Uhujumu wa tanesco, je wewe unahusika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhujumu wa tanesco, je wewe unahusika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanahisa, Jul 30, 2012.

 1. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Leo tujihoji wadau, umewahi mara ngapi kulihujumu shirika la Usambazaji umeme Tanzania (TANESCO),
  [​IMG] kwa kuleta vishoka nyumbani literally (fundi tanesco) kuibana mita ipunguze mwendo?
  [​IMG] Kuweka sumaku (magnet) ili kisahani kipunguze mwendo maana hapa ukiwasha jiko la umeme plate moja tu kisahani kinakwenda over fan.

  [​IMG] Hapa advanced kidogo, umeweka utepe wa mkanda wa video kwenye punch card ili sindano ikishuka kutoboa card itulizane umeme wa buku tatu unapigwa kwa miezi mitatu, full AC, BBQ, Water heater kama kawa.

  Tujuze wewe umeshatumia style gani kuhakikisha unakwenda sambamba na Tanesco. Karibu
   

  Attached Files:

 2. F

  Fofader JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Soul searching.........
   
 3. m

  mwenzetumwenzetu New Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inauma sana hii. Nilisoma juzi juzi hapa kuwa mapato yameongezeka kutoka shs. billion 57 hadi billion 85 mara baada ya kusimamishwa mkurugenzi. Haijapita wiki tatu tangu hii itokee. Matumizi yote kwa mwezi ni karibu shs. Billion 11. Inamaanisha Tanesco ina-ziada ya shs billion 74. Hizi pesa nyingi kiasi hiki zinakwenda wapi na kwanini itoke ruzuku tena serikalini? Tumeambiwa mafuta ya PUMA yana-save kiasi cha shs billion 6 kwa mwezi na kama yangenunuliwa kwa watu binafsi basi hizi billion 6 zingeishia kwa wachache- ambayo ndio wanatusumbua hapa mjini na magari na majumba ya kifahari kwa wizi tu.

  Hivi kama kuna ziada kubwa kiasi hiki, kwanini umeme usiteremshwe bei hata kwa asilimia 60 ili watu waweze kununua umeme na kuacha kutegemea mikaa na pia kuacha kuiba umeme? Suala la kuiba umeme halijaanza siku nyingi, watu wameshindwa kabisa kununua umeme ambao kila siku unapanda bei na umekuwa bei ghali kuliko hata mishahara yao. Wachachwe wanatuibia mamia ya mabillion ya shilingi halafu wengi wanateseka kwa umeme kuwa ghali kuliko maelezo. Kumbe watu wengine wanazima mitambo wengine wanafanya makusudi kuua machine ili waweze kununua mafuta wapate mabillion ya pesa.Watu wanashindwa kununua umeme maana ni ghali mno.

  Tumekimbilia kununua gas amabyo mtungi wa kg 15 ulikuwa shs. 23,000 lakini leo ni shs 54,000 maana watu walimbilia kununua gas baada ya umeme kupanda bei kutokana na ufisadi wa viongozi wetu.Vishoka wa Tanesco wameelewa hili ndio maana nao wana kula kwa ujanja wao kwa kuwaunganishia watu umeme au kuchezea Luku maaana umeme haununuliki. Watu wanaiba umeme kutokana na gharama kubwa inayotokana na wizi wa mabillion ya pesa. Umeme uteremshwe bei tuone kama maisha hayatakuwa bora kwa watanzania.

  Tunajua hata gas kuna watu wanafaidi ndio maana hakuna mtu anayelalamika. Hii gas inayotoka kusini haiwezi kusaidia bei ya gas kushuka? Jamani hatutaki kutumia kuni na mkaa, umeme na gas ni bei rahisi kama ufisadi utapigwa vita. Tusamehane na tuanze ukurasa mpya, kila mwenye kosa ajirekebishe na kama ulishakula pesa zako- mabillion basi yanakutosha.Anza kuwekeza zitawatosheni na familia zenu. Mungu awabariki sana

   
 4. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kweli mkuu ni vizuri kujichunguza!
   
 5. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umeme wa Tanzania ndio ghali kuliko nchi yoyote duniani.
  Tsh 700/ kw sawa na 0.46$ USD. Tanzania pekee.
   
 6. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=3]Picha yetu Jumatatu Hii:Mr and Mrs Rwakatare[/h]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"][FONT=&quot]Pichani anaonekana Mchungaji Dr Getrude Rwakatare kulia akiwa na mumewe wakati wa harusi ya mtoto wao wa mwisho Bw Mutta Rwakatare alipokuwa akifunga ndoa siku ya juzi jumamosi tarehe 26.05.2012.Ndoa ilifungwa katika kanisa la Mikocheni na Harusi ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City.[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 7. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ndiyo!!!!!!!
   
 8. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu KING KING,tuelezee wewe ulihusika vipi?
   
 9. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,746
  Trophy Points: 280
  Nafsi inazungumza! Inawezekana ukasema nyama huli, lakini supu yake ukatumia!
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  naona umeshatufundisha njia ya kuiba umeme nlikuwa sijui
  kumbe nikiwa na sumaki mambo safi sana alaaaahhh
  kama wao wahusika wanaiba kwanini nami nsiibe?
  nani anaemfahamu mfanyakazi wa tanesco anelipia umeme?
   
 11. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii nimeipenda, kweli mvi sio ishara yakua na hekima.lol
   
Loading...