ALWATAN KIZIGO
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 539
- 642
Jana siku ya Tarehe 5/5/2018 wakati Mh. Rais Magufuli akiendela na Ziara yake Mkoani Morogoro alisimamishwa na wananchi katika Kijiji cha Mang'ula, na hapo ndipo akajitokeza kijana mdogo wa kidato cha kwanza aitwaye Mlindoka Msangi akaelezea changamoto ya vyoo inayoikabili shule yao ya Mang'ula Secondary.
Mh. Rais akatoa Shillingi million 3 na kukamkabidhi kijana huyo azipeleke shuleni chini ya ulinzi wa Polisi. Pamoja na kutatua changamoto hiyo lakini bado Mh Rais alijiuliza maswali mengi sana na ndio maana hata alipokua anahutubia katika uzinduzi wa Daraja la Magufuli ilimbidi aelezee tukio hilo na akasisitiza kwa kusema kwamba "hivi hata ujenzi wa vyoo nao mpaka umsubiri Rais"
Hii ni kauli nzito sana yenye ujumbe mzito kwa wasaidizi wake Serikalini kwa maana ya wakuu wa Mikoa ,wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi na wasaidizi wake kwenye Chama kuanzia Wenyeviti wa Mikoa na Wilaya na Kamati za Siasa za Mikoa na Wilaya.
Kiukweli kuna baadhi ya kero ndogondogo ambazo hazihitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kuziondoa bali zinahitaji utashi na uwajibikaji tu, lakini zimeendelea kuwa changamoto sugu kwa wananchi.
Sasa hapo ndipo unajiuliza maswali iwapo baadhi ya wasaidizi wa Rais katika ngazi tajwa hapo juu wanatimiza majukumu yao kisawa sawa? Ujenzi wa kitu kama choo haukupaswa kusubri ziara ya Mh.Rais ili kumalizwa ni aibu.
Tatizo hili linasababishwa na baadhi ya wasaidizi Mikoani na Wilayani kutofanya ziara za mara kwa mara ili kubaini kero mbalimbali na kuzitafutia namna ya kuzimaliza badala yake wanapendelea kukaa maofisini kupuliziwa na ubaridi wa viyoyozi.
Rais hawezi kufika katika kila Kata au kijiji Tanzania nzima na ndio maana akawateua wasaidizi wake ili wakamsaidie kuwahudumia wananchi huko kwenye ngazi za chini.
Sasa inapofikia mahali wananchi wanaendelea kusumbuliwa na vikero vidogovidogo ambavyo vinaweza kumalizwa na ngazi ya Mkoa au Wilaya basi tunapata jibu kuwa kuna baadhi ya watumishi hawamtendei haki Rais aliyewateua.
Rais anahangaika huku na kule kuinyoosha nchi anasema kila siku kwamba watumishi aliowateua waache uvivu na uzembe lakini bado baadhi yao maskini ya MUNGU bado wamelala usingizi wa pono.
Mathalani kuna baadhi ya Wilaya utakuta wananchi wamejitolea kwa nguvu zao kujenga kituo cha afya mpaka ngazi ya rinta na nguvu zimewaishia hivyo basi wanapoenda kuomba msaada wa umaliziaji katika Halmshauri unakuta wanapigwa danadana.Hii inasikitisha sana.
Pia kwa wanasiasa hususani Wabunge nao wana fedha za maendeleo ya Jimbo. Fedha hizi wanapewa na Serikali ili kusaidia kusukuma maendeleo katika majimbo yao.
Lakini kwa bahati mbaya sio wabunge wote wanaofanya hivyo na ndio maana hadi leo ukitembelea majimboni utakutana na kero ndogo ndogo ambazo kama kungekuwa na Sera ya uwazi ya matumizi ya fedha za maendeleo ya jimbo basi kero hizo zingeweza kutatuliwa maramoja.
Rais ana majukumu mengi wasaidizi wake Serikalini ifike mahali wamuonee huruma jinsi alivyojitoa ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya watu wake, "li nchi hili ni likubwa" tukisema kila kitu tumuachie Rais tutakua tunamuonea kiukweli ,ni vyema wakaendana na kasi yake kwa kuwajibika kwa nguvu na kuwa wabunifu katika maeneo yao.
Muda wa kuwa na watumishi mangimeza umeshaisha huu ni wakati wa kuchapa kazi. Haingii akilini Serikali inampa mtu gari , inamlipa mshahara na stahiki zake nyingine lakini bado mtu huyo anakua mzito katika kutimiza majukumu yake.
Na viongozi wa chama nao kupitia Kamati za siasa wamsaidie Mwenyekiti wetu katika kuisimamia Serikali kwenye ngazi husika hususani katika kuziwasilisha kero za kipaumbele Serikalini ili zipatiwe ufumbuzi wa haraka.
Uzembe wa namna hiyo ndio unaochangia kupunguza kura za CCM katika uchaguzi hivyo watu wa namna hiyo inabidi wabadilike, ili CCM iendelee kupeta kwa sababu mwisho wa siku wananchi wanakiadhibu chama na sio wao na katika hili sidhani kama Mwenyekiti atakua radhi kuona chama chake kinaadhibiwa kutokana na uzembe na uvivu wa baadhi ya wasaidizi nafikiri ataanza kuwaadhibu wao kwanza kabla chama hakijaadhibiwa.
Wao ndio wanaokaa na wananchi na ni wao ambao wanazijua kero mbalimbali za wananchi hivyo kwa kutumia mamlaka waliyonayo ya Kuisimamia Serikali wanaweza kusaidia katika kutatua changamoto hizo haswa ikizingatiwa kwamba CCM sasa hivi inashika hatamu katika kuisimamia Serikali.
Wasalaam,
Augustino Chiwinga.
0659438889.