Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 imetenga shilingi bilioni 50.5 kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta ya uchukuzi kwa maswala ya usafiri wa majini.
Amesema kwa kuanzia, miradi hiyo itaanza na ujenzi wa meli moja mpya katika ziwa Victoria sambamba na hilo tayari wamekwishatenga bilioni 21 kwaajili ya ukarabati huo.
Akizungumza na East Africa Radio Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano nchini Prof. Makame Mbarawa amesema serikali imejipanga katika kuboresha huduma za usafiri katika ziwa Victoria kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.
Sanjari na hilo, Prof mabara amesema kuwa mradi wa pili ni kufanya ukarabati wa meli mbili katika ziwa Victoria ambao ni MV Butiama kwa Bilioni 3.6 na Meli ya MV Victoria kwa Bilioni 20 na kufanya ukarabati wa meli zingine ambao utagharimu bilioni 5.6 na hiyo ni kwa mujibu wa miradi inayokwenda kutekelezwa kwa mwaka huo wa fedha 2016/2017.
Amesema wamepanga kuweka mpango mkakati mpya wa kupata wataalam wa kuendesha mashirika ya meli nchini kwakuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya wataalam hasa kwa maswala ya utawala na mafundi, kwahiyo iko haja ya kutengeneza timu ya wataalam ambao itasaidia kuwahudumia watanzania ambao wanatumia usafiri wa ziwa Victoria.
Ameongeza kuwa kutawekwa utararatibu maalum wa matumizi ya vyombo hivyo kwa kufuata taratibu za SUMATRA kama vimekidhi wiwango vya kufanya kazi kwa taratibu za usafirir wa majini.