Je kwa watakaodanganya kwa kigezi cha kiafya wafanyweje ? Je watagundulikaje wakati wengine ni wataalamu wa afya wengine ma afisa utumishi? Huoni kuna changamoto kubwa? Kwanini masuala yao ya kiafya yawe hot baada ya tamko hili?Kwa takribani mwaka mzima uhamisho kwa watumishi wa umma umezuiliwa. Kwa kuwa haijulikani ni lini utaruhusiwa, mimi nashauri ni bora kwa wale walioomba kuhama kwa sababu za kiafya wakahamishwa tu ili kuongeza tija kazini.
Kuna watu swala la uhamisho wanalifanya kisiasa, yaani imekuwa ndo sehemu ya kuonyesha mahaba yao kwa chama bila kuliwazia kwa kina hasa athari hasi zitokanazo na zuio hilo, nani kasema kila mtumishi anayeomba uhamisho anagushi vyeti viwe vya hospitali ama ndoa?Uko sahihi, ila ile tabia ya kumpa daktari pesa ili amuuzie mtu ugonjwa ili apewe uhamisho kwa urahisi siitaki katu.
Wengine mpaka vyeti feki vya ndoa walivichonga na kupata uhamisho.
Rushwa kwa ma H.R, wakurugenzi, makatibu tawala zilikuwa nyingi.
Nakumbuka nikiwa Lindi miaka kadhaa nyuma watumishi walikuwa wanafanya Lindi kama chaka la kupatia ajira tu halafu wanaanza kusaka uhamisho kuja Dar, Arusha na Mwanza hasa watoto wa vigogo wa TRA.
Bora uhamisho usiwepo tu hasa ule wa kuomba.
Afisa wa PCCB Lindi alihama baada ya kutoa rushwa.
Hali hii ndo ilipelekea baadhi ya maeneo kuwa na upungufu wa watumishi wa umma.
Kweli bwana kuhama ni haki ya mtu. Jamani mimi natafuta mtu wa kubadilishana kituo cha kazi kada ya Afisa maendeleo ya jamii aje kanda ya kaskazini mimi niende kanda ya ziwa.Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akijibu hoja za wabunge, hasa la uhamisho wa watumishi wakiwemo wanandoa wanaotenganishwa, alikemea tabia ya maofisa watumishi kuzuia wenye ndoa kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwa lengo la kuwafuata wenzao.
Alisema kuwazuia ni kuwanyima haki ya msingi, na kuwaagiza wabunge katika maeneo yao wasaidia kusimamia haki za watumishi.
"Lazima sheria za utumishi zizingatiwe, walimu hawa au watumishi wanayo haki ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini pia kuishi na wenza wao, lakini utadhani mtumishi anapoomba ni kama anasaidiwa, hapana ni haki yake ya msingi, waheshimiwa tusimamie haki za watumishi,” alisema Simbachawene
We endelea kusubil bob wenzio wanahama kama kawaida.. Hii nchii dili bado zinapigwa kama kawaidaKwa takribani mwaka mzima uhamisho kwa watumishi wa umma umezuiliwa. Kwa kuwa haijulikani ni lini utaruhusiwa, mimi nashauri ni bora kwa wale walioomba kuhama kwa sababu za kiafya wakahamishwa tu ili kuongeza tija kazini.