Uhifadhi Wanyamapori kwa njia ya Katuni

Mdau Makini

Member
Sep 18, 2012
70
10
Poleni na Majukumu ya Kujenga taifa ndugu zangu!!
Mimi ni Mtanzania niliyesomea kuhusu mambo ya Uhifadhi wa wanyamapori yaani Bsc.Wildlife Management. Kutokana na wasanii wetu walio wengi kujikita katika uelimishaji wa jamii yetu kwa njia ya katuni katika mambo ya Siasa na mapenzi pekee, nimeona ninaweza pia kufikisha ujumbe wa uhifadhi wa wanyamapori wetu kwa njia ya Katuni, hasa katika mitandao ya kijamii ambayo watu wengi wanafika kuliko kwenye mapori yetu halisi. Kwa kuanzia nimeanzisha page Facebook inaitwa WILDLIFE CARTOON TZ. Huko kuna katuni zenye ujumbe tofauti tofauti lakini mlengo wake ukiwa ni uhifadhi. Japo page hiyo itakuwa na mkusanyiko wa katuni nilizo chora mwenyewe na baadhi kutoka kwa watu wengine. Ukiwa kama mdau wa uhifadhi, mwanajamii na kama Mtanzania ambaye Wanyamapori ni rasilimali yetu, ninakuomba utembelee ukurasa huo wa Wildlife Cartoon Tz ili uweze kujifunza, kushauri,kukosoa na kupendekeza pia kuhusu uhifadhi wa hifadhi zetu.Pia kama una katuni zinazohusiana na wanyamapori unaruhusiwa kuzipost kwenye page yetu chamsingi watu waburudike na pia kuelimika kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori. Zaid ya hivyo, unaweza kunishauri njia nzuri zaidi ya kuweza kuchora katuni au program rafiki zaidi kwa kazi hiyo.Ukivutiwa na Page yetu usisahau Ku-like, Ku-share na Ku-invite watu wengine ili tujifunze wote kama jamii ya Watanzania. AHSANTE KWA USHIRIKIANO WAKO.
 
Mkuu labda ungewaomba mods waweke jukwaa la watoto au peleka TBC 1 maana huko ndiyo kuna cartoon
 
Back
Top Bottom