Mkuu sababu ya wagonjwa kufariki usiku ipo kisayansi kabisa , kwa kuwa wagonjwa wengi wanaofariki muda wa usiku huwa wamedhoofu na mifumo yao ya upumuaji huwa imezidiwa katika kuchuja hewa chafu na safi (O2 na CO2). Hivyo basi kwa kuwa usiku huwa hakuna hewa ya Oxygen ya kutosha kama ilivyo kwa muda wa mchana kwani muda wa mchana (day time) mimea huvuta CO2 katika kujitengenezea chakula chake na hutoa Oxygen ambayo wanyama akiwemo binadamu huitumia. Wakati wa Usiku (no Sun light) mimea hutumia oxygen na kutoa CO2 hivyo kufanya hewa ya Oxygen kupungua na kusababisha wagonjwa hasa wale waliodhoofu kukosa hewa ya O2 kwa kiwango husika hivyo kufa.