CHIMBULI WA CHIMBULI
JF-Expert Member
- Jan 10, 2013
- 468
- 160
Habari wanajamvi,
Kwanza ningependa kudurusu maneno maarufu ya wimbo wetu tukufuuu wa " CCM mbele kwa mbele unasema, "CCM ni ile ile oooh! ni ile ile! wataisoma namba."
Sasa mwaka na kitu umepita maisha ya wananchi wengi ni magumu sana toka wapate ridhaa kwa mara nyingine. Kazi nyingi ni za kijungu jiko na ile kaulimbiu ya HAPA KAZI TU kwa sasa haitumiki kwani kazi zilianza tangu enzi za mababu zetu tatizo hapa ni tija katika kazi.
Mbele kwa mbele ya CCM haionekani badala yake kuisoma namba kwa wananchi ndiko kuko dhahiri na ukilalamika wewe ni mpiga dili hata kama hujui hizo dili. serikali imeshindwa kuajiri waalimu wapya Huku ikijaribu kuwanyanyasa wa Sanaa, ilhali wengi wa viongozi wamesoma hayo masomo, .madaktar, manes na kada zngne ajira ni kizungumkuti.
Uchumi wa viwanda hauwezi kufanikiwa kama kilimo bado hakitopewa kipaumbele kwani zaidi ya 80% wanategemea kilimo. CCM haionekani kuwa suluhisho la kweli. Hata zile takwimu za TRA hazionyeshi impact yake watu wanajiuliza serikali imekumbwa na nini? Mbona tunaenda mbele kama tunarudi nyuma? Tunaipenda Tanzania. CCM ijitafakri upya.
Karibuni kwa mjadala.