Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Sheria ni msumeno mkuu
Unapotaka kupambana na serikali yoyote duniani hakikisha kuwa ni msafi na huachi alama yoyote chafu

Tetea uovu maana uko kwenye meza ya mfalme unakula na kusaza.
 
Acha kulia lia kama mwanamke,jikite kwenye sheria

Kama mamaako analialia haimaanishi kila anayekemea uovu, atakuwa kama mama yako. Sheria tunazijua na uonevu kwa kutumia sheria tunaufahamu.
 
Si kww
Sheria ni msumeno mkuu
Unapotaka kupambana na serikali yoyote duniani hakikisha kuwa ni msafi na huachi alama yoyote chafu
Si kwweli pia serikali safi huwa hazina wakosoaji ni tawala dhalimu tu
 
Wakati huo huo mahakama nazo hazishinikizi kwa watawala kuharakisha upelelezi!

Mtu anaendelea kusota ndani kwa kukosa dhamana, miaka na miaka!
Dpp msukuma unategemea amuangushe ndugu yake
 
Wacha iendelee kuwepo ili iwakute hawa waliyoiweka. Ipo siku tu
Pana watu utembea gizani unawahurumia kesho yao,hakuna mwanadamu yeyote pasipokujali hadhi yake ajuaye kesho yake.Mwisho wao si mzuri
 
Mzee angekuwa anapitia hizi nyuzi jf zingempatia angalau ka utu fulani, kutukanwa au kusemwa vibaya mara zote sababu huwa kwa mtukanwa mwenyewe.
Chuki za mwanzo kabisa, visasi vya mwanzo kabisa, ubaguzi wa mwanzo kabisa wale walio kuchagua na wale hawakukuchagua ungewaleta pamoja nna uhakika kusingekuwa na tusi.
Haki ya kuchagua na kuchaguliwa ingetumika hapo mwanzo kabisa, haki za kisiasa zingetumika hapo mwanzo kabisa kusingekuwa na tusi.

Mbona tulianza vizuri licha ya haki kutotendwa, kuchimbua makaburi hapo mwanzo kabisa, kungefanywa kisheria na maelekezo mazuri. Naogopa kuendelea kusema nisije kukamatwa tena mie sina hata wakunisemea hivyo vihash tag

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vizuri unavyojaribu kutoa maoni ambayo kwa hakika yana uzito. vile vile tujaribu kuangalia upande wa pili wa wakosefu. na jee mbona wewe upo njee. Zungumzia na wakosefu pia ili hoja yako iwe nzito vya kutosha. Mkosefu kioo chake ni mahakama, na kila ujuaji huzaa ujuaji. hili suala ni fikirishi kwa mwenye uelewa wa mahusiano ya jamii.
 
Uta waambia nini wabunge wa Ccm wanao pitisha kila kitu kwa ndioo halafu ukimuuliza umeunga nini mkono hajui? Inatakiwa kuwe na bunge lenye wawakilishi serious sio wale wanao ongelea congo dust..
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uta waambia nini wabunge wa Ccm wanao pitisha kila kitu kwa ndioo halafu ukimuuliza umeunga nini mkono hajui? Inatakiwa kuwe na bunge lenye wawakilishi serious sio wale wanao ongelea congo dust..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ujumla wabunge wengi wa CCM ni mzigo.

Mambo mengi ya ovyo yasingekuwepo kama tusingekuwa na Bunge la ovyo. Mifumo ya kutenganisha mihimili iliwekwa na mataifa yenye watu wenye uwezo wa kufikiri vizuri, wanaofikiria mataifa yao na watu wao badala ya vyama vyao, baada ya kuujua ukweli kuwa madaraka hupofushwa.

Lakini hapa kwetu, pale ambapo serikali inapopata upofu, bunge lililotakiwa kutoa mwongozo, lenyewe linakutwa likiwa kipofu na kiziwi.
 
Sisi tunaitazama zaidi serikali na watawala maana hawa walistahili kuwa na hekima kubwa kwa vile waliapa kutumia hekima na kutenda haki wakati wote.

Ukiona huna moyo wa uvumilivu, wala huna uwezo wa kukubali kulaumiwa na kupokea maoni ya watu, na hasa wale ambao wanaweza kuhoji na kukosoa bila staha, ujue huna karama ya uongozi. Usiutafute uongozi.

Unaowaongoza, hawana mafunzo namna ya kuuliza, kuhoji au kukosoa. Yakubidi kiongozi uyapokee yote bila ya kisasi wala chuki.
 
Asante sana elimu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…