Uhusiano wa Umri na Uongozi

George Kahangwa

Verified Member
Oct 18, 2007
547
225
Wakuu,
Mojawapo ya masuala ya kiuongozi ambayo yamegusiwa sana hivi karibuni, ni uwezo wa mtu kuongoza. Wapo wanaohoji endapo kuna uhusiano kati ya umri alionao mtu na uwezo wake wa kuongoza. Jambo hili limegusa hata mijadala ya nini kiwemo katika katiba mpya tarajiwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwamba pengine kwa mfano, umri wa mtanzania kuruhusiwa kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini, unaotajwa katika katiba ya sasa, upunguzwe, uongezwe au ubakie vile vile. Sijasikia sana hoja zikijengwa kwa misingi ya kisayansi. Nimepata hata kumsikia mwanasiasa mmoja (jina naomba nisimtaje), akidai kwamba hakuna ushahidi wowote wa kisayansi kwamba umri una uhusiano na uongozi. Ni kiasi gani mwanasiasa huyu na watanzania kwa ujumla tumefanya pitio la tafiti zilizokwishafanyika kuhusu suala hili, sijui. Ni kwa sababu hiyo, natoa hoja hapa jukwaani kwamba hebu tafiti na zituambie kitu, ili hatimaye tukifanya maamuzi tusibahatishe au 'tusiingie mkenge'.

Baadhi ya maandiko ya watafiti yanaonesha kwamba, viongozi wenye umri mkubwa wamekomaa, wanatambua changamoto kwa wepesi, na wana mitazamo inayoona mbali katika kuongoza watu. Hii ni tofauti na vijana zaidi ambao sifa yao kubwa wana ari ya ushindani (soma kwa mfano; Kakabdse, 1999; Mitchell, 2000; Kabacoff & Stoffey, 2011).

Tafiti pia zimeonesha kuwa viongozi wenye umri mkubwa hutumia zaidi autokrasia katika kufanya maamuzi ya mwisho. Hata hivyo katika mchakato wa kuelekea kuamua, hupenda kuwauliza na kutafuta ushauri wa waongozwa, na utendaji wao ni wa ushirikishaji, kuliko viongozi damu changa. Lakini, wenye umri mkubwa na vijana hawatofautiani katika viwango wa kutumia mfumo wa uongozi wa 'ruksa' (rejea; Maciejewski na wenzake, 2012).

Pengine changamoto tuliyonayo watanzania, ni kufanya tafiti katika muktadha wa nchi yetu. Matharani kwa kuwachunguza viongozi wetu vijana na wale wa umri mkubwa. Kundi gani ni bora katika kipengere kipi, na akina nani ni ovyo katika uwanja upi.
Naomba kutoa hoja/kuchokoza mada.
 
Nov 25, 2012
29
0
Swala katika uongozi wa utawala na sifa za uongozi ni uzoefu ndio kigezo..umri mdogo au mkubwa sio kigezo cha uongozi...swala ni elimu, uzoefu wa uongozi na weledi wa mtu anayetaka..nimetoka kuchangia hoja kama hiyo katika mahojiano ya mb. Wa kigoma kaskazini ambaye angependa katiba ipunguzwe umri ili agombee sababu marekani na uingereza viongozi wao ni vijana..ni vijana lakini sio kama yeye.

Zitto hafai kuwa rais wa tanzania hivi sasa, atakuwa kama aliyekuwa dj akawa rais madagascar..inexperienced, greed for power, and we cant afford for on-the-job training president anajaribu kuongoza na kukosea..lets not be fooled nyerere na kawawa hawakuongoza tz hii, this is a changing world na tunahitaji someone who knows tz sio from cyberspace--no..mtu mzalendo hii ni nchi yetu sote...miaka 40 ni sawa, ila zitto hata kama amefika 40, sio sawa kwa nafasi ya urais wa nchi yetu
 

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
775
1,000
Viongozi vijana nchini Tanzania wamegawanyika katika makundi mawili. (1) Real Leaders and (2) Leaders Wannabees.

Aina hizo mbili za viongozi wanaweza kutofautsiha kama ifuatavyo:

Viongozi wa kweli huwa hawafukuzii, kufuata na kulazimisha uongozi. Badala yake uongozi huwafuata wao. Hata pale wasipotaka kuwa viongozi with time hujikuta wamewekwa katika nafasi ya uongozi na watu, mazingira au matukio. Mfano Mzuri wa viongozi wa kweli ni John Mnyika. Kijana huyu mdogo anaweza uongozi na popote alipo apende asipende hujikuta amewekwa katika nafasi ya uongozi na mazingira, watu au matukio.

Leaders wannabees, on the other hand, hulazimisha, kupigania na kugombania uongozi kufa na kupona. Hawa ni wale watu wanaogombea kila uchaguzi unaotokea. Hawa ni viongozi wanaohonga hela nyingi, kupigana kufa na kupona na kufanya lolote liwezekanalo ili kupata nafasi ya uongozi.

Mifano michache ya leaders Wannabees ni William Malecela Le Mutuz na Shyrose Banji. Vijana hawa ni mfano mzuri wa Leaders Wannabees kwakuwa ni wao wenyewe tu wanaodhani wanaweza kuongoza na hivyo huwa wanagombea kila uchaguzi, hutumia muda na rasilimali nyingi kutafuta, kufukuza na kugombania uongozi kwa udi na uvumba. Kwa kiasi kikubwa hawa ni vijana wasiojijua wala kujifahamu wao wenye. Ni watu ambao wanashindwa kuelewa wao ni watu wa aina gani na hivyo wazingatie mambo gani katika maisha. Badala yake wao wanapoteza muda kwenye suala wasiloliweza la uongozi. Utawezaje kuongoza nafsi nyingine wakati wewe mwenyewe huijui nafsi yako (kipofu anajaribu kuonyesha njia). Msomaji jiulize wewe mwenyewe, je unategemea jambo lolote la maana kutoka kwenye ubunge wa Shyrose Banji?

Viongozi wa kweli wana wafuasi (followers). Huwezi kuwa kiongozi kama huna wafuasi. Wafuasi hufuata viongozi wa kweli wapende wasipende. Leaders Wannabees, on the other hand huwa hawana wafuasi. Hata wanapolazimisha na kupata nafasi ya uongozi hakuna mtu yeyote atakaevutiwa kuwa mfuasi wao. If anything huwa wanaishia kuwa na vibaraka(puppets) wanaojipendekeza kwao ili kujipatia mradi wao (tumikia kafiri).

Mfano mzuri wa Leaders Wannabees -- wenye kundi la vibaraka -- ni Mfalme Suleiman wa Tanzania. Mzee huyu amezungukwa na kundi kubwa la vibaraka walioko busy kusema sawa mzee ili wajipatie mradi wao. Huyu Mzee ni mfano mzuri wa kiongozi feki asiye na wafuasi. Benno Malisa wa UVCCM ni mfano mwengine mzuri wa watu waliopata nafasi ya uongozi lakini wakashindwa kujipatia wafuasi kwakuwa hakuwa na uwezo, wala sifa ya uongozi.

Viongozi wa kweli wanasifa na uwezo wa kuongoza. Ukipata nafasi ya kuwajua viongozi wa kweli wewe mwenyewe utaona kuwa ni watu wenye sifa na uwezo wa kuongoza (Charisma). Ni watu jasiri, wasiofuata mkumbo, wenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu na kusimamia maamuzi yao .Wakipewa nafasi ya uongozi, hufanya kazi zao kwa ustadi mkubwa unaoleta manufaa kwa wanaowaongoza. Leaders Wannabees on the other hand huwa hawana sifa wala uwezo wa kuongoza. Wakipata nafasi ya kuongoza hufanya mambo yasiyo na manufaa na kuishia kujinufaisha wao binafsi. Ni watu dhaifu, wakufuata mkumbo, wasio na uwezo wa kufanya maamuzi magumu au kusimamia maamuzi magumu.

Viongozi wa kweli ni watu wanaosimama kwa miguu yao wenyewe kiuongozi (self made). Hawabebwi na majina, maGod Father au upendeleo. Leaders Wannabees on the other hand ni watu wasio na uwezo wa kusimama wenyewe (they are not self made). Ni watu wanaotegemea majina ya ukoo au wazazi. Na ni watu wanaopata upendeleo wa wazazi au ujamaa ili kukwea ngazi za uongozi .

Viongozi wa kweli watadumu na kuwa na maisha marefu katika Nyanja ya uongozi. Leaders Wannabees ni upepo tu- Wanakuja na kupita.
 

mtemiwao

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
384
0
Umekosea unaposema eti shy-rose na w.j.malecela ni vijana!my foot kijana gani wa above 50yrs?-malecela au kijana gana wa above 40yrs?-shyrose
 
Nov 25, 2012
29
0
[h=1]Biden turns age 70[/h][h=4]The Oval[/h]
David JacksonShare7 CommentVice President Biden(Photo: Matt Rourke, AP)
[h=3]Tags[/h]
7:32AM EST November 20. 2012 - Happy birthday to Vice President Biden, who turns 70 today.
The number 70 is significant for Biden, who has made little secret of his desire to run for president in 2016.
If Biden does run, he will try to make history as the oldest president to ever be sworn in -- by quite a bit.
The current oldest president, Ronald Reagan, celebrated his 70th birthday a month after his first inauguration; after two terms, Reagan left office shortly before his 78th birthday.
Biden would be 74 years old on Jan. 20, 2017, the day President Obama's successor is sworn in.
The vice president's age would likely be an issue if he takes the 2016 plunge, though that decision is still years away.
Meanwhile, we hope the vice president enjoys his birthday.
 
Top Bottom