Uhusiano wa mahusiano ya kimapenzi na mafanikio

Bob12

JF-Expert Member
Feb 27, 2017
11,422
58,788
Habari wana JF

Moja kati ya vitu vinavyo athiri mafanikio ya mtu ni mahusiano ya kimapenzi aliyonayo,ndo mana tunashauriwa kabla hujachagua chunguza kwanza.

Inavosemekana kuna mtu flani ukiwa nae hata kama mnapenda sana inapokuja kwenye swala la mafanikio inakua ni tofauti hata kama mnajituma katika kutafuta riziki.Lakini utakapo achana nae na kua na mtu mwingine ambaye naye hajafanikiwa, pindi mnapoanza movements za kimafanikio mnajikuta mnafanikiwa bila hata kutumia nguvu saaaana.

Hii imekaa vipi? Na kwa wale mnao amini katika maswala ya imani(za kidini) nini hasa kipo nyuma ya pazia
 
mkuu angalia usije maliza kijiji ukitafuta mwenye kuleta mafanikio kwa haraka, mm nakushauri sali sana kutokana na imani yako na muombe Mungu akusaidie uweze kuwa na mmoja ambaye mtakabiliana na yote (maisha) in a way that, Mungu atakuwa ndo mediator.
Hiyo ni idea nzuri na utakua una saidia wengi tu,ndo mana hata watumishi wa Mungu wanazunguka kila kona kufundisha na kusaidia watu wengi ambao hawajaifamu kweli
 
Na wale wenzangu na mie wanaopenda kuangalia pesa tu
Wewe ndo upo nae na unafahamu hasara na faida unazopata kwa kua nae... Kuna wengine kutoa hela kwa wasichana hakuwapunguzii kitu kwasababu wanajua nyingine nyingi tu zinaingia.
 
Wewe ndo upo nae na unafahamu hasara na faida unazopata kwa kua nae... Kuna wengine kutoa hela kwa wasichana hakuwapunguzii kitu kwasababu wanajua nyingine nyingi tu zinaingia.
Hivi unajua unaweza ukawa na hela na bado ukahitaji kua na hela zaidi?
 
Ndio najua... Ndo mana nikasema jipime wewe!!! Ukiona huitaji wapenda pesa basi ndo ivyo, wakwepe.
Hapo ni prayers tu coz kuna mtu wakati anakutongoza au unamtongoza anaficha makucha to the maximum na wengine mpk mnaingia kwenye ndoa ndo anayafungua
 
Back
Top Bottom