Uhusiano kati ya hivi viwili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhusiano kati ya hivi viwili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Jun 27, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Kama nyie ni good observants kuna uhusiano gani wa safari ya kukurupuka ya hii kamati inayoongozwa na bwana EL kipindi hiki cha Bunge? Mi naomba ziwekwe CCTVs (surveilance cameras) kum-monitor Lowassa asitie pua Uswisi! Ni hilo tu sina nia mbaya nae....

  Kamati ya Lowassa yaivaa Wizara ya Membe
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 26 June 2012 21:13 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa

  Elias Msuya
  KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imeanza ziara ya siku 14 katika balozi za Tanzania kwenye nchi za Marekani, Ulaya na Asia kukagua namna zinavyotekeleza mambo ya sera na uchumi.

  Ziara ya Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ilitangazwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar ers Salaam wakati wajumbe 20 wa Kamati hiyo na makatibu sita wanaondoka nchini.

  Hata hivyo, wakati Kamati hiyo ikienda kutembelea balozi hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe mwenye dhamana na balozi hizo, alisema ziara hiyo haikuja wakati sahihi, kwa kuwa Mkutano wa Bunge la Bajeti unaendelea.

  Lakini, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Lowassa alisema ziara hiyo imekuja wakati sahihi kwa kuwa hiyo pia ni kazi ya Bunge.

  Katika ziara hiyo, Kamati hiyo imegawanyika katika makundi sita yatakayotembelea balozi 14 katika nchi 14. Wabunge hao ni yeye Lowassa, Vita Kawawa, Khalifa Suleiman Khalifa, Rachel Mashishanga na Beatrice Shelukindo ambao watatembelea balozi za Canada, Washington na New York, Marekani na London, Uingereza.

  Wengine ni Mohamed Ibrahim Sanya, Mchungaji Israel Natse ambao watatembelea New Delhi, India na Kuala Lumpur, Malaysia.

  Kundi jingine lina Mussa Zungu, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, Betty Machangu na Mussa Hassan Mussa linaotembelea balozi za Japan na China.

  Kundi la nne litakalotembelea Ujerumani na Sweden, linawahusisha Anna Abdallah, John Shibuda na Augustino Massele, huku wabunge wengine akiwamo Mohamed Seif Khatib, Hilda Ngoye na Anastazia Wambura watatembelea balozi za Brussels, Ubeligiji na Geneva, Uswisi.

  Kundi la mwisho linalotembelea Paris Ufaransa na Rome Italia, linawahusisha wabunge John Chiligati, Engen Mwaiposa na Masoud Abdallah Salim.

  Kauli ya Membe
  Ziara hiyo imeonyesha kumshangaza Waziri Membe akisema kuwa hajui wanakwenda kufanya nini huko.
  Akizungumza na gazeti dada la The Citizen jana katika uwanja huo, Waziri Membe aliyekuwapo katika uwanja huo, alisema ziara hiyo haikuja wakati sahihi.

  “Shughuli za Kamati huko nje huwa ni kujifunza kutoka kwa wenzao kwenye mataifa tofauti, na ziara hii hilo halikufanyika….lakini nimesikia wanakwenda kutembelea balozi zetu huko nje na sio zilizoko katika bara la Afrika,” alisema Waziri Membe.

  Aliongeza kuwa, “Hapo inabidi sote tujiulize kama lengo ni kuangalia utendaji wa balozi zetu mbona sasa zinakuwa za Ulaya na Asia peke yake?"

  Waziri Membe alifafanua kuwa kwenda kutembelea balozi si tatizo, lakini katika kipindi hiki ambacho Bunge la Bajeti linaendelea mjini Dodoma, kwa busara ya kawaida, mbunge anatakiwa kuwa bungeni akifuatilia Bajeti.

  Alisema kulingana na ratiba ya Bunge, ziara kama hiyo ilitakiwa kufanyika wakati wa vikao vya Kamati za Bunge, lakini si sasa ambapo Bunge linakutana.
  Licha ya kukanusha mara kwa mara, Waziri Membe na Lowassa wamekuwa wakitajwa kuwania Urais kupitia CCM siku za usoni, jambo ambalo limekuwa likiwataja wabunge hao kama mahasimu wa kisiasa.

  Kilichotokea kwenye kamati
  Tayari Kamati hiyo imewahi kuripotiwa kuingia katika mvutano Membe, ambapo Juni 6, mwaka huu ilimbana ikisema alichelewa kugawa vitabu vya bajeti yake kwa wajumbe wa Kamati.

  Mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo aliliambia gazeti hili kwamba wajumbe waligomea Bajeti hiyo kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho na kutokuonyesha madeni ya wizara yakiwamo makato ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

  Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara hiyo, Assah Mwambene alipinga taarifa hizo, lakini akafafanua kilichotokea kuwa hoja ya vitabu kuchelewa iliibuka, na tayaru waziri aliwaeleza wajumbe kuwa hilo ni suala ambalo lilitokana na kamati husika.

  Alisema vitabu hivyo viliwasilishwa mwisho wa wiki, lakini kwa kuwa labda haikuwa siku za kazi, ndiyo maana havikuwafikia mapema wajumbe.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  Kamati ya Lowassa yaivaa Wizara ya Membe

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Vigogo waficha bilioni 300 Uswisi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 25 June 2012 21:43 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Mwandishi Wetu
  KITENGO cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kinachunguza Sh303.7 bilioni ambazo zinadaiwa kukutwa kwenye akaunti sita za Watanzania, wakiwamo wanasiasa, katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

  Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya Interpol kilichonukuliwa na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen, kimesema baadhi ya wanasiasa nchini na watu wengine ndiyo wanahusika na ufisadi huo kwa kuwa na akaunti zenye fedha nyingi nchini Uswisi.
  Fedha hizo zimeelezwa ziliingizwa katika akaunti hizo na kampuni za uchimbaji mafuta na kampuni za uchimbaji madini, ambazo zinafanya kazi Tanzania.

  Chanzo hicho kiliongeza kwamba fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti, zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa.

  Kiasi hicho cha fedha kilichofichwa Uswisi, kinatosha kuendesha Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa miaka mitano, au kusaidia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuendesha shughuli zake kwa miaka miwili.

  Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi moja.

  "Wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini," kilidokeza chanzo hicho.

  Mabilioni hayo yamebainika kufichwa wakati takwimu zilizotolewa na Umoja wa Taasisi za Kupambana na Rushwa barani Afrika ikiwamo Tanzania, zikionyesha kwamba Sh22 trilioni, zimekuwa zikitoroshwa nchini humo na kufichwa katika nchi za kigeni, ikiwamo Uswisi.

  Fedha hizo zimebainishwa na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB), iliyotolewa hivi karibuni, ikibainisha nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, na kiwango cha fedha zake zilizohifadhiwa huko.
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hivi sasa inafuatilia suala hilo kwa mamlaka za Uswisi, ili kujua fedha hizo ziliko na nani anazimiliki.

  Mbali ya Tanzania, nchi nyingine ambazo zina fedha nyingi katika benki za Uswisi ni Kenya (dola 857 milioni), Uganda (dola 159 milioni), Rwanda (dola 29.7 milioni) na Burundi dola 16.7 milioni.
  Jumla ya fedha zilizoko katika benki za Uswisi kutoka nchi hizo nyingine za Afrika ni Faranga 1.53 trilioni za nchi hiyo na ripoti hiyo imeelezwa kuwa kuna msukumo wa kimataifa wa kuitaka nchi hiyo izitake benki zake, kubadilishana taarifa za wateja na serikali za kigeni.

  Ripoti hiyo imekuja wakati pia Uswisi ikiwa na rekodi ya kuhifadhi mabilioni ya dola kutoka nchi za kigeni ikiwamo Afrika, kwani iliwahi pia kuhifadhi dola zaidi ya bilioni 1.5 za aliyekuwa Kiongozi wa Kijeshi wa Nigeria, Jenerali Sani Abacha na dikteta Mobutu Seseseko wa iliyokuwa Zaire.

  Gavana azungumza
  Akizungumzia ripoti hiyo, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndulu (pichani) alisema uamuzi huo wa Uswisi wa kuanza kufungua milango utaiwezesha BoT kuwa na rekodi ya kiasi halali cha fedha zilizopo katika nchi hiyo.

  Profesa Ndulu alifafanua kwamba katika siku za nyuma, Uswisi haikuwa imefungua milango kwa kutaja kiasi cha fedha za wateja wake walioweka fedha katika benki zake, hivyo ilikuwa vigumu kwa mamlaka za ndani kuweza kufanya uchunguzi.

  "Ndiyo kwanza wameanza kufungua milango, sisi siku zote tulikuwa hatuwezi kujua nini kinaendelea. Lakini, angalau sasa tutaweza kujua na kuwa na rekodi baada ya uamuzi huo wa kufichua kiasi cha fedha kilichomo katika benki zake," alifafanua gavana.
  Kiutaratibu, BoT inapaswa kuwa na rekodi ya fedha halali za Watanzania zilizopo nje ya nchi.

  Kauli ya Takukuru
  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alikaririwa na The Citizen hivi karibuni alisema kuwa ofisi yake ina taarifa kuhusu suala hilo na kwamba wanaanza mawasiliano na Serikali ya Uswisi kujua ukweli wake.

  Dk Hoseah alisema taasisi hiyo inataka kujua jinsi gani fedha hizo ziliwekwa kwenye benki za Uswisi, watu waliohusika na namna uhamishaji wa fedha hizo ulivyofanyika.

  "Tutakapogundua fedha hizo zimetoka wapi, tutafuata taratibu zinazohusika kuhakikisha zinarudi nchini," alisema Dk Hoseah na kuongeza: "Tutatumia sheria zilizopo katika nchi hizi."

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa yuko likizo, hivyo aulizwe msemaji wa Jeshi la Polisi.
  Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema hawajapata ripoti hiyo na kwamba atawaomba watu wa uchunguzi kumpatia, ili aweze kutoa taarifa.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Vigogo waficha bilioni 300 Uswisi
   
 2. v

  vngenge JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kila m2 hajui sasa hizi kodi zetu tuanzowalipa ni za nini?. Pesa nyingi sana hizi jamani zinaweza kujenga kilomita 500 za barabara ya lami. Inatia uchungu
   
Loading...