Naandika ili kama taasisi hizi wanapita hii forum wajue utata wanaosababisha - Rita, heslb pamoja na TCU.
Leo nimeenda kuhakiki cheti cha kuzaliwa binti yangu wilayani wakaniambia nikipeleke kule waliokitoa, ni mbali sana (wakati huo nilikuwa nafanya kazi huko, sasa nimehama) wakasema kama siyo nikitume Rita kwa email.
Wakati huo walikuwepo vijana wanalalamika wana wiki tangu watume na hawajajibiwa. Kwa mini inakuwa hivi, kama mtu alizaliwa na kupata cheti Iringa na sasa hivi yuko Kagera, aende kweli Iringa?
Kwanini mwaka huu usumbufu wa kuomba vyuo umekuwa mkubwa hivi tofauti na mwaka huu.
Gharama za kuomba kila chuo ziko juu, baadhi ya vyuo 50,000 vingine 30,000 vingine 10,000. Ukiomba vyuo 4 jiandae na 200,000.
Rita nao wanataka 3000, mahakama kuweka mhuri 5000 kila sahihi. Bodi ya mikopo 50,000.
Kweli tutafika?