Uingereza na Canada kuendelea kusaidia sekta ya elimu

Uingereza na Canada kuendelea kusaidia sekta ya elimu

Jemmie

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2018
Posts
216
Reaction score
285
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia zimekubalina kuendelea kuimarisha programu za Mpango wa Elimu kwa walioikosa (MEMKWA) na Mpango wa Elimu Jumuishi baada ya Kumaliza elimu msingi (IPPE), ili kuwezesha wanafunzi wanaokatisha masomo kabla ya kumaliza shule waweze kuendelea na masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika Mashariki na Kusini kutoka nchini Canada Mars Andre Fredette aliyeambatana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O Donnell ambao wote kwa pamoja wamejadili masuala mbalimbali pamoja na nchi hiyo kuendelea kuisaidia Tanzania katika Sekta ya Elimu.

Waziri Ndalichako amesema nia ya serikali ni kuona kila mtoto wa kitanzania anayepaswa kupata elimu anaandikishwa na kubaki shule mpaka anapomaliza masomo yake ingawa kumekuwepo na Changamoto ya baadhi wa wanafunzi kukatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali.

“Ukitembea barabarani unakutana na watoto wadogo wakifanya biashara ndogondogo unapoongea nao wanakwambia wameacha shule ili kusaidia wazazi kufanya biashara hizo, wengine utawakuta wapo mashambani wanawasaidia wazazi kulima hivyo changamoto ya watoto kukatisha masomo ni kubwa, na ndiyo maana serikali inaona namna bora ya kuhakikisha wale wote wanaokatisha masomo wanajiendeleza”alisisitiza waziri Ndalichako

Waziri Ndalichako amesema programu ya MEMKWA inamwezesha mtoto ambaye hakwenda shule kabisa kusoma na kisha kufanya mtihani wa darasa la nne na baadaye anapofaulu huandikishwa katika mfumo rasmi na kuendelea na masomo kama wanafunzi wengine wakati mfumo wa IPPF ni kwa ajili ya wanafunzi wanaokatisha masomo ya sekondari unawawezesha kumaliza masomo hayo na kuendelea na elimu juu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Afrika Mashariki na Kusini kutoka Canada Mars Andre Fredett amesema Canada inajivunia uhusiano wa muda mrefu uliopo katika ya Tanzania na Canada ambao umewezesha nchi kupata misaada mbalimbali ya kuendeleza sekta ya elimu ambayo imewezesha watoto wa kike na kiume kupata elimu bora pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu.

Waziri wa Elimu pia amefanya mazungumzo na Balozi wa Finlanda nchi Pekka Hukka na Mkuu wa Dfid Tanzania Beth Arthy ambao wamezungumzia masuala mbalimbali ya namna bora ya kuboresha elimu nchini ikiwepo masuala ya kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu bora kwa kila mtoto wa kitanzania.
 
Donor kantri inaendelea kuwa omba omba...

Ivi hii mikopo atalipa nani?
 
If you can't beat them, join them.
Ni kwa mustakabali mzuri wa Watanzania wote, hasa wale waliopata ujauzito kwakuwa jamii nyingi bado mtoto wa Kike hajapewa thamani.
Endeleeni nao vyema.
 
Back
Top Bottom