Uhitaji wa kubadili hukumu mbali mbali za kodi, makosa ya barabaran

zuberi Abraham

JF-Expert Member
Feb 13, 2016
480
389
Wana Bodi

Nimekuja na wazo hili Nchi yetu imepata kiongozi mzuri sana na amekua akijitahidi kufanya yalio mengi kwa muda mfupi na yamekua na Impact kubwa kwa kiasi fulani, Na katika hatua zake hizo muheshimiwa Raisi wetu JPM amepata support kubwa kwa wananchi lakini kwa nguvu ya kwake pekee itafika pahala atashindwa kwasababu sheria zimekua nyepesi sana Tanzania.

Tuanza na baadhi ya penalty na interest wanazotakiwa kulipa makampuni na watu binafsi wanapokwepa kodi illegally. Anayekwepa kodi anatakiwa kulipia 2.5% ya kodi aliyokwepa ama 100000. Na mtu binafsi 10000 au 2.5% ya kodi aliyokwepa. Ila kama tungekua na sheria kali za kifungo na penalty ya around 40% ya kodi naamin hata wafanyabiashara wangeogopa kukwepa kodi.

Pili ni hili sakata la sukari wenzetu uingereza ukicreate artificial demand kwa kuficha bidhaa unahukumiwa kifungo cha miaka 5 je sheria yetu inasemaje na tunazifuata.


Tatu ni sheria za kuzidisha mizigo kwenye magari yetu. Gari lina ruksa ya kubeba Tani 7 unalikuta na tani 10 sheria kwa tanzania wanalipia laki 5 au laki mbili na nusu kama sijakosea. Ila kwa wenzetu UK ni £5000 kwa tani uliyozidisha sasa hapa uone ni kiasi gani tunasheria rahisi hizi.

Ni wazo tu Wanabodi
 
Kama darasa la 7 yuko bungeni unategemea sheria itakayotungwa iweje? Lazma iwe rahsi.
 
Back
Top Bottom