SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,947
- 2,032
Nimeanza kufikiria watoto wadogo wanaolivuta vumbi hili,wafanyabiashara ambao ofisi zao ziko kando ya barabara hii inayojengwa.
Wakuu nyumba za maeneo haya ukiangalia mapaa yake zimefunikwa na vumbi la kifusi kilichosambazwa barabarani.
Ina maana barabara hii haikutengewa bajeti ya kuimwagilia maji kupunguza vumbi.Mradi ni mzuri lakini kumbukeni wananchi wa maeneo haya ni masikini wasioweza kumudu kunywa maziwa kila siku.
Wahusika ninawaagiza ikiwezekana jioni ya leo muanze kumwagilia barabara hizi kwani vumbi hil linaingia hadi kwenye nyumba.
Kuna wakati nilikuwa Mbozi huko Mbeya kulikuwa na mradi ukiendelea wa barabara ya vumbi nilishuhudia ikimwagiwa maji asubuhi na jioni.Iweje miradi ya mjini iwe shida?
Watu wa afya msiishie tu kukagua mazingira machafu kagueni na vitu kama hivi,serikali ya mtaa wa Kigogo/Mkwajuni tuliitoa CCM ili msimamie vile vilivyowashinda tumieni uwezo wenu.
VUMBI HILI NI BAYA SANA.