Uharibifu wa viti zaidi ya 200 uwanja wa Taifa DSM wakati wa mchezo wa Yanga na Simba

simba imeonewa, ingefaa hiyo M5 alipishwe huyo refa aliye sababisha mashabiki wangoe viti
Hata wewe ni mwendawazimu kama hao waliofanya uharibifu tu! Kwani viti ndio vilifanya makosa? Kwa nini wasiingie uwanjani wakapambane na refa kama wanaona kakosea!
 
Ni kweli kabisa kwakuwa ile sio netball bali ni football
Kama refa na lineman hawakuona ni kitu cha kawaida..... inatokea na ni sehemu ya mchezo. Hata Maradona alifunga kwa World cup. Mbaya ni kama waamuzi waliona na kuachia TFF wamuadhibu baada ya kupokea taarifa ya mchezo ndiyo utaratibu. Siyo kufanya vurugu
 
Ningekuwa Mimi ndo kiongozi.ningeng'oa viti vyoteeee.wakija kuangalia mechi wakae chini au wasimame.upuuuzi huo.ila Simba nguvu moja.
 
Kama refa na lineman hawakuona ni kitu cha kawaida..... inatokea na ni sehemu ya mchezo. Hata Maradona alifunga kwa World cup. Mbaya ni kama waamuzi waliona na kuachia TFF wamuadhibu baada ya kupokea taarifa ya mchezo ndiyo utaratibu. Siyo kufanya vurugu
ila yanapotokea maamuzi mawili makubwa dhidi yako tu hapo haiko sawa! Unafunga goli halali linakataliwa na unafungwa goli haram linakubaliwa, hapo haiko sawa!!
 
TFF iache kutumia marefa wa ndondo cup kwenye mechi kama hizi.

Hata kama Simba itaadhibiwa lakini watu wameonesha hisia zao.
 
simba imeonewa, ingefaa hiyo M5 alipishwe huyo refa aliye sababisha mashabiki wangoe viti
Sasa ndugu tuseme kila timu inayoonewa na refa mashabiki wake wang'oe viti huo uwanja si ungebaki mtupu?
 
Huyu nae vipi!?Kwani viti vimekua roho vikitoka havirudi! Tutalipa ila sms imefika next time ujinga kama huu tunaondoka na magoli
TFF wamesema hakuna mashabiki kuingia tena uwanjani michezo minne, kwa hiyo mechi za simba na yanga zitachezwa bila mashabiki
 
ila yanapotokea maamuzi mawili makubwa dhidi yako tu hapo haiko sawa! Unafunga goli halali linakataliwa na unafungwa goli haram linakubaliwa, hapo haiko sawa!!
Ni kweli haipo sawa lakini chukua maamuzi sahihi siyo nawe ufanye makosa katika kosa
 
Mimi nawaomba Simba siku nyingine tujitahidi hata kungoa zaidi ya nusu labda tutasikilizwa tumelalamika vyavkutosha sisi ni wa kuonewa tu...au sisi ndiyo watakatifu sana huyo refa siku nyingine angalau apate hata kikofi...
Yaani nyie Simba mkifungwa mnalalamikaaaa, lakini mbona Yanga hawalalamiki kama nyie,? Timu yenyewe ya kumfunga yanga hamna afu mnakujatokwa povu huku kaa lipumba
 
Back
Top Bottom