Uingizaji sukari vs uingizaji mayai, tuache unafiki

mleta mada kawaita watetezi wa wazalishaji sukari wa ndani kuwa ni wanafiki!! sijaongelea suala la mayai, nlitaka awe sawa kuhusu kilio cha wazalishaji wa sukari. kama kwa mayai kuna kilio kama hicho, basi kisikike na serikali ifanye kazi yake. sio kuandika-andika kwa hasira kana kwamba wazalishaji wa sukari na watetezi wao wanafanya kosa.
 

thank you.
 

mkuu idoyo Kumbe hukunielewa, kilio changu ni sawasawa na walima miwa na wazalishaji wa sukari, na Sauti hii ipazwe pande zote. Tatizo wewe unaona kilio chetu wafugaji si Lolote.
 
kwani mayai ya tanzania sh ngapi na kutoka nje sh ngapi.
kwa wastani,
 
Kwa nilivyomuelewa mleta mada kilio chake kikubwa kipo hapa: " Iweje polutry na sugar industries zote zinaathiriwa na importation lakini no one is paying attention kwenye industry yao?" Probably hajaipresent persuasively enough, lakini mimi naona udhaifu wa Mamlaka husika katika suala zima la kuprotect local industries na hata initiatives za local people. Nchi za wenzetu wapo serious sana kulinda innovations na growth za local industries.
 
kwani mayai ya tanzania sh ngapi na kutoka nje sh ngapi.
kwa wastani,
Kipindi Wakati soko ni la wastani tray Moja tulikua tunauza 5500 mpaka 5700, Wakati mfuko wa Chakula cha kuku ni 39000. Now mayai kutoka Kenya 4000, bei ya Chakula iko pale pale , mishahara ya vijana pale pale , petrol ya generator ya kisima, vitamins, madawa....,
 
Ni Sawa Kabisa hicho ndio kilio changu/chetu.
 
I deal but it should not be at the expense of social cost, these international business or importer look at the price gap in the market.

Wafanyabiashara watanzania inabidi wajifunze where the importer gain in their margins, usikute watu wanatumia volume tu kutengeneza faida za biashara, sera za nchi zinakodi ndogo kwenye bidhaa, government subsidies etc.

This is the reason ppl do marketing research lakini habari za bei ya kilo za mchele kuwa tofauti kati ya sokoni iringa na dar kisa watu hawana maarifa halafu waendelee kilindwa na hadithi za uzalendo zinadumaza akili za wafanya biashara hata IMF wanasema these businesses are simple for the most part you can see why.

Watu inabidi waongoze maarifa au waje tu wakenya kama atuwezi kuwekeza kwenye kuinua maarifa ya ujasiriamali Rwanda, Uganda na burundi wapewe coastal area wawekeze, wanaotaka kulima wapewe mashamba walime, wanaotaka kufuga kisasa wafuge; time is moving society bado imelala tumezidi people can not even come up right pricing strategies zaidi ya kuangalia fulani anauzaje wakizidiwa serikari iwatete hapana enough, swala hapa ni jinsi gani hizo biashara zinalipa kodi Tanzania walau kuwe na fairness.
 
japo kuwa tupo ktk soko huria.
wafugaji ni muhimu kujadili hili na kuwa msimamo wa pamoja. maana mayai ni bidhaa ghafi.
 

tatizo lets ni Kwamba tukiuza kwa price ya 4000 unapata hasara daily
 
Mkuu tumejaribu kukutana Mara kadhaa pale UDSM, however the turnout was more than dis pointing . Yet we can't negotiate prices za vyakula Vya kuku ilihali eggs price inakwenda chin daily

Una point nzuri lakini ulitakiwa uiwasilishe BILA KUHUSISHA waagiza sukari. Mimi naona kama umetaka kufanya ulinganifu ni kipi cha kupewa kipaumbele zaidi na kipi hata kisipopewa kinaweza kisiwe na athari kubwa. Hapa umekosea. Point yako ingejikita zaidi kwenye: Wafugaji wa Kenya wana nini cha zaidi mpaka mayai yao yanakuwa rahisi kuliko yetu? Nimesema hivyo kwasababu hata ukitaka serikali ipige marufuku kuingiza mayai ya Kenya, uzoefu unaonyesha ile kanuni maarufu ya demand and supply itaendelea kufanya kazi.... hata kwa mlango wa nyuma! Hivyo muhimu ni kutopingana na hii kanuni bali kufanya hali itakayowezesha mayai ya Tanzania yashuke bei.
 
Asante mkuu, nakubali kosa na nashukuru kwa kuliweka vizuri. Naipenda nchi yangu
 
poultry industry imekuwa maarufu recently, hapo kabla haikuwa vibrant kama sasa. ishu ya sugar ni ya kitambo na ilikubaliwa kuwa SI. sasa asilalamike eti 'no one is paying attention' kwa sababu hata yeye tayari ameshatoa kilio, serikali ikisikia kazi itafanyika kuona kama ina-qualify kuwa SI. kumbuka kuwa tanzania haitakurupuka kuyazuia mayai, lazima pawe na makubaliano na SADC, EAC.
 

i have tried to go thru your posts, I have no idea what exactly are you defending? Wewe ni mtanzania?
 

Unq hoja nzuri... Ila presentation imeuwa hoja yako.
Hatuwezi Sacha ililia su ari kwa vile tu wewe unadhani wauza/wazalisha maya wapo wengi.

Sukari ina impact kubwa kwenye uchumi wa nchi ukilinganisha na mayai
 
gharama zako za product cost ziko wapi mpaka chini ya 4000 ni hasara, na kwanini kwa importers kuwe na faida?

mkuu Zinjanthropus, kwa haraka haraka na achalia Mbali costs zote za ku lea kifaranga from 1 day old mpaka 19th week anapoanza kutaga. Tuanzie kuku mkubwa week 25 anataga.

breed Nzuri Kabisa bovan from Arusha, mwanza au dar Akifa ktk umri Huo anataga 80 to 85% so Kama una kuku 2000 Maana yake unaokota mayai 1600 per day. Hapo ni Sawa na trays 53 per day. Kwa standard ya feeding poultry, kuku 2000 wanakula kilo 225 Sawa na mifuko 4.5 na kila mfuko ni 39000 ukiwa Dukani. Hivo bei ya Chakula ni 175500 na kufikiri shay kwako in average 10000-15000hivyo Jumna 190500. Daily wanakunywa lita 400 mpaka 600 za maji (5000) vitamins (5000) labour, etc. mwisho wa siku ni hasara kubwa.

wakati mauzo ya tray 53 210000 na production percentage decreases as age become bigger
 
Unaona tatizo linapoanzia akija mtu na kiwanda cha poultry line ambapo kuku wake wanaanza kutaga nusu ya muda wako na anapata mayai zaidi ya shamba lako la kuku, faida zake zingine ni kuchinja na kuuza uoni kama anauwezo wa kuuza nafuu zaidi kwenye soko hilo hilo ambalo wewe unategemea mayai. Wakati yeye faida zake anajumlisha kuku na mayai ya kuuza at industrial production surely they can afford cheaper prices.

Sasa kama hizo bidhaa zinaingia sokoni na wateja hawajui ubora wa mayai kati industrial production na farm egg utamlaumu mwenye kiwanda kuzima mitambo mpaka lini au serikari ikusaidie wakati mwenzio ana technology. Challenge hapo naona ni wewe kutafuta a different segment kama hipo ambapo inatambua mayai bora yanafananaje na ujue ku-position biashara yako tofauti na mayai ya mwengine for the purposes of justifying your higher prices.

Kama aipo you know the saying if you cant beat them join them.
 

kuku hawezi kutaga wiki 9 mkuu na hap tunazungumzia juku wa mayai sio wa nyama. However ni kweli inabidi kua halima market segmentation. Ushauri Mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…