IGUDUNG'WA
JF-Expert Member
- Oct 22, 2011
- 2,071
- 1,316
Habari.
Nimekuwa nikitumia kitua tajwa hapo juu kama kituo changu cha usafiri kuondoka kurudi home baada ya majukumu yangu ya siku nzima.
Kinachonikera kituoni hapo kunakuwa na rundo kubwa sana la mateja ambao wamekuwa wakifanya kazi ya kupiga debe kama geresha lakini kubwa wafanyalo ni kuwaibia abiria hasa kwenye daladala zenye msongamano wakati wa kupanda.
Wahanga wakubwa katika uharifu huu wamekuwa ni watanzania maskini hasa wanaotoka mikoani. wanaibiwa sana simu pamoja na pesa. mateja hawa wamekua jasiri kiasi kwamba anaiba hadharani kabisa bila uoga wowote. jambo hili huwa linanikera sana kiasi kwamba leo nusura nizichape nao baada ya kuokoa simu aliokuwa ameichomoa toka mfukoni mwa kijana aliekuwa anahangaika kugombania daladala.
Nimefikia mpaka naandika haya kwa hasira kwa sababu siku moja nilipoteza vitu vyangu hapo ubungo darajani nikaenda kuripoti kituo cha polisi urafiki. wakati naandikisha maelezo nilistaajabu kukuta mateja kibao na maarufu ya ubungo yamo selo,nikajipa moyo kuwa afadhari yamedhibitiwa. haikupita hata siku 3 nayaona yanadunda viunga vya ubungo.
Mara kwa mara polisi wa kituo cha urafiki wamekuwa wakifanya ambush kituoni hapo wanakamata wachache kwani wengi hukimbilia chini ya daraja. lakini hata wanaokamatwa huachiwa kwa madai kuwa mateja huchangishana pesa kisha kwenda kuwatoa wenzao. Juzi jumamosi tarehe 11.06.2016 mida ya saa kumi jioni nilishuhudia landcruiser pick up likiwa limesheheni askari polisi kibao wakifukuzia kuwakamata mateja hao huku wakiwa wametanguliza mbele vijana kibao wa polisi jamii na matshirt yao meusi yenye chata mgongoni Expendable team. sijui walikamata wangapi siku hiyo maana uhalifu umeendelea mpaka leo.
Swali langu kwa askari polisi urafiki ni hili je ni mpaka lini mama zetu,kaka zetu,baba zetu,shangazi zetu toka mikoani wataibiwa na hawa mateja?simaanishi kuwa wanadar es salaam hawaibiwi wanaibiwa pia.
Je polisi hawa wanasubiri mpaka tena magufuli aseme ile kauli yake kuwa polisi wapo,mkuu wa wilaya yupo,rpc yupo, ocd yupo niongeze nyingine Meya wa manispaa yupo ndo watachukua hatua?
Hawa mateja ni moja ya watu aliotaka magufuli wakajisaidie gerezani sasa ajabu watu wamefanya mitaji yao pindi wakifulia wanawakamata wanapiga hela wanaachia. Huenda comrade Mwigulu Nchemba akawaamsha hawa askari wetu wanaoacha tuteseke na mateja.