Goodluck Mshana
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 1,271
- 1,119
Hebu ifike pahala CCM muwe watu wazima na kuacha Siasa za kijinga na za kitoto. Ni dhahiri kwa idadi ya madiwani wa UKAWA lazima watatengeneza Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Michezo mnayoifanya mnasababisha watu wengine wadhalilishwe na kutiwa aibu mbele ya jamii na familia zao. Ninamuona Mama mtu mzima anavyochapwa makofi na vijana! Mmemuacha peke yake huku nyie mkiwa maofisini mmetulia. Shame!
CCM lazima mkubali kuwa mlizidiwa kwenye uchaguzi Mkuu. Mkaelekeza nguvu na rasilimali zote kwa Lowassa. Mkanununua media, watu na hata kura. Mkasahau ya Jiji la Dar es Salaam. Mkasahau nguvu ya madiwani baada ya uchaguzi. Mkasahau kuna swala la Meya! Leo mnastuka tayari UKAWA wamewazidi kete. Kubalini yaishe na muwaachie UKAWA waendeshe Jiji. Jipangeni kwa uchaguzi ujao ambao hamtawasahu madiwani na kuelekeza nguvu na fitina kwa mgombea wa UKAWA.
Na labda niwakumbushe kitu. Hakuna mwenye hati miliki ya kuiongoza Tanzania. Zanzibar mlichemka hivyo muachieni Maalim Seif ili wazanzibari waendelee na maisha yao. Tuliamua kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Hivyo tukubaliane na matokeo yake. Tuukubali uzao wa vyama vingi ambapo chimbuko lake ni demokrasia. Tukubali na kuheshimu maamuzi ya sanduku la kura yasije tukuta ya Misri, Kenya na ile aibu anayoitenda Museveni pale Uganda.
Tuwe na utamaduni wa kuheshimu maamuzi ya wananchi. Wanapopiga kura huwa na lengo la kuadhibu upande dhaifu. Upande ambao haukukidhi haja ya maendeleo yao. Watanzania hawajafikia kushikiana mitutu ili kuingia kwenye Uongozi. CCM kisitupeleke huko. Rafu mlizocheza kwenye uchaguzi Mkuu zinatosha na sasa wapeni UKAWA kipande cha Nchi waongoze. Watanzania wawapime kwa weledi na uchapa kazi wao. Wakiharibu basi 2020 wananchi waamue vinginevyo.
Miradi na mipango ya Jiji imesimama. Hakuna wa kuliongoza Jiji kisa Siasa chafu na za aibu. Ni kichekesho kuona naibu Meya anaahirisha uchaguzi eti kwasababu ya zuio la Mahakama! Kama kulikuwa na zuio ikawaje aitishe uchaguzi?! Je, kama CCM wangekuwa na idadi kubwa ya madiwani mpaka sasa Jiji la Dar es Salaam lingekuwa halijapata Meya kutoka CCM?! Tungetumia muda gani kumpata Meya? Na je, historia inasemaje kuhusu namna na muda wa kuchaguliwa mameya waliopita chini ya CCM? Tuache Siasa za mabavu yasiyo na tija kwa Taifa letu.
Na Goodluck Mshana
Mfuasi wa ghafla wa Donald Trump