ya kwanza imeanza kujengwa Aprili 2017 ikitarajiwa kukamilika baada ya miezi 30 yaani Novemba 2019, wakati awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma ikitarajiwa kukamilika mapema 2021.
Uamuzi huu mgumu na wa kihistoria katika karne ya 21 wa kujenga Reli hii ya kisasa (Standard Gauge Railway-SGR) kwa asilimia kubwa kutumia fedha za ndani, umefikiwa kwa jitihada kubwa za kubana matumizi na kuweka nidhamu ya matumizi ya fedha za umma uliofanywa na Ndg John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo ameweza kupandisha makusanyo ya fedha kutoka shilingi bilioni 800 mpaka kufikia tirioni 1.3 kwa mwezi.
#T2020JPM #TeamUshindi #TeamMafanikio
Sent using Jamii Forums mobile app