Uhuru Kenyatta: Mapolisi mwambieni anayewatuma msisumbue familia yangu. Nikamateni Mimi niko hapa acheni uwoga!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,168
142,304
Haya mambo ya Uongozi ni magumu Sana Hata ukistaafu basi utaandamwa tu mimi ndio sababu Nampongeza Sana mzee Mwinyi Ruksa alipostaafu tu alikimbilia Msikitini na kujikita na mambo ya muumba tu

Nchi jirani ya Kenya Rais Ruto anampelekea moto Boss wake mstaafu Uhuru Kenyatta na kuizongazonga familia yake akiwemo mama na mtoto wake

Uhuru kamtolea uvivu Ruto kwa kumwambia amkamate Yeye asizungukezunguke tu na kuwasumbua Wanawake na Watoto

Kupitia Citizen TV Uhuru ameonekana alimwambia Ruto kwamba kuanzia sasa atailinda familia yake kwa gharama yoyote ile

Duh.... Ukiona kwako kunafuka Moshi just kwa mwenzako moto unawaka

Mlale Unono 😃
 
Wana katiba nzuri sana lakini?
Tuliokuwa tunafahamu na tunasema kuwa katiba mpya hata iandikwe vipi siyo mwanzo au mwisho wa matatizo hatukueleweka.

Kudai katiba mpya ni turufu tu ya upinzani uliokosa sera. Kwa sababu katiba inaweza ikabadilishwa kidogo kidogo vifungu vikaongezwa au vikapunguzwa au vikarekebishwa.

Waafrika tu wajinga sana na hatutafikia mwisho wa ujinga kwa muda mrefu sana. Ujinga tulionao siyo wa asili ni wa kupandikizwa na huo ni mbaya zaidi kuliko ujinga wa asili.
 
Kama katiba haina msaada basi teueni mgombea urais wa miaka 25 ,na pia Samia aongoze mpaka 2030 bila uchaguzi.

Ukiona Kiongozi anasiliba katiba means anacheza na loopholes zilizopo kwenye katiba lakini kukiwa na katiba konki hakuna yeyote atakayekiuka ndiyo maana hamjawahi kuteua mgombea urais mwenye umri chini ya miaka 40 au rais akaendeleza kipindi cha pili bila kufanya uchaguzi mlioweka kila baada ya miaka mi5 ,mbona hayo mnafuatisha? Mnafuatisha kwasababu yapo straight hakuna mbambamba(loopholes).
 
Kama katiba haina msaada basi teueni mgomea urais wa miaka 25 ,na pia Samia aongoze mpaka 2023 bila uchaguzi.

Ukiona Kiongozi anasiliba katiba means anacheza na loopholes zilizopo kwenye katiba lakini kukiwa na katiba konki hakuna yeyote atakayekiuka ndiyo maana hamjawahi kuteua mgombea urais mwenye umri chini ya miaka 40 au rais akaendeleza kipindi cha pili bila kufanya uchaguzi mlioweka kila baada ya miaka mi5 ,mbona hayo mnafuatisha? Mnafuatisha kwasababu yapo straight hakuna mbambamba(loopholes).
Kwani iliyopo sasa inasemaje?
 
Back
Top Bottom