WanaJF,
Kwanza ieleweke wazi kuwa, hii bomoa bomoa inayoendelea ni jitihada za rais Dkt Magufuli kusafisha maovu ambayo yamekuwa yakifanywa na viongozi watangulizi hususani mawaziri waliowahi kupatiwa dhamana kwenye wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.
Kihistoria wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi pamoja na kubadilishwa badilishwa majina kadri uhitaji wa kufanya hivyo ulivyokuwa ukionekana, lakini ndio wizara inayosimamia mambo yote yanayohusu sekta ya ardhi nchini ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999, sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 ya mwaka 1999 na sera ya ardhi ya mwaka 1995.
Pamoja na mawaziri wengi kuwahi kuhudumu katika wizara hii, ni ukweli usiopingika kuwa ni Lowassa ndiye aliyehudumu kwa miaka mingi kuliko mawaziri wengine wote kwenye wizara ya ardhi. Lowassa amekaa kwenye hii wizara kwa miaka 9! Na katika kipindi chake akiwa waziri wa ardhi ndio kulikuwa na ongezeko kubwa la watu kwenye miji na majiji huku ongezeko kubwa zaidi la watu lilionekana katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha, kama waziri mwenye dhamana ya sekta ya ardhi wakati huo, Lowassa kisheria alikuwa na mamlaka ya kuhakikisha viwanja vinapimwa kwa wingi ili kuendana na uhitaji wa watu na pia ndio ilikuwa wakati muhafaka kwa wakati ule kuhakikisha maeneo tengefu, ikiwemo maeneo hatarishi na maeneo ya wazi hayaingiliwi na wananchi ambao walikuwa wakihamia mjini kwa kasi wakati huo.
Lakini kutokana na uzembe, kujisahau, ubinafsi na kutojua majukumu na mamlaka yake, Lowassa alikuwa amejikita zaidi kwenye kujimilikisha mashamba na maeneo ya malisho huko Arusha, Tanga na Morogoro, huku jiji la Dar es Salaam likipokea maelfu ya watu kila siku kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na wananchi hao walijikuta wakivamia maeneo ya mabondeni na yale ya wazi ili kuweza kupata hifadhi kwa maana ya kujenga nyumba zao kwenye maeneo hayo hatarishi. Hii ilitokana na kutokuwepo kwa usimamizi wa sheria wakati huo.
Hivyo tunapokuwa tunazungumzia hili tatizo la ujenzi holela hasa mijini tusisahau kuwataja wale viongozi ambao walikuwa na wajibu wa kuhakikisha sheria, taratibu na kanuni zinafuatwa ili kuepusha wananchi kujenga kwenye maeneo ambayo yamekatazwa na sheria au maeneo hatarishi. Lakini kwa masikitiko makubwa nasema kuwa Lowassa akutekeleza wajibu wake wakati huo na matokeo yake ndio haya ya wananchi kubomolewa nyumba zao bila fidia yoyote ile kutoka serikalini.
Note: Kisheria fidia utolewa kwa mtu ambae anamiliki eneo kihalali kwa mujibu wa sheria kwa maana nyingine mtu mwenye hati ya umiliki wa kiwanja husika. Na ikumbukwe pia, hati utolewa kwa maeneo yaliyopimwa tu, ambayo kwa Tanzania nzima ni 30% ya ardhi yote ndio imepimwa hadi sasa. Kwa bahati mbaya sana wananchi hawa walioathirika na zoezi la bomoa bomoa hakuna hata mmoja mwenye hati. Hivyo kisheria hawana vigezo vya kupatiwa fidia. Kwa kuwa sheria hiyo hiyo inawatambua wananchi hao kama wavunja sheria kwa kitendo chao cha kuvamia na kujenga katika maeneo ya wazi na maeneo hatarishi (mabondeni).

Last edited by a moderator: