Kila aina ya uwekezaji ili uwe na tija ni lazima kwanza miundombinu muhimu ya kuuwezesha kufanya kazi iwepo, bila hivyo tutazidi kushuhudia mitaji mingi ikipotea, na tayari tumeshuhudia biashara nyingi na uwekezaji mwingi unafanyika lakini baada ya siku au miaka kadhaa yote inakufa, hii ni kutokana na kukosa kuandaa miundombinu itakayoendelea kuleta uhai kwenye uwekezaji, Ni lazima miundombinu ya msingi iandaliwe kama vile:
1. Kusuka mfumo imara wa kupata taarifa za muhimu na wakati wowote juu ya sekta unayohitaji kuwekeza.
2.Kuandaa/ kutengeneza watu sahihi watakao kusaidia katika kila hatua ya uwekezaji utayoifikia, kuna baadhi ya uwekezaji unahitaji kutumia watu wengi wenye ujuzi na uzoefu mbalimbali na watu hawa kila mmoja ana nafasi yake kulingana na hatua ya mradi ulipofikia
3. Kujijengea uwezo wa kiufahamu, maarifa na uelewa wa sekta husika, ni lazima utafute ujuzi wa kutosha juu ya sekta hiyo ikiwemo kufahamu, jinsi ya kuendesha na kuisimamia miradi hiyo, Changamoto zake, Muda wa mradi kuanza kuzalisha faida, soko, na hata kujua mustakabari wa sekta hiyoKwa leo tuishie hapa, ila kumbuka kama samaki anavyohitaji maji ili kuishi kadhalika na uwekezaji pia unavyohitaji kujengewa miundombinu imara ya kuiwezeha kuishi, katika hali halisi si jambo rahisi kuandaa miundombinu ya uwekezaji kwani inahitaji muda wa kutosha,utulivu,uvumilivu na akili za kutosha, na baadhi ya sekta zinahitaji kujitoa zaidi kuandaa miundombinu yake.
Kama waswahili wasemavyo maji hufuata mkondo kadhalika na Pesa nyingi na nzuri huifuata miradi iliyojengewa miundombinu imara.
Itaendelea sehemu ya pili.
Imeandikwa na: Allen Lupembe.
Kwa makala nyingine za uwekezaji tembelea tovuti ifuatayo: Uwekezaji Tanzania