Uhamisho wa mtumishi bila malipo

FLYAIR

Member
Jul 11, 2015
23
9
Ndugu zangu poleni na majukumu..
Hivi tuulizane jamani, inawezekanaje halmashauri kuwapangia vituo vipya watumishi (uhamisho ndani ya halmashauri bila malipo) tena kwa vitisho usipoenda ilhali sheria ipo wazi kabisa.

Sasa swali ni je kwa mshahara wa sasa kama wa mwalimu chukulia amepanga nyumba na amelipa kodi kwa miezi 6 na ametumia pengine miezi 2 au 1 na unaambiwa unatakiwa kuhama pasipo kupewa hela yoyote, hivi ndivo tamisemi walivowaagiza kweli?

Halmashauri wajitathimini kwanza kabla ya kufanya haya mambo yao ambayo binafsi naona sio sahihi kwa mtumishi ili hasa walimu waweze kufanya kazi kwa weledi na moyo. Hili limeshawatokea baadhi ya walimu wa IGUNGA Tabora.

Nawaomba tamisemi waweze kuangalia hili tatizo ili watumishi waweze kupata haki zao kwani huku ni kuteswa.
 
Huku tanga nako kuna upuuzi huohuo labda ni maelekezo toka juu,sijui hii nchi ina matatizo gani aisee, mwanzo wanakuambia fedha zimeshakuja kila halmashauri now watu wanatishwa kifa.la
 
Nenda karipoti urudi,andika barua za kuomba malipo yako ili uweze kwenda kituo kipya cha kazi
 
Chukua barua ya uhamisho nenda karipoti kituo kipya halafu omba ruhusa urudi ushughulikie madai yako ya uhamisho, hapo kama ni mtego hawakupati ng'o
 
Back
Top Bottom