Uhujumu wa mali za asili Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhujumu wa mali za asili Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GOMASI, May 20, 2011.

 1. GOMASI

  GOMASI Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepata habari kutoka gazeti la Raia Mwema la wiki hii kuhusiana na habari za uhujumu wa uchumi kwenye wizara ya maliasili. Habari hii kutoka ndani ya moyo wangu imenihuzunisha sana kama sio kunitia kichefuchefu.

  Ndio maana nimeamua nitapikie bakuli hili la jamii forum. Watanzania wenzangu taifa hili la Tanzania limegubikwa na kashifa nyingi kila kukicha. Sijajua kama viongozi wetu wanazidi kujipanga kuboresha au wanajipangua.

  Wananchi wenzangu kama kweli wote tuna uchungu na rasilimali za taifa hili kwa manufaa yetu wenyewe na vizazi vijavyo, naomba tusaidiane mawazo kuhusiana na jambo hili la kutia taifa letu umasikini wa kuua.

  Kumetoroshwa wanyama pori 130 wa aina 14. Wanyama hawa ndio hao mnaosikia wanaliingizia taifa kipato kupitia utalii na mambo yanayohusiana na hayo. Mbali na hilo maliasili ndio uhai wan utamaduni wa taifa letu ndio maana TWIGA anatumika kama nembo ya Tanzania.

  Kati ya wanyama waliotoroshwa na Mpakistani mmoja kwa ndege ya jeshi la Qatar kwa ushirikiano na watanzania wenzetu ni TWIGA NEMBO YA TAIFA wapatao 4. Je Kwa jinsi ninavyofahamu umakini wa vyombo vyetu vya usalama ni kweli jambo hili halikuwa na taarifa kwa wakubwa?

  Kwa mambo ya ajabu yanayotendeka hapa nchini naamini kuwa ni dili kati ya hawa wakubwa wetu wa nchi. Kidole cha kwanza ninamnyooshea waziri wa maliasili na utalii ambaaye kwa jina anajulikana.

  Kama sio kweli, ni kwa nini wanyama hawa walipakiwa kwenye ndege uwanja wa ndege KIA vyombo vya usalama hawakuonyesha juhudi zao kudhibiti uharamia huu?

  Lakini pia jambo la kujiuliza ni kwamba wahusika wa forodha waliruhusu vipi upakiaji wa maliasili zisizokuwa na nyaraka halali za kusafirisha maliasili kwenda nje ya nchi?

  Na hata kama huyu mpakistan angekuwa na nyaraka hizi hairuhusiwi kusafirisha TWIGA NEMBO YA TAIFA nje ya nchi.

  Naomba maoni yenu watanzania
   
Loading...