Anonymous
Senior Member
- Feb 3, 2006
- 125
- 321
Habari zenu wakuu,
Tukubaliane tu kwamba utalii unatutangaza, unatuingizia fedha za kigeni, kuinua uchumi na kutoa ajira. Lakini utalii usiposimamiwa vizuri madhara yake ni mtambuka na ni makubwa sana!
Ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuna mwamba mmoja anaendelea na ujenzi wa hoteli ya watalii (Hii hapa Serengeti Lake Magadi Lodge | Wellworth Collection Hospitality ). Juu kabisa ya mlima. Usiku akiwasha taa zake anamulika mbuga nzima. Yaani ni kama lightouse, taa imewekwa kilingeni kabisa kuongoza watu usiku.
Ujenzi huo ni kinyume kabisa cha sheria za hifadhi na sheria ya mazingira. Zoning pia inaonesha kuwa eneo lenyewe ni tengefu kwa ajili mazalia ya wanyamapori hasa Faru, Simba, Chui n.k. Kwenye hili watalii wanakerwa sana!
Halafu bado kuna zile changamoto za Kambi za kuhama hama kurundikwa sehemu moja hasa kule Kogatende na Ndutu! Na hivi utalii unavorudi kwa kasi, tusipokuwa makini tutajiharibia wenyewe.
Ajabu ni kwamba wanakazana kuandika "Serengeti shall Naver Die" Lakini kwa matamaa ya fedha wanazidi kuiua!
Tupaze sauti zetu haya masuala ya ujenzi holela yakome. Ifike mahali wenye mamlaka wangetanguliza misingi ya taaluma zao na uzalendo wasitishe vituko kama hivi hifadhini.
Hoteli inajengwa kileleni mwa mlima. Yaani, juu ya mlima ni hoteli yenyewe (lounge/main areas)... Rooms za wageni zimesambaa juu ya mwinuko kuelekea upande wa ziwani (Lake Magadi).
Hiyo sehemu na majengo yanayoonekana chini ni yalipo makazi ya staff.
Kwa ujumla maeneo husika ni mazalia ya wanyamapori hasa chui. Na ni maeneo maarufu sana kwa migration ya wanyama upande wa central Serengeti kabla hawajaelekea Moru na Southern Corridors.
SHERIA ZIPI ZINAHUSIKA?
1. Sheria ya Mazingira (EMA #20 ya mwaka 2004, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2018) - anzia kuasoma Sehemu VI ibara ya 81-85, 89-90, 92-97, 161, 184, 193, 198 n.k
2. NEMC EIA na Audit Regulations 2005 na 2018.
3. Tourism Investment Manual pia
NB:
1. Wachunguzi wa mambo wanahisi janja janja nyingi ndani ya SENAPA yametokea baada ya GMP kuisha muda wake.
2. Kuna usiri mkubwa unaotia mashaka kwenye mchakato wa EIA, ukizingatia unyeti wa eneo la Lake Magadi.
3. Kwa unyeti wa eneo husika la mradi haiwezekani na ni very unprofessional kwa EIA kuanza na kukamilika ndani ya mwaka mmoja (kwa mujibu wa maelezo yanayoibua mashaka ya msemaji wa TANAPA HQ). Wataalamu wanajua kuwa EIA huchukua muda mrefu kiasi (field - rejea NEMC audit regulations 2005).
4. Ili kulinda maslahi ya wawekezaji wengine ndani ya hifadhi - TANAPA'S TOURISM INVESTMENT MANUAL inaelekeza minimum distance ya 10kilometers kutoka accommodation facility moja hadi nyingine. Well-worth Collection's Lake Magadi Lodge pamoja na kupachikwa juu ya kilima na taa zake kusumbua wageni kwenye lodges za jirani ujenzi wake haukuzingatia umbali elekezeki!
REJEA:
TANZANIA ENVIRONMENTAL MANAGEMENT ACT, 2004
TANZANIA ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT AND AUDIT REGULATIONS, 2005
TANZANIA NATIONAL PARKS ACT
Serengeti National Park Rules | Tanzania
General Management Plan (2006-2016), Serengeti National Park, Tanzania
Ieleweke kuwa, Watalii mbalimbali, Wawekezaji, Wafanyakazi (hata wa TANAPA wenyewe) na waongoza utalii (tour guides) wenye uzoefu wa muda mrefu kuhusu utalii na uhifadhi hawaridhishwi na uwekezaji wa Wellworth Collection ndani ya SENAPA!