Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,983
- 5,801
Jana ilitolewa taarifa kuwa wapinzani wa siasa za Kenya; Uhuru na Raila walikutana na kumaliza tofauti zao kufuatia uchaguzi mkuu wa 2017.
Baada ya mkutano wao, Rais Uhuru alisema kuwa ni wakati wa kubadili mwelekeo wa siasa za Kenya na kuwa Kenya ni kubwa kuliko mtu yoyote na wao viongozi wanapaswa kukaa pamoja na kujadiliana kwa uhuru kero za nchi.
Kwa upande wake, Raila alisema wamekubaliana na Uhuru kuzima migawanyiko na kuwa pamoja.
Kwa upande wetu Tanzania naona migawanyiko inazidi, Rais naona kama anaamini sana juu ya matumizi ya nguvu ktk kuwadhibiti wenye maoni tofauti na yao na kusababisha msuguano na migawanyiko mkubwa baina ya Rais na wapinzani kiasi kwamba wapinzani wamebanwa sio kwa hoja wala sheria bali kwa kutumia mabavu. Hata vyombo vya habari navyo vinabanwa na kutishwa pale wapoonekana kukosea au kukosoa watawala.
Yanayotokea Ethiopia ambapo pia kwa muda mrefu wapinzani na wenye maoni tofauti na watawala wamebanwa, kutishwa na kufungwa jela naona hayatusaidii. Vurugu zimezozuka huko hazijatusaidia kutufundisha kuwa nguvu hazisaidii bali kujenga ufa miongoni mwa wananchi.
Mimi kama Mtanzania sioni kama hali ya kisiasa ni tete kama ambavyo dola na watawala wanavyosema kwenye kauli zao (Rejea hotuba ya Rais jana, Polisi na CDF). Kauli zao naona kama ndio zinaleta hofu na migongano badala ya umoja na utengemano.
Tujifunze kwa Uhuru na Raila, tuangalie yanayojiri Ethiopia kwa akili. Naomba nimnukuu Mzee Tupatupa : "Tunashindana kwa hoja, bunduki ni za nini? "
Vv