Uhusiano wa usiku na kifo

''Allaah Anafisha nafsi wakati wa mauti yake; na zile zisizokufa katika usingizi wake, basi Huzizuia ambazo Amezikidhia mauti, na Huzituma nyingine mpaka muda wake maalumu uliopangwa. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (dalili, ishara n.k) kwa watu wanaotafakari.'' .39:42
 
Wakuu, amani iwe kwenu.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza nimekuwa nikijiuliza ni kwanini watu wengi hasa wagonjwa waliolazwa mahospitalini hufariki usiku na sio mchana?

Karibuni tushirikishane mawazo.
Usiku ni muda wa mashetani kujivijali, mchana ni wa Mungu wa kweli na malaika wema.
 
Asante kwa kufikiri kisayansi mkuu. Sisi kila kitu ni uchawi tu. Tungekuwa tunajaribu kwanza kutafuta sababu za kisayansi tunapokabili jambo kama ulivyofanya hapa kabla ya kukimbilia uchawi naamini tungekuwa kwingine kimaendeleo.
 
Mbona mi maza alifariki mchana, acha uongo mtoa mada!
 
Kila nafsi itaonja mauti! ... umemaanisha hivyo kwa sababu gani?
Kwa kuwa umesema usiku ni wa mashetani kujivinjari na mchana ni wa Mungu wa kweli
 
Kifo kama nicha mapenzi ya mungu mtu hufa mda ule aliozaliwa kama ilivyo mtoto anavyo zaliwa mda mimba iliyotunga hivyo watu wengi hufa usiku kwakua pia watu wengi huzaliwa usiku kutokana naukweli kwamba mimba nyingi hutungwa usiku
 
Muda wote Mungu anatawala,,, usiku nguvu za Giza huwa zinafanya kazi Sana'a,,,,lkn kifo hakihusian unless kuna mazingira ya nguvu za Giza,,,,wagonjwa hufa usiku kwa sababu body system zimetulia,,,normal rate and routine of blood supply inakuwa dogo,,, if no blood supply no Life,,,,
 
Kifo kama nicha mapenzi ya mungu mtu hufa mda ule aliozaliwa kama ilivyo mtoto anavyo zaliwa mda mimba iliyotunga hivyo watu wengi hufa usiku kwakua pia watu wengi huzaliwa usiku kutokana naukweli kwamba mimba nyingi hutungwa usiku
hiii ni statement mpya katika maisha yangu,asante kwa kuw nmejifunza
 
Mbona hujiulizi kwa nini kidonda hupona usiku na Si mchana? Ukitaka kuangalia maendeleo ya kidonda asubuhi
 
Hakuna sababu ya kisayansi hata moja. Ni mkururo wa usambamba (parallelism) usio na uhusiano wo wote wa cause and effect. Mwafrika na imani zake za mauzauza sijui mpaka lini. Muulize mzungu hili swali na more than 75% utapata jibu la kisayansi mf. ishu za mfumo wa damu, quality ya Oksijeni usiku, ubongo kuwa dormant kidogo usiku etc...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…