MKUU wa Mkoa wa Pwani, Hajjat Amina Said, sasa ameamua kutoa makucha yake dhidi ya watendaji wazembe ambao amedai kuwa ndio wanaokwamisha maendeleo ya mkoa huo na si kukosekana kwa fedha kama inavyodaiwa na baadhi ya watendaji.
Mkuu huyo alifanya hivyo juzi akiwa wilayani Kisarawe, ambako aliaamuru watendaji sita wa halmashauri ya wilaya hiyo, wakatwe asilimia 15 ya mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili, ikiwa ni adhabu kwa kosa la kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Watendaji hao ambao wataanza kukatwa mishahara yao kuanzia mwezi ujao ni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Alquin Ndungwi.
Wengine ni Ofisa Elimu ya Msingi wa Wilaya ya Kisarawe, Winifrida Mbuya, Ofisa Elimu ya Sekondari Donard Chavila, Ofisa Afya Dk E. Helela, Mhandisi wa Wilaya Ayoub Myaule, Ofisa Mipango, Deus Mbalamwezi, na Mweka Hazina, Isaya Moses.
.
Mkuu huyo wa mkoa alitaja baadhi ya miradi iliyokwama kutokana na uzembe wa watendaji hao kuwa ni ile ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za kata, zahanati na ukosefu wa madawati, jambo linalosababisha wanafunzi kuketi sakafuni.
Hijat Amina alitoa agizo la kukatwa sehemu ya mishahara watendaji hao katika kikao chake cha majumuisho ya ziara ya siku moja aliyoifanya wilayani humo, ziara iliyokuwa na lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kimsingi, wilayani hiyo imeshindwa kutekeleza ipasavyo ilani hiyo.
Alisema serikali ilikwishapeleka fedha za miradi katia vipindi tofauti vya kuanzia Julai mwaka jana na kwamba alichogundua ni kwamba watendaji hao kila mmoja kwa nafasi yake, alikaa nazo hadi Februari na Machi mwaka huu, walipoamua kuzipeleka kwa wananchi.
Mkuu huyo alisema kitendo kukalisha fedha hizo kwa muda wa miezi sita bila kufika kwenye miradi, kinaashiria kuwa zilikuwa zinahifadhiwa katika akaunti za watu binafsi kwa lengo la kupata faida.
"Hapa msinieleze kitu,katika taarifa mlioniletea, mmeonyesha miradi imekamilika sasa leo nimeamua kupita na kujionea hali halisi kuwa nyie ni waongo, na mmeidanganya serikali katika hili simfumbii macho mtu wala sitajali cheo chake,"alisema Mkuu wa wilaya.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo alitembelea shule tano za sekondari za kata za Gongoni, Makulunge, Msimbu, Mfuru na Kibuta.
Hijat Amina alielezwa kuwa kwa pamoja shule hizo zina madawati 120 tu kati ya madawati 640 yanayohitajika.
Kukata mtu mshahara sio kinyume cha sheria?
Baadhi ya watz watu wa ajabu sana siku hizi,mtu anavunja sheria the great thinkers tunakuja hapa kusifia!
Kwani huyu mama ndiye Waziri mkuu wetu?Huyu mama hivi sasa ndiye waziri wa UTUMISHI?huyu mama ndiye waziri wa TAMISEMI?
kama hana nafasi hizo 3 nilizotaja juu,basi kwa madaraka gani ndani ysa katiba ya jamhuri ya tz inayompa nguvu kufanya haya aliyoyafanya kwa maafisa wenzake wa serikali kuu?
Namshauri kama lengo lake ni kujitutuma aonwe na wananchi wa kiteto ili wampe ubunge afanye hivyo bila kuvunja katiba,na kama anataka sana kukata watumishi mishahara yao basi afanye hivyo kwa house girl/boy wake(kama anao),maana hao ndiyo wapo chini yake kiuajiri !
Namshauri kama lengo lake ni kujitutuma aonwe na wananchi wa kiteto ili wampe ubunge afanye hivyo bila kuvunja katiba,na kama anataka sana kukata watumishi mishahara yao basi afanye hivyo kwa house girl/boy wake(kama anao),maana hao ndiyo wapo chini yake kiuajiri!
nadhani tutakuwa tumetimiza wajibu wetu pia kama tutaweza kumshauri endapo tu hii motive yake ina nia njema na nchi hii .... tusiishie tu kukatisha watu tamaa, kulalamika na kulialia hovyo ... we need solutions jamani!
malafyale ... you can do better than this ... !![/QUOTE
Please accept my apologetic attitudes(if any)kwa habari hii hasa kama imekukukwaza mwana jf mwenzangu Madabwada!
Huyu Coastal Region RC alinikera sana na ha-make sense at all,kama ndiyo ingekuwa ukiwa mtendaji mbaya unakatwa mshahara basi angekatwa toka Jk na baraza lake lote na wengine wengi aliowateua akiwemo yeye maana hakuna walilowatendea kuwapa maisha bora watz;achilia wabunge wetu wengi ambo ni gvt rubber stamp!
kwanza suluhisho la kuwaondoa wafanyakazi inefficient sio kuwakata mishahara bali ni kuwafukuza kazi jambo ambalo litafanywa na mwajiri wao na huyu mama sio mwajiri wa watumishi hawa!
kukatwa mtu mshahara ni kinyume na utawala bora na hapo labda ndipo nikakasirika hadi nikateleza kuandika ndugu madabwada-nisamehe sana!
Interesting..
Najiuliza watakataje mishahara wakati inapitia Benki kutoka Hazina...Nasikia dalili ya sarakasi na muwasho wa upupu hapa.
kimsingi kama ndivyo alivyo; hafai kuwa Mbunge wa kawaida. Anatakiwa kuwa mbuneg wa kuteuliwa halafu anapewa uwaziri wa kusimamia matokeo.. we need results oriented leadership..
malafyale ... you can do better than this ... !![/QUOTE
Please accept my apologetic attitudes(if any)kwa habari hii hasa kama imekukukwaza mwana jf mwenzangu Madabwada!
Huyu Coastal Region RC alinikera sana na ha-make sense at all,kama ndiyo ingekuwa ukiwa mtendaji mbaya unakatwa mshahara basi angekatwa toka Jk na baraza lake lote na wengine wengi aliowateua akiwemo yeye maana hakuna walilowatendea kuwapa maisha bora watz;achilia wabunge wetu wengi ambo ni gvt rubber stamp!
kwanza suluhisho la kuwaondoa wafanyakazi inefficient sio kuwakata mishahara bali ni kuwafukuza kazi jambo ambalo litafanywa na mwajiri wao na huyu mama sio mwajiri wa watumishi hawa!
kukatwa mtu mshahara ni kinyume na utawala bora na hapo labda ndipo nikakasirika hadi nikateleza kuandika ndugu madabwada-nisamehe sana!
malafyale tuko pamoja mkuu ... tuendelee kutaka issues kwa manufaa ya taifa letu ... naheshimu sana michango yako humu ndani ndio maana nikashtushwa na tamshi lako ... lakini sio issue .. naomba tuendelee na mjadala
Interesting..
Najiuliza watakataje mishahara wakati inapitia Benki kutoka Hazina...Nasikia dalili ya sarakasi na muwasho wa upupu hapa.
mkuu inawezekana pia alitamka hivyo akiwa anaamini kuwa wana-share the same opinion na ngazi husika za maamuzi za hao maafisa na hivyo atalifikisha hilo suala huko e.g waziri husika and the like.

anajiamini...ni shangazi yake mkulu