Uhaba wa Vipaumbele "Priority" katika Taifa na ubovu wa mbinu "Aproach" za kutekeleza mambo katika Nchi.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Ukiondoa UHABA mkubwa wa kitu kinachoitwa Kipaumbele "Priority" katika nchi yetu ya Tanzania, Kwa miaka mingi Tanzania imekumbwa na UBOVU wa kitu muhimu kinachoitwa mbinu za kufanikisha jambo flani "Approach".

Kila jambo hasa linalohusu maslahi ya nchi linalotendeka katika nchi basi aproach yake ni mbaya na mara nyingi limekuwa likifeli mbeleni na kulitia hasa taifa ama kudumaza fikra na maendeleo ya watu katika nchi. Baadhi ya mambo yamekuwa yakitendeka ambayo hayana maslahi kwa taifa zaidi ya kikundi cha watu wacheke wanaonufaika kisiasa.

Mfano wa mambo yasiyo na maslahi kwa taifa yanayotendwa na serikali ni kama haya ya kuzua shughuli za kisiasa ambazo zinatambuliwa na kulindwa kikatiba na kisheria, Kuzua madai ya katiba mpya, Kumbambikia Mbowe kesi ya Ugaidi. Kitendo cha serikali kuyatenda haya mambo ni kulihujumu taifa kwa maslahi ya kikundi cha watu wawili au watatu tu ambao wanapuuza haki za watu na maslahi kwa taifa.

Mfano wa Mambo muhimu kwa taifa ambayo aproach yake ilikuwa mbaya na matokeo yake yakawa hasi, Urais wa Rais Samia na maongozi yake. Maongozi ya Rais Samia awali kinadharia yalionyesha mwanzo mwema, yes ilikuwa ni good aproach pale alipoanza kuyashika madaraka. Baada ya kikao cha kamati kuu ccm Dodoma mwezi May 2021 ambacho ndicho kilikamilisha ushikaji rasmi madaraka kisiasa, Aproach ya kwanza mbaya ilijitokeza, na hili sio la bahati mbaya, Ni real ccmlism halisi. Ccm haijawahi kuwa na Aproach nzuri kwa taifa.

Kauli ya kwanza ni shughuli za kisiasa zisubiri ujengwe uchumi, kauli hii ilionyesha rasmi kuwa Rais Samia anapingana na kauli yake ya awali kuwa anakusudia kukutana na vyama vya siasa ili kujadili mstakabali mwema na mwanzo mpya wa siasa za nchi hii, ikizingatiwa kuwa vyama vilikuwa kifungoni kwa miaka mitano, hoja ya uhuru wa kisiasa ilikuwa ndio mojawapo ya hoja kuu za kikao tajwa na rais.

Kauli ya pili tata kwamba Katiba Mpya isubiri ajenge uchumi, hii pia ilikuwa ni majibu tosha ya kuwa hakuna kikao tena kati ya Rais na vyama vya siasa. Yes kimaandiki vyama vya siasa agenda yao kuu katika dhamiri ya kukutana na rais ilikuwa ni Katiba Mpya. Sasa Rais akaijibu nje ya miadi ya mkutano husika, je nini kingejadiliwa tena ikiwa tayari Rais ameshaweka msimamo wake na ifahamike kuwa huu ndio msimo wa ccm.

Aproach mbaya kabisa, Katika kukazia misimamo hiyo miwili Rais na chama chake, Serikali ya Rais Samia Ikambambikia kesi ya Ugaidi Kiongozi wa Upinzania nchini akiwa anaongoza kampeni za kudai katiba Mpya. Izingatiwe kuwa kinachoitwa kesi ya Ugaidi ni zilezile hujumu na vurugu alizokuwa anafanyiwa Mbowe nyumbani kwake na Lengai Ole Sabaya aliyekuwa DC wa Hai.

Katika utawala wa Rais Magufuli Mh Mbowe alivamiwa mara kadhaa nyumbani kwake Dodoma na Moshi na jambazi Sabaya akitumia magari ya namba za usajiri za UN akaharibiwa mali nk, walinzi wake wakatekwa wakapigwa na kudhalilishwa, Yeye akavungwa miguu yake na kutembelea viti vya wangonjwa kwa miezi kadha, Haikutosha akavamiwa hotelini kwake Moshi wakatekwa walinzi wake wakabambikiwa kesi ya Ugaidi enzi za Magufuli, Hakuna aliyewahi kukanatwa kwa mavamizi hayo ambayo tafsiri ya kisheria Mbowe alifanyiwa ugaidi halisi na serikali ya Magufuli chini ya CCM.

Serikali mpya hajawajibika kushugulikia kuwachukulia hatua waliomfanyia ugaidi wa kutisha Mbowe, Badala yake leo katika kuzima madai ya Katiba Mpya, Serikali ya Rais Samia amerithi matendo ya Rais Magufuli dhidi ya Mbowe, Leo Serikali ya Rais Samia imemfikisha mahakamani Sabaya kwa madai mazito ya ujambazi utakatishaji na uhalifu dhidi ya binadamu, mtu huyu huyu ndie aliyewabambikia kesi Walinzi wa Mbowe ambapo serikali hii ya Mama Samia imemuunganisha Mbowe na kesi hiyo ya kubumba kama nyenzo ya kuzima mjadala wa katiba. Hapo ndipo dhana ya hoja yangu kwamba nchi yetu imekosa Priority na Best Aproch inaposimamia.

Wakati wa Utawala wa Magufuli kwenye saga la Makinikia niliandika makala hii nchini nikionya kwamba aproach yetu katika ishu hii itafeli huko mbeleni na tutakwama. Lakini kwakuwa siasa ilikuwa nanguvu kubwa kuliko utaalamu, Wapambe wa utawala ule walikomaza sana shingo. Implementation ya kile nchi ilikubaliana kikoje leo? Jibu liko kwa Mh Lissu Ubelgiji akiuguza makovu ya uzalendo wake kwa taifa. Nyimbo za mabeberu na dhihaka zingine ziliishia chato na sasa tunawakaribisha sana.

Naomba uisome hapa chini makala hii niliyoandika July 30, 2020.

"Katika mambo yanayonifikirisha zaidi tangu siasa za makinikia zianze, ni namna ya majadiliano baina ya makampuni ya uwekezaji toka Ughaibuni na Serikali ya Tanzania, Kitendo tu cha kufikia katika majadiliano mezani ni heshima kubwa kwa Nchi yetu.

Ninafikiri kwa kina sana, ninaitafuta diplomasia ya kiuchumi katika uzao wa ardhi yangu, ninamuangalia mkuu wa sheria nchini Prof Kabudi, ninawaangalia waambata wengine mnasaba wa mjadala huu, ninafika mbali sana, ninaifikiri tabia ya utanzania wetu, ndio ni hiihii tuiishiyo, hii tunayoweza kugeuza moja kuwa elo na kumi kuwa loo.

Kwa wageni nafikiria sana ugwiji wa marehemu Creg Wilkins aliyewalea akina Jayson Myers na Newt Gingrich, hawa ni watu ambao mnasaba wao hauna mfanowe, wao wanazungumza lugha za kibiasha zote tatu ulimwenguni, yani diplomasia ya uchumi, ujasusi wa kiuchumi, sheria ya biashara na mikataba ulimwenguni. Kwalugha rahisi hawa mabeberu akina Newt Gingrich na wenzao huitwa ( the best Business negotiators). Na sio hawa wetu politic-tor stomach.

Ninauona mchakato mtamu sana wenye kila aina ya mbinu mtambuka, ninamwamini sana mwanamedani Daktari Mahiga, lakini nafikiri mchezo utaamuliwa mshindi pale mezani Paris mahali pa pilato wa kibiashara ikiwa ni matokeo ya Dar es Salaam kushindwa kuzaa matokeo chanya.

Ninawaangalia mumiani waliopo nyuma ya Barick Gold Mining, ambao ni George Herbert Bush, Adnan Khashogg, Peter Munk na Brian Mulroney. Kwahakika si vita ya ACACIA, bali ni vita ya CIA na Pentagon, ni vita ya M16 bila kusahau ubwa wa Toronto Canada. Vita kwelikweli ambayo tukiendelea kuzibeba siasa za kijinga za Dar huku ndoto za mang'amung'amu zikitupeleka 2020, kwahakika matokeo tayari tunayo mkononi.

Wenzetu nchini Chad walijaribu kuwatikisa kamouni ya ExxonMobil kupitia mahakama zao, kufumba na kufumbua wakawekewa kisu shingoni, matokeo yake wameipa kampuni ile kuchimba mafuta mpaka mwaka 2050 na hawasemi tena kuwa wamelipwa au wanawadai.... Mzungu ni mshenzi, alijipa nusu ya uungu hapa duniani, lakini mimi Mtanzania ni mshenzi zaidi ya mshenzi.

Ninaungana na nguvu ya kidiplomasia toka Dar es Salaam, ninalaani kama siasa zitajitwalia utukufu, Ninafikiri kwamba, kusudi la mwenye heri moyoni ni tunu kwa Tanzania ya leo na kesho. Vita usiyojiandaa umeshindwa kabla ya vita, Ushindi dhidi ya mjadala huu ni ushindi wa Tanzania, kushindwa kwa Mjadala huu ni kushindwa kwenu. Bahati mbaya sana uongo wa watawala ni baraka za kiutawala na laana kwa watawaliwa.

NB: Picha chini ni wajumbe wa Barick Gold Mining (ACACIA) wakipokelewa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof Kabudi tayari kwa meza ya majadiliano..."

Na Yericko Nyerere
IMG_20210731_123021_056.jpg
 
Back
Top Bottom