Ujanja ujanja wa Msechu umefika mwisho

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
3,097
1,352
Nilichokisikia kwa mkurugenzi wa shirika la Watumishi Housing Company. Ndg fredy msamwa; maelezo yake kama kweli wanajenga nyumba za sh. 30, 40 na 50. nadhani ukiritimba wa huyu jamaa ndg.Nehemia na shirika letu l NHC utafikia mwisho.

Nimependa sana ubunifu wa mifuko ya hifadhi ya jamiii kwa kubuni kitu hiki kitawasaidia sana watumishi wa umma kwa kupata nyumba za bei nafuu. Hasa watumishi wenye mishahara midogo km polisi, walimu na kada nyingine za level ya chini.

Miradi yao ni muda mrefu kati ya miaka 25 mpaka 30. Ushindani na NHC italeta ufanisi na kuondoa ukiritimba wa NHC.
 
Ngoja tuone, maana hata katika mitandao yao simu USHINDANI wao haujatusaidia kitu!
 
Kama kuna Mbadala watu wengi watawakimbia,Yaani bei zao hazina uhalisia wa gharama za ujenzi wa nyumba katika kipindi cha sasa,bei yao inazidishwa mara 4 zaidi ya bei ya nyumba kwa sasa
 
Nilichokisikia kwa mkurugenzi wa shirika la Watumishi Housing Company. Ndg fredy msamwa; maelezo yake kama kweli wanajenga nyumba za sh. 30, 40 na 50. nadhani ukiritimba wa huyu jamaa ndg.Nehemia na shirika letu l NHC utafikia mwisho.

Nimependa sana ubunifu wa mifuko ya hifadhi ya jamiii kwa kubuni kitu hiki kitawasaidia sana watumishi wa umma kwa kupata nyumba za bei nafuu. Hasa watumishi wenye mishahara midogo km polisi, walimu na kada nyingine za level ya chini.

Miradi yao ni muda mrefu kati ya miaka 25 mpaka 30. Ushindani na NHC italeta ufanisi na kuondoa ukiritimba wa NHC.
TAARIFA: NHC ni mbia katika watumish housing company, wako partner wawili NHC na LAPF kama sikosei, so huyo msechu unayemsema hapo ndo kaanzisha hiyo initiative
 
NHC ni wapigaji tu, wamepiga pesa sasa wanataka kuzirudisha kwa kuuza nyumba kwa bei ambayo haipo.
 
TAARIFA: NHC ni mbia katika watumish housing company, wako partner wawili NHC na LAPF kama sikosei, so huyo msechu unayemsema hapo ndo kaanzisha hiyo initiative
Kuna mifuko ya hifadhi ya jamii yote, na kweli NHC sijui kwanini wanaingilia na huku kweli hapa ushindani utakuwa shida.
 
Mkuu hizo bei ni bila VAT na pengine alikuwa anavutia wateja. Mimi niliwapigia simu wakaniambia bei zao ni 57M kwa nyumba ya chumba kimoja, 89M kwa nyumba ya vyumba viwili na 120M kwa ya vyumba vitatu.

Hii ni kwa mradi wao wa Magomeni na Mwongozo Kigamboni.
 
Back
Top Bottom