mtaalamu123
Senior Member
- Oct 15, 2015
- 185
- 203
Licha ya wabunge kushinikiza ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge), Serikali imeendelea kusisitiza kuwa haiwezi kujenga reli hiyo kwa kutumia bajeti yake, huku ikishikwa kigugumizi kueleza mpango ilionao kuhusu ujenzi huo. Akijibu hoja za wabunge kwenye mjadala wa mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya serikali mwaka 2016/2017, waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema kama serikali itatumia fedha za mfuko wa reli, ambazo ni Sh 50 bilioni kila mwaka, itatumia miaka 320 kujenga reli hiyo.
Hivi karibuni wabunge wanaotokea kwenye mikoa ambayo reli ya kati inapita, waliungana kushinikiza ujenzi wa reli hiyo wakisema bila ya Serikali kusikiliza kilio chao, watahamasishana ili waisusie bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017.
Katika maelezo yake, Dk Mpango alisema gharama za kujenga reli hiyo ni kati ya dola bilioni saba mpaka tisa na nusu (Sh 15 trilioni).
Alisema hata nchi ikitumia mapato yake yote ya kodi ambayo ni takriban Sh 12 trilioni, kwa mwaka mmoja na miezi mitatu, reli hiyo itajengwa kwa miaka minne. Alisema mbali na uwezo wa Serikali kuijenga kwa mapato yake ya ndani, utafiti uliofanyika unaonesha kuwa ili mradi huo uwe na manufaa kiuchumi, lazima matawi yake ya kwenda nchi za Burundi, Rwanda na DRC yajengwe. Alisema kama nchi itaamua kujenga reli hiyo kulingana na mawazo ya wabunge, nchi itakosa fursa kubwa kwa kuwa mzigo wa kwenye reli ya kati hautaweza kurudisha gharama ya ujenzi.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema Serikali imejipanga kujenga reli hiyo yenye urefu wa kilomita 2,560. "Tutajenga reli ya Dar es salaam-Tabora hadi Isaka. Uvinza hadi Msagati, Isaka hadi Mwanza, Isaka hadi Kaze, Kaze hadi Kisumo. Baadhi ya njia za reli zimeshafanyiwa upembuzi yakinifu, ikiwamo reli ya Tabora kwenda Kigoma." Alisema.
Akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge, Dk Mpango ambaye alikua kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alisema bila kushirikiana na sekta binafsi, ni ndoto kujenga reli hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Reli (UWR), Ezekiel Maige, Msalala (CCM) alisema wataendelea kuishinikiza Serikali kuijenga reli hiyo bila kuchoka na kwamba walichelewa kuunda umoja huo.