Ujasiriamali 1.1

May 24, 2012
84
33
niwashukuru wadau walioniunga mkono katika kuipitia thread yangu ya somo la mjasiriamali mdogo na wa kati na kuniomba niendelee kutoa somo hili ambalo wengi hulitafuta kwa gharama kubwa lakini huwa hawalipati ipasavyo.leo nataka nianze na ile amri ya kwanza ya ujasiriamali ambayo

  1. ubunifu (mpango biashara)

ndugu yangu unayetaka kuwa au umeshakuwa mjasiriamali tafuta kuanza na kitu ambacho unafikiri kuwa kitakuwa ni cha tofauti na wale waliotangulia na kabla hujaingia kwenye biashara hiyo andaa mpango wako kwanza. ubunifu ninaouzungumzia hapa unaweza kuwa katika mambo yafuatayo;

  • tafuta bidhaa mpya ambayo wengine hawajaivumbua lakini inahitajika katika eneo husika. mfano umeme ni tatizo vijijini, tafuta solapawa au jenereta nenda kaanze biashara ya kuchajisha simu vijijini.simu 1 ni sh 500 kuchaji, ukipata simu 20 kwa siku utakuwa na elfu 10 kwa siku, je mara siku 30 una bei gani?
  • kuwa mbunifu katika bei za bidhaa zako mfano bidhaa ambayo utaiuza huku uswahilini sh. 500, masaki usiende kuuza kwa bei hiyo, pandisha bei kulingana na matakwa ya maisha yao kwani ukiuza kwa bei hiyo bidhaa hiyo wataidharau
  • kuwa mbunifu katika kugundua mahitaji ya soko lako
  • kuwa mbunifu katika muda wa wa shughuli zako.MFANO biashara ya kahawa unaweza kuifanya pia katk viwanda ambavyo huwa na shifti ya usiku kwani huitraji sana bidhaa hiyo kuondoa usingizi.
  • kuwa mbunifu katika kuvuta wateja. mfano peleka au weka wazi bidhaa yako na mfafanulie mteja wako matumizi sahii ya bidhaa hiyo.
  • kuwa mbunifu katika kupata bidhaa na kuzileta sokoni. mfano tumia usafiri usio na gharama kubwa kwani ni muhimu kufanya hivyo ili kusevu faida


NASHUKURU WADAU KWA KUNIPOKEA.


 
Back
Top Bottom